Mzee Mohamed Said acha kupindisha historia, ni Nyerere aliyetuletea uhuru, sio wengine

Da'Vinci

JF-Expert Member
Dec 1, 2016
35,686
106,811
Salute!

Heshima yako mzee Mohamed Said natumai u mzima wa afya.

Mzee hongera kwa uwezo wa uandishi wako wa makala za historia ya taifa letu hili.

Mimi nimekua nikifuatilia sana mada zako hasa kipindi cha nyuma lakini siku hizi si msomaji tena wa baadhi ya mada zako kutokana na sababu nitakazo zieleza hapa chini.

Katika mada zako nyingi za historia ya taifa hili hua nikiangaliama Context naona mada zako zote zinalia kwa uchungu huku zikitoa ujumbe kua Waislamu tunaonewa, nikimaanisha kwamba mada zako karibu zote hua zina chembe chembe za Udini. Baadhi ya member hasa mkuu Pascal Mayalla wamejaribu kuchambua mada zako na kuonyesha ni jinsi gani zilivyojaa mahaba ya dini, na upotoshaji wa historia pia hata wasomaji wako ambao mko imani moja wanadiriki kuupinga hata ukweli ili tu kumtetea mwarabu na dini yake. Mfano kwenye mada aliyoanzisha mkuu Pasco akionesha jinsi Waarabu walivyowatesa wazawa wa Zanzibar, watu wengi (Muslims) waliukataa ukweli huona na kukubali kumtetea Mwarabuu kisa tu ndio alieleta dini hiyo.

Mzee wangu, wewe ni mwandishi na unazifahamu vyema ethics za mwandishi, moja ya sifa kuu za mwandishi ni kutokuandika habari fulani kwa kuweka mbele emotions na mahaba yake juu ya kitu anachotaka kutoa taarifa, mwandishi unatakiwa uandike/utoe habari ya kitu hicho ukiwa kwenye free state, yaani uandike kitu kama kilivyo bila kuweka mahaba yako juu kitu hiko. Kwa hilo mzee wangu naona umefeli kulitekeleza labda lengo lako kuu hua ni kuonyesha jinsi gani ndugu zetu mnavyo kandamizwa.

Nikupe mfano kidogo, humu JF kuna mwandishi wa makala mbalimbali anaitwa The Bold (habibu B Anga) ni mwislamu pure! Lakini kamwe akiandika kitu ambacho hua kinagusa imani yake hua anaandika kama kilivyo bila kuweka upendeleo. Ref uzi wa: Adhabu ya kuchinjwa mbele ya kadamanasi Saudia.

Lakini mzee hata mimi mwenyewe ni Mkatoliki lakini kama nikichangia mada au kundika mada juu ya mauaji yaliyofanywa na Kanisa hili siwezi kubisha au kuandika tofauti na ilivyokua kisa ni kanisa langu, siwezikubisha wala kuandika kwa upendeleo kua kanisa katoliki kipindi cha Holocust liliagiza (Papa) wananchi wote wa nchi ya Uholanzi
(Netherlands) wauawe.

NB: Yote hayo najaaribu kukuonyesha ni jinsi gani kuna udini kwenye mada zako, lakini lengo langu sijaandika uzi huu ili tujadili udini wala dini yako ila lengo langu hasa kuandika huu uzi ni

Mkuu, kama nilivyokwisha kukuonyesha jinsi mada zako zilivyo na udini, sasangoja niende kwenye lengo la uzi huu..Mada zako nyingi nilizowahi kusoma kuhusu historia ya uhuru wa Tanganyika, ukiangalia nyuma ya pazia ujumbe ulio jificha unaonyesha kua Mwl. Nyerere hakutakiwa kuwa recognise kama mtu aliye tuletea Uhuru nchini toka kwa wakoloni, Bali kuna wazee wa kiisalmu wa hapo Dar kama Sykes familly n.k ndio wamehangaika zaidi kuleta uhuru.

