Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,811
Kwa wale wasiofahamu maana ya Dogma, Kamusi ya Kiswahili inatafsiri Dogma kama fundisho la Imani lisiloweza kukanushwa kamwe na wafuasi wa hiyo Imani. lkn pia linaweza kutumika kwa maana isiyo ya kidini kama vile ninavyotaka kuitumia hapa!
Mambo mengi sana ambayo tunayafanya, tunayafanya tu kwa sababu Mzungu alituambia kwamba aidha tufanye au tusifanye, na hapo tunakuwa vipofu kabisa na hakuna aliye tayari hata kuhoji sababu za kwa nini jambo fulani Mzungu alituambia tusilifanye na kwa nini jambo lingine alituambia tulifanye yaani ni Dogma!
Mifano iko mingi sana ambapo mambo mengi ambayo kabla ya kuja Mzungu tulikuwa hatuyafanyi lkn alivyokuja Mzungu akatuambia hili linapaswa kuwa hivi basi ikawa ni kama Dogma kwetu na tunafikri hivi ndivyo Dunia inavyopaswa kuwa na anayefanya kinyume na hivyo basi amepotoka hata kama jambo ambalo Wazungu wenyewe waliotufundisha wameshaliacha kwa maana wameona halina maana lkn sisi bado tunaling'ang'ania!
Kwa mfano viboko Shuleni, kuchapa watoto wa Kiume matakoni na wa Kike mikononi hii aina ya adhabu ambayo tulikuwa hatuijui kabla ya ujaji wa Mzungu, Mzungu akaja akatufundisha kwa kuwa hata huko kwao zamani ilikuwa ni kawaida sasa Mzungu kaondoka huko kwao wameshaipiga marufuku lkn hapa nyumbani ukitaka ugombane na mtu ongelea kuhusu kufuta adhabu ya viboko ingawaje kila tafiti za hao hao Wazungu waliotufundisha hii adhabu zinaonyesha kwamba kumchapa mtoto hakumsaidii bali kuna muharibu, lkn kwa kuwa alichotufundisha Mzungu ni Dogma hapa na Mwafrika mtakesha na somo haliingii!
Ukija kwenye kwa mfano ishu rahisi kama usafirishaji wa Wanyama kwa kuwa Mzungu alisema inatupaswa tulinde na kuwatunza Wanyama waliopo porini basi imekuwa Dogma mtu anamuona Twiga au sijui Tembo kama vile Mungu wkt ni Mnyama tu!
Kabla ya Wazungu kuja tulikuwa tunaishi na hawa Wanyama kama majirani na hata Wamasai ni kama utamaduni wao kuuwa Simba au wanyama wengine wa porini lkn Mzungu alikuja baadaye akawakuta wanyama wote wapo lkn akatufundisha jinsi ya kuwatunza kama tungekuwa hatujui kutunza Wanyama wetu Mzungu si angekuta wameisha? Ni kwa nini amewakuta ingawaje tumekuwa tukiwawinda na kuwaua maisha yetu yote?
Leo hii kwa sababu ya Dogma aliotuachia Mzungu tunashindwa hata kutumia common sense ndogo sana, mtu anashindwa kuelewa kwamba tunaweza tukauza Twiga 10 nje tukazalisha 20 au 50, ona sasa ishu ya kuuza Tumbiri inafukuzisha mtu kazi kwa nini?
Kwanini hata tunajadiri kuhusu Tumbiri? Ni kwa nini tusifanye utaratibu wa kuwakamata na kuwauza nje kama export na hizo fedha amabzo tunazihitaji kwa mfano kujengea madawati au Shule? Halafu tukafuga tumbiri wengine wengi tu, unaweza kwenda Misitu ya Mabwepande ukazalisha hata Tumbiri 1000 ukitaka au twiga 100 hiyo ni kazi rahisi sana!
Na kwa wale wasiofahamu tu, Kwa Bonde la Ngorongoro lilianzishwa kama Shamba la Wazungu walowezi na Wazungu walikuwa wanakamata hawa wanyama na kuwauza kama export Dunia nzima na kuzalisha wengine mara mbili yake na hizo fedha ndizo walizojengea baadhi ya Miji kama Arusha ni vitongoji vyake lkn sisi leo hii tunamuona Tembo kama vile Mungu, angalia Afrika Kusini Wazungu wanakuja wapiga risasi Tembo wanalipa fedha wanaondoka, mbona Tembo wako wangi mpaka wamezidi? lkn AK ni Wazungu ndiyo maana wamebadilisha waliachoambiwa!
Sasa tofauti na Wazungu utaona nchi zote za Kiafrika kwa mfano mpaka leo hii Majaji, Maspika wanavaa wigi kichwani kama Uingereza hiyo nayo ni Dogma ukimuuliza Mwafrika kwa nini Majaji wetu wanavaa wigi? Mtabishana mpaka kesho atakwambia sisi ni Jumuiya ya Madola na ni Utaratibu kuvaa kwa sababu ya common Law blah blah lkn kama ni hivyo ni kwa nini Australia ambao ni Wazungu wenyewe Waingereza au New Zealand hata AK hawavai wig wkt ni Jumuiya ya madola na wanatumia common law na tena Mkuu wa nchi zao ni Malkia wa Uingereza?
Sasa unajua ni kwa nini? Ni kwa sababu Mzungu ana challenge Dogma na ndiyo maana wameweza kuendelea!
Ndiyo maana nilimsifu sana Mkuu wa Dar Mkonda alivyo challenge dogma na kufuta utaratibu wa PF3 kituo cha Polisi na kuupeleka Hospitalini, aina hii wa ufikiri ndiyo tunayohitaji Waafrika, kufikiria nje ya box!
Hivyo mimi kwangu bila ya kubadilisha Dogma hapa Afrika hatuwezi kuja kuendelea kamwe, kwani ikumbukwe kwamba sababu hasa za Wazungu hata kutukataza kufanya jambo fulani wakati huwo ilikuwa siyo kwa manufaa yetu bali ilikuwa ni kwa manufaa yao na hiyvo kuendelea kufwata na kutii walichotufundisha ni kuendelea kuwanufaisha na ndio maana mpaka leo hii export ya chai yote inaenda Uingereza hakuna mtu anayeweza kufikiri nje ya hapo kwamba kwa mfano Ujapani wanapenda Chai na ni matajiri klk Waingereza hivyo kwa nini tusiuze kule, hapo Mwafrika hatakuelewa, chai yetu lazima iende Uingereza!