Davion Delmonte Jr.
JF-Expert Member
- Oct 27, 2013
- 2,149
- 1,718
Katika nchi maskini kama Tanzania naamini kabisa kiongozi hatakiwi kufanya decision bila kutizama hali halisi ya wananchi. Mfano katika siku za karibuni kumekuwa na maamuzi ambayo kwa kweli ni magumu hasa ukizingatia yanagusa moja kwa moja tabaka la wananchi wa ngazi ya chini.
Mfano tu kuna hili suala la bomoa bomoa ambalo naona kama limeshika kasi. Nisingependa kukosoa kwani kuna sababu stahiki za bomoa bomoa lakini wasiwasi wangu ni kwamba zoezi linaenda katika hali ambayo kwa namna moja inawaacha raia walengwa katika ugumu fulani wa maisha.
Ningetoa Rai yangu kwa Magufuli na watekelezaji sera wake " Hii ni Tanzania na ni moja wapo ya nchi masikini ambayo pia raia wake wengi hawana elimu kwa hiyo basi ingepaswa maamuzi kama haya yawe yanawashirikisha walengwa badala ya kuvamia tu na matingatinga na kuanza kuvunja nyumba za raia"
Mh Rais hii nchi yetu bado changa na huwezi tu ukafuata sheria bila kuangalia uhalisia wa maisha ya wananchi. Hapo tutakuwa hatujengi bali tunabomoa. Naelewa vema azma yako ya kuipatia maendeleo nchi hii lakini kuna sehemu nyingine lazima tuende kwa speed ya ki pwani pwani maana tukienda kwa speed ya ki London London ni wazi utaumiza wengi.
Hata hii hatua ya kubomoa nyumba za watu zenye thamani kubwa na mahoteli kwa dhana kwamba eti wamejenga kwenye viwanja vya wazi hilo nalo nna mashaka nalo maana jenzi zozote zinapata vibali kutoka halmashauri husika. Kwa hiyo kama ni tatizo saa nyingine halipo kwa raia bali kwa watendaji wa serikali wenyewe.
Mi sitaki kuamini kuanza ku deal na bomoa bomoa kwa kipindi hiki kutanufaisha wananchi walio wengi. Nadhani kuna mambo mengi ya kufanya kwa sasa. Hata na hivo bomoa bomoa haikuwa kwenye ilani ya CCM.
Halafu tangu uchaguzi uishe naona harakati za kisiasa na kazi za serikalini ni Dar es salaam tu, ina maana mikoa mingine sio sehemu ya Tanzania? Mara muhimbili hospital mara sijui wap wap.. yaani Dar tu. Tabora nayo ni Tanzania na kuna shida nako kweli kweli..
No offence,, namkubali sana Rais ila kuna mambo yananipa ukakasi na lazima niandike.