Mkuu ni kweli wamechangia kiasi kikubwa kupatika uhuru hapa lakini, ukweliutabaki pale palekua ni J.K.Nyerere the Almighty ndio kaleta uhuru Tanganyika na sio hao wengine bila kuzingatia kigezo cha udini. kwanini nasema hivi?
Kila mtu akizaliwa hapa duniani huja na kusudi (Purpose) aliloletwa kulitimiza, kwa mantiki hiyo Mwalimu aliletwa kwa kusudi la kuikomboa Tanganyika kutoka kwenye mikono ya wakoloni,Mwalimu nyerere kazaliwa 1922 lakini mwaka 1945 akiwa ana miaka 23 tu aliweza kuhudhuria mkutano wa 5 wa Pan African Congress jijini Manchester hivyo basi waweza kuona ni jinsi gani alivyikua ashajua kusudinla yeye kuja dunianina kuanza kulifanyia kazi. mkuu hatima ya uhuruwa Tanzania ilikua mikononi mwa mwalimu, na kama inavyojulikana "You can escape your destiny, nobody can take away your destiny"

Mfano kidogo ili kuenea kwa imani ya kiislamu duniani allah ilibidi amletee Mtume maswahaba ambao walimsaidia pakubwa kusambaza uislam kwenye maeneo ya makafiri, vilievile ili YESU kueneza wokovu duniani ilibidi awe na wanafunzi na mitume wa kusambaza Habari za wokuvu ulimwengu mzima, kupitia wanafunzi wake Yesu aliweza kutimiza kusudi lake la kueneza wokuvu, Mwisho wa siku tunasema Yesu katuleta wokuvu mpaka kwetu huku ndani ndani ( ila hatusemi mitume wanatakiwa ndio wtambulike kama walioleta wokovu duniani bali Yesu) Mkuu hata wewe hadi kufika hapo ulipo kuna watu walisimama nawe hadi kua wewe uliyoko sasa hivi, ila hatusemi kwamba wale wiloku-push kipindi cha nyuma ndio wanaotakiwa kufahamika kama wanaoandika makala humu jF bali mzee Mohamed Said.

Kwa mantiki hiyo namaanisha kwamba ili kutimiza kusudi fulani ulilopewa na Mungu basi Mungu hukuandalia watu ambao watafanya kazi bega kwa bega ili kutimiza kusudi lako (mfano mzuri ni wazazi/walezi). hivi mkuu unatambua kua kuna watu hua wamezaliwa kusudi lao la kuzaliwa likiwa ni kuja kumsaidia mtu fulani aje kutimiza kusudi lake alopewa na Mungu,mfano mzuri ni Yohana mbatizaji. kusudi lake hata kwenye vitabu vinasema alikuja kuandaa njia/kusudi la Masihi Kristo....Hivyo hivyo kwa Mwalimu wetu Kuna watu wengi sana waliletwa hapa Tanganyika kuja kutimiza kusudi hilo. Ili kutimiza kusudi lake la kuiletea nchi yetu uhuru ilibidi watu wengi washirikiane nae. hatimaye aliweza kufanikiwa kuleta uhuru, hivyo basi hakuna suala la udini wala nini The Godman Nyerere atabakia kutambuliwa kama shujaa aliyeleta uhuru Tanganyika haijalishi ni wangapi walishirikiana nae.

Niombe radhi kwa yoyote ambae andiko langu limemuudhi kwa namna moja au nyingine.

Ciao
- Da'Vinci
 
Sijawahi kusoma mada za huyo Mohammed ila historia huwa haifutiki.

Ninachokijua mimi ni kwamba kuna kikundi cha watu kilicho anzisha chokochoko za kudai Uhuru, wengi wao wakiwa ni wakazi wa Dar es salaam wakati huo Nyerere alikuwa mwalimu wa Pugu secondary.

