Mzimu wa bungeni sasa waingia UWT | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mzimu wa bungeni sasa waingia UWT

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mbonea, Nov 26, 2009.

 1. Mbonea

  Mbonea JF-Expert Member

  #1
  Nov 26, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 640
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33


  [​IMG]
  Mwandishi Wetu​
  [​IMG]
  [​IMG]Ni mbio za kuteka wafuasi
  MPASUKO uliotajwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa upo miongoni mwa wabunge wa CCM pekee, umeanza kusogea na kugawa si tu Baraza la Mawaziri na viongozi waandamizi wa chama, bali sasa unazitafuna jumuiya za chama hicho na hasa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), Raia Mwema limeelezwa.
  Kwa mujibu wa habari za uhakika zilizotufikia kutokana na ukimya wa Rais Kikwete, kila kambi sasa inazidi kujitafutia wafuasi kuanzia kwa watendaji waandamizi serikalini na hasa wizara, baadhi ya vyama vya siasa vya upinzani na sasa katika jumuiya za CCM.
  Kwa upande wa serikalini, tayari baadhi ya wizara zimedhibitiwa na makundi hayo mawili hasimu ikielezwa kuwa hali hiyo pia imeingia hadi Ikulu ambako baadhi ya watendaji wasaidizi wa Rais ni sehemu ya kundi mojawapo kati ya mawili hayo yanayohasimiana. Katika baadhi ya vyama vya upinzani, tayari baadhi ya viongozi wa vyama hivyo wamegawanyika.
  “Kwenye chama kimoja cha upinzani, upande wa viongozi waandamizi umegawanyika. Kuna baadhi wanaungana na kundi la CCM linalodaiwa kuwa la mafisadi tena kwa kupewa fedha nyingi tu ili kunadi baadhi ya ajenda za kundi hilo,” alisema mmoja wa viongozi anayepinga kuwapo kwa makundi yanayovutana katika suala la ufisadi.
  Aliongeza kiongozi huyo: “Lakini pia kuna wengine wapo upande wa kundi linalodaiwa kupinga au kupambana na mafisadi na hawa wanaungana na waliomo CCM kwa sababu nia zao zinaonekana kufanana.”
  Maelezo ya kiongozi huyo yanabainika katika mijadala mizito ya ufisadi uliotikisa nchi kama kashfa ya Richmond na wizi wa mabilioni ya fedha kwenye Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) kwenye Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
  Katika mwendelezo wa kashfa ya Richmond hivi karibuni kuliibuka kundi lililokuwa likilenga kumhusisha Rais Kikwete na kashfa hiyo na Ikulu kulazimika kutoa taarifa ya kukanusha kwanza ikiwa imetolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu na baadaye taarifa ya kina zaidi kutolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo.
  Miezi kadhaa baadaye, Rais alifanya mabadiliko ya makatibu wakuu wa wizara mbalimbali kutokana na baadhi ya waliokuwapo kustaafu. Katika mabadiliko hayo alimtoa Ikulu, aliyekuwa katibu wake, Jairo Kitundu, kwenda kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, ambayo ndiyo kiini cha kashfa ya Richmond na miradi mingine ya umeme nchini. Jairo alikwenda kuchukua nafasi iliyoachwa na Arthur Mwakapugi aliyestaafu kwa mujibu wa sheria lakini pia akiwa ametajwa kutakiwa kuwajibishwa kwenye ripoti ya Kamati Teule ya Bunge kuhusu kashfa ya Richmond.
  Habari zaidi kutoka kwa viongozi waandamizi serikalini wanaochukizwa na mpasuko unaozidi kutanuka zinaeleza kuwa lengo ni kila kundi kupigania kuwa na nguvu zaidi ya jingine kwa kuwa Rais Kikwete haonekani kuweka bayana msimamo wake licha ya kuwapo kwa vitendo visivyo vya moja kwa moja vinavyoonyesha anachokusudia.
  Kwa mujibu wa viongozi hao waandamizi, wakati fulani Rais Kikwete anaonekana kuwa na msimamo wa kupinga ufisadi wakitoa mifano ya kuacha aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na mawaziri wengine kujiuzulu. Lowassa aliandika barua ya kujiuzulu kwa Rais na ikakubaliwa tofauti na Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, ambaye wakati aliyekuwa waziri wake, Iddi Simba alipoandika barua ya kujiuzulu, Rais huyo akionyesha kuwa bado anamuhitaji, alimtuma kushiriki mkutano licha ya barua kuwasilishwa na hivyo alikubali kujiuzulu kwake kwa shingo upande.
  Katika mpasuko wa sasa, inaelezwa kuwa kundi linalodaiwa kupinga ufisadi wazi wazi limeanzia bungeni likiungwa mkono na Spika Samuel Sitta na baadhi ya wabunge, wakati huo huo kundi linalopingana na kundi hilo nalo chimbuko lake ni bungeni likidaiwa kuundwa na wabunge, Rostam Aziz wa Igunga, baadhi ya mawaziri na wabunge wengine.
  [​IMG]

  Mwenyekiti UWT, Sophia Simba
  Imeelezwa kuwa ni makundi haya mawili ndani ya Bunge na CCM ambayo yako nyuma ya mvutano wa mjuda mrefu lakini uliobuka wiki hii mjini Dodoma katika mkutano wa Baraza Kuu la UWT, ukiwagonganisha Mwenyekiti Sophia Simba na Katibu Mkuu wake Husna Mwilima.
  Taarifa za ndani ya UWT zinasema wote Simba na Mwilima wana ufuasi tofauti kati ya makundi hayo mawili na hiyo ndiyo iliyosababisha kila mmoja kuwa na orodha yake ya makatibu wa wilaya jambo linalotajwa ndilo lililowafikisha katika mvutano ulioshuhudiwa wiki hii katika kikao cha baraza lao baada ya muafaka kushindikana baina yao na wakaanza kukomoana.
  “Kwa kweli sasa ni dhahiri Rais Kikwete hakuwa na taarifa za kina kuhusu kumeguka kwa chama anachokiongoza. Mpasuko au uhasama si tu miongoni mwa wabunge wa CCM, umesambaa hadi katika jumuiya za chama, na kila kambi inajizatiti kuizidi kete kambi nyingine,” alisema mmoja wa viongozi wastaafu wa UWT.
  Hata hivyo, mgogoro wa viongozi hao wa UWT unatafsiriwa kuwa ni kupuuza kauli au wosia wa Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete ambaye katika hotuba yake ya Januari 7, mwaka huu, ukumbi wa Kilimani, Dodoma alifungua mkutano wa saba wa UWT, akiwataka kufanya kazi ya kusaidia wanawake wengine nchini badala ya kubaki katika majungu na fitina kati yao.
  Lakini kabla ya kueleza hayo, kwenye hotuba yake hiyo Rais Kikwete aliwaasa wapiga kura waliokuwa na jukumu la kuchagua viongozi wao akiwamo Mwenyekiti wa umoja huo kwa kusema; “Naomba mkumbuke kuwa mnachagua viongozi wa kuongoza Jumuiya yenu kwa miaka mitano. Hivyo, hamna budi kuwa makini. Mkifanya kosa, mtalijutia kwa miaka mitano. Majuto ni mkujuu. Chagueni viongozi madhubuti, wanaoijua na kuipenda Jumuiya na wachapakazi. Watu mtakaokuwa nao wakati wa jua na mvua na kuwavusha kuwapeleka kwenye neema na mafanikio.”
  Na katika kuwaasa zaidi Rais Kikwete aliwataka kutochaguana kutokana na urafiki, ufadhili au ushoga akisema; “Chagueni watu kwa kufaa kwao na si kwa urafiki wenu au kufadhiliana. Ushoga na kufadhiliana au kupeana chochote isiwe kigezo cha kufaa kuwa kiongozi. Chagueni mtu anayeweza kuiongoza Jumuiya kutimiza ipasavyo wajibu na majukumu yake kwa maslahi ya mwanamke wa Tanzania.”
  Kutokana na kauli hiyo ya Rais, inaelezwa kuwa mvutano baina ya viongozi wakuu (mwenyekiti na katibu) ni dhahiri umetokana na kupuuzwa kwa ushauri wa Rais na kwamba kitendo cha viongozi hao wawili kubaki wakivutana kwa lengo la kutimiza haja za makundi ya kisiasa kunazidi kuchochea ugumu wa chama hicho kubaki salama.
  Kutokana kuyumba kwa uongozi wa juu wa UWT wapo watu wanaodai kuwa baadhi ya viongozi waliochaguliwa hawana sifa madhubuti na walichaguliwa kutokana na nguvu ya fedha.
  Watu hawa wanakumbuka kauli ya Rais Kikwete, kwenye hotuba yake hiyo kwamba; “Aina na sifa za viongozi mnaowahitaji mnazifahamu. Na nyie wenyewe ndani ya Jumuiya yenu mnafahamiana vizuri zaidi. Sina haja na hakuna mwenye uwezo wa kuwapa mhadhara kuhusu nani wanaowafaa. Wito wangu kwenu ni kwamba, chagueni viongozi watakaoitoa Jumuiya yenu hapa ilipo na kuipeleka mbele zaidi kwenye maendeleo. Viongozi waadilifu na wanaosisitiza umoja na si mifarakano”.
  Miezi michache iliyopita kamati iliyoundwa na Halmashauri Kuu ya CCM kuzungumza na wabunge wa CCM pamoja na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar ilifanya hivyo na mambo kuzidi kuwa mabaya zaidi na hasa upande wa wabunge wa CCM ambao walishambuliana katika mwelekeo wa kila kundi kulenga kuwa imara zaidi likipangua hoja za ‘wapinzani’ dhidi yao.
  Katika mjadala huo wa wabunge wa CCM baadhi ya mawaziri na naibu mawaziri walionekana dhahiri kuwa na upande kiasi cha kutumia taarifa za ofisini kwao kushambulia upande wa pili, jambo ambalo limewahi kutafsiriwa na baadhi ya wasomi na watu mashuhuri nchini kuwa ni kinyume cha matakwa ya utawala bora.
  [​IMG]
  Source: Raia Mwema
   
