Mzee wa Upako anaanza lini biashara ya Gongo?

Hussein Massanza

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
1,015
2,191
Nmekutana na bandiko la mwandishi aitwaye Luqman Maloto likikumbushia ahadi ya Mch. Anthony Lusekelo kuhusu mkwara wake alioutoa dhidi ya waandishi waliomwandika kuhusu skendo yake ya kulewa 'bapa' na kufanya vurugu kwa majirani...

Nami nauliza, biashara yake inaanza lini tukapunguze stress?!
-------------

Wakati leo watu wengi walijazana Kanisa la Ufufuo na Uzima kwa Askofu Josephat Gwajima kujua ameandaa huduma gani, ana ubuyu gani, ana skendo gani mpya, anataka kum-Bashite nani, mimi nilikuwa Kanisa la Maombezi kwa Mzee wa Upako.

Kwa unyenyekevu mkubwa, kipindi hiki nikiwa kwenye toba ya Kwaresma, leo nilikwenda Kanisa la Maombezi kwa Mchungaji Anthony Lusekelo 'Mzee wa Upako' kupokea ripoti muhimu.

Unajua tangu Desemba mwaka jana tulipewa ahadi na Mzee wa Upako kwamba waandishi wote wa habari waliomwandika vibaya, wangefariki dunia kabla ya Machi mwaka huu, vinginevyo ataacha kutoa huduma ya Kanisa na kwenda kuuza gongo.

Ishu ni ile kashfa ya Baba Mchungaji (Mzee wa Upako) kudaiwa kulewa tilalila kisha kuwamwagia matusi na kuwaangushia timbwili zito majirani zake, Kawe, Dar. Aliahidi kuwa waandishi viherehere waliomwandika vibaya wangekufa kabla ya Machi 2017.

Leo ni Aprili 2, yaani siku mbili baada ya kukamilika kwa Machi, kwa hiyo nilikwenda kwa Mzee wa Upako kupokea ripoti juu ya vifo vya waandishi waliomwandika vibaya, au kusikia chochote kuhusu mpango wake wa kuanza kuuza gongo baada ya Mungu kugoma kuwachukua hao waandishi.

Hicho ndicho kilichonifanya nitofautiane na wengi waliojumuika Ufufuo na Uzima kisha mimi nikawa mmoja wa waliokuwemo kwenye huduma ya Maombezi kwa Mzee wa Upako.

Tumetofautiana sana. Jinsi tunavyofikiria na tunavyoamua ndivyo utofauti wetu unavyoonekana. Wewe huduma au ubuyu kwa Gwajima, mimi ripoti ya vifo vya waandishi au uamuzi mgumu wa mchungaji kubadili kazi na kuwa muuza gongo.

Ndimi Luqman MALOTO
 
Sasa ndio wakati wake wa 'kupiga hela' iliyonyooka maana VIROBA vimefungiwa in his favor. Naziomba tu mamlaka zisisahau kumpatia EFD ili tupate kodi yetu boda boda wanapoenda 'kunyonya' mma
 
Afrika na Tanzania wazee wetu waliotangulia wanatuona!!
 
49d256d18726b870d5811312de22bac3.jpg

Mzee jipaba
 
WATASHINDANAAAA LAKINI HAWATASHIDAAAAA HAO WAANDISHI MIMI NIMEWASAMEEE AMEIN
 
Aliwasamehe mtumishi mapema kabisa hata ninyi wa JF alisema hamjamuinua hamtamshusha hivyo anawasehe
 
Back
Top Bottom