Baadae hiki kikundi kikaon kinahitaji mtu wa kumsimamisha mwenye kariba km ya Mwalimu Nyerere ndipo walipoenda Pugu secondary na kukutana na Mwalimu Nyerere na kumpa mikakati.
 
Nakupongeza kwa maandishi na hoja zenye upeo na akili kwa jumla. Mzee MS kwa sisi tunaofahamu asili ya imani yake anayoitetea kwa hila hatushangai ila tunampuuza

Tabia yake ya kugeuzageuza mambo kwa hila ndiyo pia iliyounda hiyo imani yake! Kupindua pindua historia, kuchanganya uongo na ukweli, hila n.k...
 
Da ' Vinci,

Ahsante sana kwa kuniandikia.

Hakika mimi nimeandika historia ya Waislam jinsi walivyokuwa mstari wa mbele katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika wala sikatai na wala sijuti kwa kufanya hivyo.

Wengi wameumizwa na historia hii kwa kuwa hawakuwa wanaijua, historia waliokuwa wanaijua ni ile historia rasmi ambayo ndiyo iliyokuwa imepasishwa na kusomeshwa kuanzia shule za msingi hadi Chuo Kikuu,

Hii ndiyo historia niliyoikuta mimi ikisomeshwa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam nilipokuwa mwanafunzi na nilikuwa nawashangaza hadi walimu wangu ninapowaambia kuwa historia hiyo ina upungufu mkubwa.

Laiti mimi nisingeliaandika kitabu cha ''Maisha na Nyakati za Abdul Sykes...'' historia hii ilikuwa imeshafutika na kupotea kabisa na hakuna jamii katika ulimwengu huu ambayo inaweza kukubali au kuvumilia kuona historia yake inafutwa.

Hakuna mahali popote ambapo mimi nimedogosha mchango wa Julius Nyerere katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika na laiti ningelikuwa mjinga nikafanya hivyo ningekiua kitabu changu kwani wasomaji wangenipuuza.

Nilichofanya mimi ni kueleza kuwa ikiwa ni historia ya TANU basi haiwezekani kuanza na Julius Nyerere 1954 itabidi turudi nyuma hadi 1924 na tusome mswada wa Kleist Sykes alioandika kabla ya kifo chake 1949 akieleza historia ya African Association yeye akiwa mmoja wa waasisi wa chama hicho (mswada huu mwaka wa 1973 ukawa moja ya sura ya kitabu kilichohaririwa na John Iliffe, ''Modern Tanzanians.'').

Katika mtiririko wa historia hii kuna wazalendo wengi kama Hassan Suleiman na Ali Juma Ponda, Hamza Kibwana Mwapachu na wale madaktari watano - Dr. Joseph Mutahangarwa, Dr. Vedasto Kyaruzi, Dr. Wilbard Mwanjisi, Dr. Michael Lugazia na Dr. Luciano Tsere.

Pamoja na hawa ndipo wanapoingia Abdul Sykes na mdogo wake Ally katika historia ya TAA, TANU na harakati za kudai uhuru na ndipo pia nilipotumia nyaraka waliazokuwanazo kuanzia miaka ya 1920 zinazoeleza na kuthibitisha historia yao katika kuunda TANU na mchango wao katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Kwa nini historia hii ilifutwa swali hili nitakuachia wewe ulijibu.
Naamini hujusikii vibaya kwa kuandikwa historia hii.

Ama kuhusu manung'uniko ya Waislam yapo na si mimi peke yangu ambae nimeandika kuhusu tatizo hili.

Somo hili limeandikwa na Bergen (1981), Sivalon (1992) na Njozi (2002) ingawa kitabu cha Njozi kimepigwa marufuku.

Kwa nini kitabu cha Njozi kimepigwa marufuku badala ya serikali kujibu yaliyosemwa hili swali pia nakuachia wewe ulijibu.

