TandaleOne
JF-Expert Member
- Sep 4, 2010
- 1,644
- 709
Mzumbe wajipanga kupanua chuo
Monday, 06 September 2010
Hussein Issa
CHUO Kikuu cha Mzumbe kimenunua eneo la ukubwa wa ekari 384 za mraba, katika eneo la Luambi, mkoani Mbeya, kwa ajili ya ujenzi wa tawi lake.Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, jana, Mkuu wa chuo hicho, Jaji Mkuu mstaafu wa Tanzania, Barnabas Samatta, alisema, hatua hiyo inalenga katika kupanua chuo hicho chenye makao makuu yake,nje kidogo ya mji Morogoro.
Alisema hata hivyo eneo hilo ni dogo ikilinganishwa na ekari 600 ambazo chuo katika tawi lake la Mbeya, kimekuwa kikihitaji kwa ajili ya shughuli zake.
Alisema pamoja na kupata eneo hilo, chuo pia kinatafuta eneo lingine huko Mbweni, ambalo kitalitumia kwa ujenzi wa majengo.
Kwa upande wake Makamu wa chuo hicho, Profesa Joseph Kuzilwa, alisema chuo kina lengo la kutoa wahitimu zaidi, wazalendo.
Alisema ili kufikia malengo hayo, serikali inapaswa kukiwezesha kwa kukitengea fedha za kutosha kuendesha mipango yake.
Uongozi wa chuo hicho upo katika ziara maalumu ya kukagua miradi ya maendeleo inayofanywa na chuo hicho katika mikoa ya Morogoro,Mbeya na Dar es Salaam.
Source: Mwananchi