Mzunguko wangu wa siku za mwezi unanichanganya

Miss Natafuta

JF-Expert Member
Sep 16, 2015
26,582
48,737
Hapo mwanzo nilikuwa na mzunguko wa siku 28, siku hizi kila Tarehe 23 ya mwezi mpya ndo naanza kuona siku. Tarehe 23 hadi 23 nyingine ni siku ngapi? Na je ni mzunguko mzuri?

Maana naogopa isije ikawa uzee ushanifikia hadi kwenye uzazi mwenzenu naogopa sana sijazaa bado.
 
umezidi maigizo

nadhani una msongo ama stress za maisha. unaonyesha namna gani una u pessimist. kwako wewe kila kitu kibaya mara unene hupendi, hupendi wanaume, upendi mapenzi upendi upendi upendi kila kitu na bado unapendi. mwisho wa siku utakuwa mwendawazimi.

do not think loud.... enjoy your life be optimist you will enjoy hakuna binadamu malaika na hata wale malaika wazuri walibadilika na kuwa mashetani
 
huna matatizo mamy .. wengine hubadilika badilika lakini mambo safi .. ila acha kuwatusi wanaume wakupende ha ha hahaha .. wapende mahaba niue kubali kufa,....... ila pesa nayo uangalie iwepo
 
Ninahisi Kuna watu wengine humu JF au wanaogopa sindano au kuna matatizo yao hawapendi kupeleka sehemu husika. Hili tatizo lako sio la kuliweka wazi wazi namna hii. unaweza kuwauliza hata wanawake wenzako kuliko kutupa jiwe gizani. Wapo watakushauri wapo lakini nenda sehemu sahihi yaani Hospitali. Anyway linaweza kuwa tatizo kubwa na likaendelea na kuendelea.
 
kwani hapa kuna shida gani?
 
Umebadilisha mazingira?

Ulisafiri kwa muda mrefu na sasa umerudi ulipokuwa ukiishi kabla?

Unatumia dawa zozote za uzazi wa mpango? (hii ni pamoja na morning after pills)

Umefanya ngono siku za karibuni (kabla ya mabadiliko hayo ya tarehe, na huenda ilikuwa ngono zembe hata kama ulikuwa siku salama)?

Huu mzunguko mpya umeupata kwa muda gani sasa?
 
Generally mzunguko kubadilika sio shida au tatizo la kiafya hasa kama baada ya mabadiliko umebaki constant.

Huenda unaposema menopause - hapa nawaza huenda uko 34ish kuendelea - na labda (R) labda huenda ni dalili. Ingawa siikubali hii sana maana ingekuwa menopause ungekaa mwezi mmoja usipate, mwezi ujao upate, au zipishane tu bila kuwa na tarehe maalumu.

Anyway, ni vyema ukafanya taratibu za kuonana na daktari umuelezee hofu yako. Wakati mwingine unahitaji tu mtu wa kuongea naye na kukusikiliza. Hata asipokupa dawa...nakushauri uende kumuona daktari wako umpendaye. Usiende kwa wale madaktari ambao tangu unaingia hadi unatoka yeye macho yako kwenye karatasi mezani. Nenda kwa dokta mwenye kuijua fani yake na anayejua kutibu ni zaidi ya kuandika.

All the best.
 
umezidi maigizo

nadhani una msongo ama stress za maisha. unaonyesha namna gani una u pessimist. kwako wewe kila kitu kibaya mara unene hupendi, hupendi wanaume, upendi mapenzi upendi upendi upendi kila kitu na bado unapendi. mwisho wa siku utakuwa mwendawazimi.

do not think loud.... enjoy your life be optimist you will enjoy hakuna binadamu malaika na hata wale malaika wazuri walibadilika na kuwa mashetani
 
Umebadilisha mazingira?

Ulisafiri kwa muda mrefu na sasa umerudi ulipokuwa ukiishi kabla?

Unatumia dawa zozote za uzazi wa mpango? (hii ni pamoja na morning after pills)

Umefanya ngono siku za karibuni (kabla ya mabadiliko hayo ya tarehe, na huenda ilikuwa ngono zembe hata kama ulikuwa siku salama)?

Huu mzunguko mpya umeupata kwa muda gani sasa?
kuhusu mazingira sijabadili mkuu!wala sijasafiri .pia situmii dawa zozote za uzazi maana sifanyi mapenzi na yoyote
kuhusu ngono sijafanya kitambo sana mkuu almost yrs!
 
kwani hapa kuna shida gani?

Aaaaaaah! Dada yangu Mambo mengine yanahitaji staha. Bado sisi waafrika. Mboma tukijaribu kufungua mikoba yenu mnatukemea kwamba tutakuta vitu visivyotuhusu hii huwa mnamaana gani. Staha/Heshima na maadili. Sio Vibaya mtu kufunguka mambo yao ya SIRI lakini tunamuangalia kwa jicho la tatu.
 
Back
Top Bottom