Tatizo la udini tunalo nchini na serikali inalijua na Waislam hawajajificha katika kulieleza tatizo hili na linafahamika.

Ikiwa wewe huamini kuwa lipo kwangu ni sawa pia.
Kughitilafiana kwa binadamu katika fikra hili haliepukiki.

Sina tatizo na kutambuliwa kwa Nyerere kama shujaa wa uhuru wa Tanganyika na narudia tena kusema kuwa laiti ningelikuwa mjinga na kudogosha mchango wa Mwalimu Nyerere katika historia ya TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika kitabu changu kingelikufa mapema sana.

Kitabu kimepokelewa vyema kote katika Vyuo Vikuu wanakosemesha African History na baadhi ya vyuo hivi wamenialika kuzungumza katika vyuo vyao kwa mnasaba wa kitabu hiki nilichoandika.

Kitabu kimepata ''review,'' tatu ndani ya Cambridge Journal of African History na kimechapwa kama ''series'' katika, The East African Magazine (Nairobi) na katika baadhi ya magazeti hapa nyumbani.

Kitabu hiki kinatambulika kama ''corrective history,'' yaani imesahihisha historia ambayo kwa bahati mbaya ilikuwa na makosa.

Wako waliopendezwa na kitabu changu na ndiyo maana sasa tunakwenda toleo la tatu Kiingereza na la nne Kiswahili.

Halikadhalika wako ambao hawakupendezwa na kitabu changu wangependa historia ibaki kama ilivyokuwa zamani kwa kufuta historia za wazalendo wengine katika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika ibakie historia ya Mwalimu Nyerere peke yake.

Muhali wa hili ni kuwa wale waliokuwa na Mwalimu Nyerere katikaTANU mimi ni wazee wangu kutoihifadhi historia yao ni kujidhulumu mimi mwenyewe na kizazi changu.

Unaweza kuisoma historia ya babu yangu Salum Abdallah katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika hapo chini:



Hata wewe ungelitoka katika mifupa ya wazee kama wangu usingestahamili kuona historia yao inafutwa.
 
Nakupongeza kwa maandishi na hoja zenye upeo na akili kwa jumla. Mzee MS kwa sisi tunaofahamu asili ya imani yake anayoitetea kwa hila hatushangai ila tunampuuza!

Tabia yake ya kugeuzageuza mambo kwa hila ndiyo pia iliyounda hiyo imani yake! Kupindua pindua historia, kuchanganya uongo na ukweli, hila n.k.
Ahsante kwa pongezi. Kwakweli mzee wetu ajikague upya aangalie wapi walipokosea wao wenyewe na falsafa za dini yao.
 
Nina maswali mawili tu kwako kaka.

1) Una uhakika gani kama Nyerere ndiye aliyetupatia uhuru ilhali harakati za uhuru alizikuta?

2) TAA inaanzishwa ndio Nyerere anazaliwa mpk inabadilishwa kuwa TANU waasisi wote walikuwepo nyerere ndiyo anazaliwa yeye alishiriki tu km mteuliwa wa kuwakilisha watafuta uhuru.

Je, uhuru kautafuta yeye ama kawakilisha ktk kuutafuta, ni nini maana ya kuutafuta huo uhuru km muktadha ndio huo?
 
Nina maswali mawili tu kwako kaka.

1) Unauhakika gani km Nyerere ndiye aliyetupatia uhuru ilhali harakati za uhuru alizikuta???
2) TAA inaanzishwa ndio Nyerere anazaliwa mpk inabadilishwa kuwa TANU waasisi wote walikuwepo nyerere ndiyo anazaliwa yeye alishiriki tu km mteuliwa wa kuwakilisha watafuta uhuru,je uhuru kautafuta yeye ama kawakilisha ktk kuutafuta,ni nn maana ya kuutafuta huo uhuru km muktadha ndio huo?
Namimi naomba nikuulize unadhani kwanini afahamike JKN kama aliyetuletea uhuru ilihali kulikua na watu walioanza kabla..?
 
