Mzungu apiga risasi watu 9 Kanisani Marekani

Elungata

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
40,343
Reaction score
33,507


Source: Nine Dead in Shooting Rampage Inside South Carolina Church; Gunman at Large
 

Attachments

  • 29BA4BC900000578-3129109-image-a-117_1434605395621.jpg
    62.4 KB · Views: 5,890
Elungata
Polisi katika jimbo la South Carolina nchini Marekani wanamsaka mtu mwenye silaha alihusika katika shambulio katika Kanisa la Methodist lililo katika eneo la Charleston.
Habari ambazo bado hazijathibitishwa kutoka vyombo vya habari vya eneo hilo zinasema kumekuwepo na vifo kadha.
Polisi huko Charleston wanasema mtuhumiwa ni mzungu mmoja akiwa katika umri wa miaka ya ishirini.
Shambulio hilo limefanyika katika Kanisa la Emanuel African Methodist Episcopal Church, moja ya makanisa kongwe ya Waafrika Wamarekani nchini Marekani.
 
Last edited by a moderator:
Mzungu mmoja huko Marekani amewapiga risasi Wamarekani 9 ambao ni weusi na wenye asili ya Afrika wakiwa kanisani kwenye ibada!

Hili tendo na mengine mengi kama kupigwa risasi na polisi bila hatia n.k linatufundisha nini sisi kama Waafrika na watu weusi?

Ni kwamba Mzungu hata siku moja hawezi kumpenda mtu mweusi mwenye asili ya Afrika kwa maana kama ni rangi hata India ni weusi lakini Mzungu hawezi kuwapiga risasi Wahindi!

Tutajipendekeza tunavyotaka, tutaongea Kiingereza kama wao tunavyotaka, tutawachukia Waarabu kwa kuwa tu ni Waislamu na kuwapendelea Wazungu kwa kuwa wao ni Wakristo na sisi tunajiita Wakristo au kinyume chake, lakini mwisho wa siku kwa Mzungu mtu mwenye asili ya Afrika ni wa mwisho kabisa.

Na haijalishi kama umejipa jina kama lao ukifikiri ya kwamba watakuthamini kwa kujiita Wilbrod, Agustino, Bernard, Freeman, au sijui Julius na Charles, Edward au Mark kwa Mzungu wewe ni mnyama tu anayestahili kuwindwa na kupigwa risasi!

Kwanini huyu Mzungu hajaua Waarabu Waislamu? Ni kwa sababu ukimwambia Mzungu achague Mwafrika Mkristo na Mwarabu Muislamu atachagua Mwarabu Muislamu na huo ndio ukweli!

Hata watu Waafrika mnaojiinginza kwenye ugomvi usiowahusu kuhusu Wapalestina na Waisraeli, ukweli ni kwamba wote Waisraeli na Wapalestina ni bora waishi wenyewe kuliko waishi na Mwafrika mweusi!
 
Wazungu wabaguzi sana,kwahili Obama aonyeshe msimamo wake sasa
 
Sasa wewe ni kitu gani kinachokwambia hapo kuna udini kwenye hii issue na sio ubaguzi wa rangi? Kwani umeambiwa huyo aliyewapiga risasi hao wakristo weusi ni muislamu?

Baseless conclusion.

Tiba

Haujanielewa nilichotaka kusema ni kwamba iwe fundisho kwetu kama kuna lolote la kujifunza hapo ya kwamba Mzungu Mkristo anachukia Mtu mweusi Mkristo mwenzake tena mwenye jina kama lake la Julius, Edward, Sospeter n.k kuliko anavyomchukia Mwarabu ambaye ni Muislamu na hata asiye na jina kama lake na wala asiyejua kiingereza!
 
What a poor analysis!!! Wewe umeongozwa na udini badala ya reality.

Tiba

Hata ujaribu kuongea kiingereza kama wao huyo jamaa Mzungu angeona tu uso wako pia angekuwasha risasi lakini angemuona Mchina au Muhindi asiyejua Kiingereza kama wewe asingempiga risasi, hivyo Kiingereza chako hakitakuokoa!
Wale waliopigwa risasi wana majina kama wewe ya wazungu kama John, Michael, Grace, n.k, wanaongea kiingereza kama wewe lkn wapi kwa Mzungu ni Nyani tu wa kuwindwa!
 
western media ni double standard sn,ingekua ni mwarabu apo ungeskia GAIDI,kila media,kila kiongozi ange-conderm hilo tukio,lkn kwakua ni mzungu utaskia one-man incident, na ss waafrika tunapelekwa km kondoo,western media chooses on how and what we should think and believe
 

Wewe ndio tatizo na siyo wao na huyo jamaa angekuona na wewe angekuwasha tu risasi dadadeki!

​
 
hakika ili ni la kulaaniwa na kila mtu..huyo dogo aliyeshoot atakuwa victm wa drug
R.I.P MY BROTHERS FROM ANOTHER MOTHER
 
fulukundo
Hata Mwarabu akikuona pia atakuwasha tu kwa kuwa wewe ndio tatizo mpaka tujifunze na tupate somo!
 
Last edited by a moderator:
Wamarekani ni wabaguzi sana mara nyingi sana matukio ya kuua wamarekani weusi yanajitokeza,lakini hakuna hatua inayochukuliwa na Viongozi wao.
 
aretaskimario
Ndio maana yake hapa siyo Mzungu vs. Mwarabu bali ni sisi kujitambua na kuamka, tutambue ya kwamba hatumuhitaji Mwarabu au Mzungu ili tuwe tukamilishe Ubinadamu wetu, bali tunajihitaji sisi wenyewe na kwamba wote Waarabu na Wazungu watuona kama wanyama tu ambao mtu anaweza kuwinda na kupiga risasi ajisikiavyo!

Hivyo wakati umefika sasa wa kujitambua tuanzie na yanayowezekana Majina! Serikali ipige marufuku utumiaji wa Majina yote ya Kizungu na Kiarabu na hili liwe kwa watoto wote wanaozaliwa na baada ya kizazi kimoja haya majina ya Kizungu na Kiarabu yatakuwa yamepotea, hilo linawezekana bila ya shida!

Kama Muhindi anatumia Jina lake la kihindi, Mchina anatumia jina lake la kichina ni kwa nini sisi Waafrika tuitwe George, Muhamad, Ahmed au sijui Benjamin? Ni kwanini tusiitwe Masanja, Neema, Furaha, n.k?
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…