Naam yametimia

ngozimbili

JF-Expert Member
Jul 28, 2011
1,398
1,006
Viashiria vyote vya kuonyesha kuwa taifa letu limeshaianza safari ya kuelekea kwenye Maangamizi yake yenyewe imeshaanza, kwa hakika watu wema walikwishatuonya kwa namna tunavyoendesha nchi lakini sikio la kufa.

Ufisadi umetamalaki kila mahala ambao kama ilivyo ada ukazaa ugumu wa maisha kwa mwananchi wa kawaida huku watawala wakijenga ghorofa la michuzi kuelekea angani.

Mara ukaja mchakato wa katiba kama suluhisho la uendeshaji mbovu wa taifa letu, wananchi wakahamasika wakatoa maoni tuwe na maadili ya uongozi mikataba iwe wazi kusiwe na usiri.

Viongozi wawajibike kwetu na siyo kwa vyama wakayatoa ya moyoni masikini Mzee Warioba kayaandika kayaweka kama walivyotaka wananchi.

Kumbe amepiga Ikulu ya watawala wote waliokuwa na ugomvi wakaungana Warioba mbaya sana huyu Mzee anazeeka vibaya.

Mara wimbo ukadakwa na wapambe, Warioba mbaya anazeeka vibaya ukiuliza ubaya wake nini mbona yeye anajenga hoja na nyinyi jibuni hoja kimya, wanakung'uta nguo hao kwa mbali nasikia wanaimba Warioba mbaya.

Nikaona ngoja nimsikilize kwa makini Mzee sasa watawala with busara zipo likizo ya muda mrefu badala ya kujibu hoja hata za propaganda hawawezi, wakati bado watu kumbukumbu ya kuchakachuliwa theluthi 2 ya bunge la katiba wanatuma watu kuleta fujo kwenye midahalo kwa maana nyingine wanafungua mzinga wa nyuki.

Wanasahau kuwa upande wa pili una hasira zaidi na una watu waliopinda zaidi kiasi kwamba mapambano ndiyo maisha yao na kwa hiyo kwa kuunga mkono yaliyotokea jana ni kwamba wameruhusu matumizi ya nguvu katika siasa, sasa tusubiri siku wao watakapozungunza na wananchi.

Naam yametimia ni Warioba kuliko MTU mwingine yeyote ndiye anaeliporomoa ghorofa la michuzi la watawala.
 
Shillingi ina pande mbili, mbona unaangalia pande moja tu, kulikoni?
 
Tutaendelea kwenda kwenye mijadala na sisi tumeshaelewa watumeni tena tutakutana nao na mauwaji yataanzia hapo ndo mtambue kualibika kwa nchi pumbavu nyie,mzee wetu walioba kwa sasa utalindwa na vijana us tie Shaka
 
Rais aliwadhalilisha wajumbe wa Tume ya Katiba siku ya kuzindua Bunge la Katiba. Makonda hana platform ya kuwatukana kama aliyonayo Rais. Makonda ametekeleza kile kilichoanzishwa na Rais.


Chanzo cha haya yote ni JK
 
Shillingi ina pande mbili, mbona unaangalia pande moja tu, kulikoni?

Huwezi kujua thamani ya sarafu kwa kutazama upande wenye picha ya mtawala, lazima ugeuze upande mwingine ndiko kwenye maandishi ya Thamani ya sarafu husika.

Mwandishi yuko sahihi, upande wa watawala ni kuuza sura tu lakini nguvu ya sarafu iko upande wa pili wa sarafu. Jifunze kutoka Burkina Faso!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom