Mzungu mgeni anayesema sheria ya mitandao haifai anatukana bunge, rais na wapiga kura

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,902
51,992
Sheria ya mitandao ilipitishwa na wabunge walio wengi kwenye bunge lenye wabunge wa upinzani na chama tawala.Wabunge hao wamechaguliwa na wananchi wafanye hiyo kazi kwa niaba yao.Na raisi aliyechaguliwa kwa kura za watu wengi akaisaini kuwa sheria baada ya kupelekewa na bunge.
Na ikishapitishwa kinachofuata ni utekelezaji.

Sasa akija mzungu akasema haifai ni kutukana wapiga kura waliochagua wabunge na raisi na kutukana bunge kuwa ni BOGUS limepitisha kitu ovyo na kutukana Raisi aliyesaini kuwa naye ni bogus.

Hiki kitu kusemwa na mgeni si cha kuvumilika.Sheria za nchi hutofautiana kati ya nchi na nchi .Kama tungekuwa tunashupaliana na sisi tungewakomalia kuwa sheria za kuruhusu ushoga na usagaji ni bogus.Wangeturukia kuwa tumewatukana wapiga kura wao na bunge lao.

Hawa wazungu tufike mahali tuheshimiane tafadhali.Mimi nashukuru sijawa raisi ningekuwa kwenye mikataba ya gesi, mafuta na madini ningeweka kipengele kinachotamka wazi kuwa kama nchini kwako umepitisha sheria ya kuruhusu ushoga na usagaji na ndoa za jinsia moja sikupi kisima cha gesi,mafuta wala shimo la madini hadi ukarekebishe hiyo sheria huko kwenu.Tukifanya hivyo hapo tutaenda sawa wao watataka turekebishe sheria ya mtandao na wao wakafute sheria zao za kuruhusu usagaji na ushoga na ndoa za jinsia moja ili wapate watakacho
 
Mkuu,
Unataka tujadili nini hapa? Anyway title na contents mbona haziendani?

Sheria hii kandamizi, tumeipinga toka mwanzoni mwa mswaada, kama ulikuwepo hapa. January akaanza kuruka ruka tu.

Lakini pia JF Media ipo mahakama kuu kupinga sheria hii.

Unaweza kuwa na hoja ila hujajipanga.
 
Back
Top Bottom