Mzee Pwagu Afariki Dunia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mzee Pwagu Afariki Dunia

Discussion in 'Matangazo madogo' started by MziziMkavu, May 30, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 30, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280


  [​IMG]
  Mzee Pwagu enzi za uhai wake Saturday, May 29, 2010 2:57 AM
  Muigizaji mahiri nchini Tanzania, Rajab Kibwana Hatia au maarufu kwa jina la Pwagu ambaye alitamba sana redioni kwenye mchezo wake wa Pwagu na Pwaguzi, amefariki dunia jana akiwa na umri wa miaka 87. Mzee Pwagu alifariki jana ijumaa kwenye hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam baada ya kuugua muda mrefu maradhi ya uzeeni.

  Mzee Pwagu alitamba sana redioni kwenye miaka ya 60 hadi 80 katika kipindi cha redio kilichokuwa kikirushwa hewani na redio ya taifa Redio Tanzania Dar Es Salaam (RTD) akimshirikisha rafiki yake Ali Said Keto ambaye yeye alikuwa maarufu kwa jina la Pwaguzi.

  Mzee Pwagu ambaye alizaliwa mwaka 1923 mjini Tabora atakumbukwa zaidi kwa juhudi zake za kuinua sanaa za maigizo nchini.

  Mzee Pwagu ndiye aliyekuwa muanzilishi wa kundi la Kaole ambalo limetoa wasanii wengi wanaotamba hivi sasa kwenye anga la filamu Tanzania kama vile Ray na Kanumba.

  Mazishi ya Mzee Pwagu yatafanyika leo kwenye makaburi ya Kigogo jijini Dar es Salaam.

  MUNGU AMLAZE MZEE PWAGU MAHALI PEMA PEPONI -- AMEN
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  May 30, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Mungu akurehemu....
  Rest in peace.....

  Mchango wako wa sanaa ulikuwa mkubwa....
   
 3. F

  Fernandes Rodri JF-Expert Member

  #3
  May 30, 2010
  Joined: Apr 11, 2009
  Messages: 407
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  INNA LILLAHI WA INNA ILAIHI RAJIUN Poleni wafiwa wote
   
 4. Fisherscom

  Fisherscom JF-Expert Member

  #4
  May 30, 2010
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,441
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  Mwenyezi ailaze pema roho ya marehemu.
  Aamin!
   
Loading...