Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,720
- 215,776
Kijana wa kizungu alikuja kuwakilisha mada UDSM kama moja ya hitimisho la PhD programme. Wakati yuko pale alikutana na binti wa kibongo, mwanzo ulikuwa urafiki, kwani mzungu alipata shida kuwasiliana na locals hata kwenye kujipatia mahitaji yake muhimu. Yule binti alimpa ushirikiano hasa.
Yule binti alikuwa amesuka rasta, mzungu alizisifia sana, baada ya pale yule dada afaifanya ile ndiyo style yake. Mzungu hakukaa sana TZ bali baada ya kuondoka mawasiliano na yule binti yalishamiri, alikuwa anamtumia ticket angalau mara mbili kwa mwaka aende ulaya.
Binti alimaliza shule na kupata kazi, mzungu akapropose, harusi ilifanyika, binti akahamia ulaya. Jamaa baada ya kumaliza PhD yake alipata kazi kwenye ofisi ambayo iko nje sana ya mji mkuu. Kama mnavyofahamu waafrika wengi wanaishi katika miji mikuu ya ulaya, huko vijijini ni wenyewe wazawa. Basi dada ameshakuwa mwenyeji sasa amefumua nywele kipilipili, amemwambia hubby anataka pesa aende kwenye mji mkuu kusuka. Mzungu ameanza kupiga mahesabu ya gharama za ticket, malazi yake akiwa mjini, pesa ya kusukia. Akamwambia usoni, mimi sikujua kama zile rasta hazikuwa nywele zako. Ulinidanganya.