Mzee wa TSC vipi?

Anselm

JF-Expert Member
Nov 16, 2010
1,710
291
Binafsi hupenda kumwita Mzee wa TSC ksbb blog yake husheheni matukio ya kituo hiki cha kuendeleza soka la vijana sijui kwasababu walimu'offer safari ya kuandamana na ile team yao kule Ujerumani? I dont know!!,lkn huyu si mwingine bali ni Kaka yangu Shaffih Dauda....nikiwa kama mfatiliaji mkubwa wa blog yake nimegundua licha ya Media na sites nyingi kuhamia kule Kigali na ku'report kile kilichokuwa kikifanywa na Mabalozi wetu Yanga a.k.a team ya Wananchi Brother yeye amegoma kabisa ku'report kwa undani yaliyokuwa yanaendelea kule na matokeo yake akaamua(tena nafikiri kwa kuona aibu) ku'report kidogo sana tukio la Rais Kagame kuwaalika Yanga Ikulu kwake labda kwa kutambua safari/mwaliko ule ulikuwa na mchango katika kuimarisha uhusiano mzuri baina ya nchi hizi mbili.
Kwa mtazamo wangu,inawezekana Brother Shaffih hajaipenda safari ya Yanga na ndo maana ameipa nafasi ndogo sana kwenye blog yake na amefanya hili bila kujali kuwa blog yake niliyokuwa naiamini kuwa ni moja ya blog makini za michezo hapa nchini hutembelewa na mashabiki wote(wa Yanga,Simba,Azam,Mtibwa,Mgambo Shooting etc).
Ni dhahiri shahiri kuwa Shaffih ameshindwa kusoma alama za nyakati na kufahamu ni habari gani sasa hivi katika kipindi hiki zinaweza kuuza kwa mashabiki wote, habari za Yanga kuwa Kigali mchakato wa Twite kama atajiunga au hatajiunga na Yanga zilikuwa zikitupiwa macho na masikio hata na wapenzi wa Simba zaidi kuliko hata safari ya Simba kutembelea kiwanda cha Bia huko Arusha.
Hivi ameshindwa kujiuliza kwanini Global walitoa Mtu na kuandamana na Yanga kule Kigali, kwanini MCL waliamua kuweka picha ya Yanga ikifanya mazoezi kwenye ukurasa wa kwanza wa gazeti lao la Mwananchi,kwanini walikuwa na mtu maalum aliyekuwa akiwapa taarifa kamili za kule, ameshindwa kujiuliza haya yote, I wish angewauliza Global walichotengeneza kwa mauzo yao ya Gazeti lao la Champion la Ijumaa ambalo lilikuwa limesheheni habari za Kigali.
Kihalisia kama ingekuwa ni mauzo "Shaffih Dauda in Sports" lazima ingekuwa ime'drop sana, napenda kumshauri kwa mara nyingine ajitahidi kwenda na ethics za hiyo professional yake,aweke unazi pembeni na kufanya kazi yake kwa usawa,aangalie wenzake wenye blog nyingine za michezo wanavyo'balance habari zao licha ya kuwa na mapenzi yao binafsi pia, siyo yeye kila siku Simba watembelea Mwananyamala,Simba watembelea kiwanda cha bia,Simba watembelea wapi sijui, nani na nani wa Simba B waing'arisha TSC,kila siku TSC,Simba...TSC,Simba.
 
Yanga ndio mdudu gani?. Hivi huwezi kupata habari za yanga mpaka ziandikwe na Shaffih?. Mwambie Kitenge nae aanzishe blog ili asiwe anakupepesea macho kwenye habari za Yanga.
 
Yanga ndio mdudu gani?. Hivi huwezi kupata habari za yanga mpaka ziandikwe na Shaffih?. Mwambie Kitenge nae aanzishe blog ili asiwe anakupepesea macho kwenye habari za Yanga.

Hapo kwenye blue dada'ngu ukiingia hata kwenye website ya Ikulu ya Rwanda unaweza kupata majibu mazuri ya hilo swali lako, by the way kama blog ya Shaffih kuandika habari za Yanga ni haramu basi aibadilishe jina iitwe "Simba S.C Official Blog"
By the way mimi namsaidia tu kwani ubaguzi wake unaweza kufanya baadhi ya wadhamini waka'withdraw,shauri yake.
 
Acha blog ya Shaffih ,
Rais Paul Kagame ameweka kwenye website yake, tembelea Paul Kagame
Hapo ndipo utakapojua Yanga iko level zp, Shaaffih ana chuki binafsi, maana hata sports bar jana katuwekea interview ya mwaka jana mwezi wa 8 na Nteze John 'Lungu' Seattle Sounder!

Je ni kweli kwa wiki nzima hapakua na habari nzuri za kuvutia zilizotokea nchini mpaka atuwekee interview ya mwaka jana??
 
Back
Top Bottom