 2. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #2
  Nov 26, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Uyu mama wasipomthibit atakuja haribu,ni kheri achukue kama kavacation akapumzike maana nimegundua issue za mfululizo zinamfanya aongee kama headless kabsaaa.ivi ana mume?
   
 3. Dr. Chapa Kiuno

  Dr. Chapa Kiuno JF-Expert Member

  #3
  Nov 26, 2009
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 445
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ndy tatizo la Wabunge wa kuteuliwa! Wat I wonder is how mbunge wa kuteuliwa alivyoweza kupata nyadhifa kubwa kama hizo... Somethin must be cookin....
   
 4. D

  Dalilah Member

  #4
  Nov 26, 2009
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 47
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Hasa ukimteua mtu asiye na uwezo, umemtoa kwenye kapu, maana alishindwa jimbo, akajaribu viti maalum, akapigwa chini, akajaribu ndani ya "kapu" hakutoka, hapo mtu makini alitakiwa ajiulize huyu ni vipi mbona anaonekana hakubaliki? Lakini unamteua, halafu unampa ofisi nyeti mamaa wa mipasho, lazima apagawe. Matokeo yake ndo haya.
   
 5. Fugwe

  Fugwe JF-Expert Member

  #5
  Nov 26, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,680
  Likes Received: 230
  Trophy Points: 160
  For any change to happen, there must be two conflicting sides. Remember during slave era (Masters vs Slaves), Feudalism (Landlords vs workers), Capitalism (Capitalists vs Proletarians). Now, for the Chama Cha Mapinduzi (Mafisadi vs Ant-Mafisadi). These conflicts are capable for disintegrating the existing ruling system which led to the emegency of new system, the system which favored by all parts in conflict.
   
Loading...