Mohamed Said hayo anayoyaandika ndio kweli anayoijua, na kitabu chake ninacho na ki rejea
 
Yeye atafahamika kwasababu ndiye aliyewakilisha vema kupatikanika uhuru wa Tanganyika.
Mathalan kaka mm,ww na watu wengine tuna harakati za ku launch satellite.

Tulianza muda mrefu kuja ww tukaketi nawe na kukupa formula na kukuomba utuwakilishe ktk lile.
Je bro itakua ww ndiye pioneer wa satellite launcher ama volunteer?

Ukisema yeye ndiye aliyetupatia uhuru basi yeye ndiye Pioneer of freedom fighting ilhali si kweli kaka.

Yeye aliwakilisha vema namsifia ila hakuutafuta yeye.
Namimi naomba nikuulize unadhani kwanini afahamike JKN kama aliyetuletea uhuru ilihali kulikua na watu walioanza kabla..?
 
Namimi naomba nikuulize unadhani kwanini afahamike JKN kama aliyetuletea uhuru ilihali kulikua na watu walioanza kabla..?
Kwenye mechi captain ndio hupewa kombe Nyerere alichaguliwa kama kaptani ndio maana uhuru kutolewa yeye ndio alie kabiziwa. Mfano ccm wamemteua Magufuli kugombania urais 2015 lakini Lowasa mkongwe kuliko Magufuli kwenye ccm.


Nangatukaa 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Mzee Mohammed Said huyu mpe mtihani mdogo tu mwambie alete ushahidi wa mwalimu Nyerere pamoja na mapadri kama zile picha alizo piga na kina sheikh Takadiri na wengine.

Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
Huu ndio unaitwa UDINI. Why Mapadri? Uhuru wa nchi hii haukutafutwa kwa makundi kiasi iandikwe Historia ya Mapadri, Mashehe, Mabudha, Wapemba, Wageni, Wazawa na wengineo.
 
Inaelekea wewe ni kizazi baada ya uhuru ila kwa wale ambao walikuwa na akili zao ingawa watoto walishuhudia mengi na anachoandika Mohamed Said kwa yeyote yule alizaliwa miaka ya 40 na 50 na kukulia dar anaelewa.

Mimi ninakumbuka zile enzi ambapo Bibi Titi na wenzake walikuwa wanapita nyumba hadi nyumba kuhamasisha akina mama kuingia TANU.

Na ninamkumbuka mwalimu kipindi kile ambacho alikuwa anakuja mtaa wa Sukuma na Mafia yalipokuwa makazi ya Yanga kwenye vikao pamoja na wazee wetu. Wacha kupotosha wenzako.
 
Sijawahi kusoma mada za huyo Mohammed ila historia huwa haifutiki

Ninachokijua mimi ni kwamba kuna kikundi cha watu kilicho anzishisha chokochoko za kudai Uhuru wengi wao wakiwa ni wakazi wa Dar es salaam waki huo Nyerere alikuwa mwalimu wa Pugu secondary

Baadae hiki kikundi kikaon kinahitaji mtu wa kumsimamisha mwenye kariba km ya Mwalimu Nyerere ndipo walipoenda Pugu secondary na kukutana na Mwalimu Nyerere na kumpa mikakati
Kabla ya hilo kundi kudai uhuru watu walikuwa wanafurahia kunyonywa. Tangia muarabu aanze kuja kuuza ndugu zetu kama watumwa watu walikuwa wananungunika na kugombana kutoka katika hali ya Unyonyaji. Mjerumani alivyokuja wapo kina Mkwakwa n.k.

Sasa kusema kwamba hilo kundi ndio lilikuwa na wazo la kudai uhuru na Nyerere alikuwa tu pugu anashika chaki. Basi hilo kundi lisingemfuata Nyerere bali lingemfuata jamaa yoyote pale mtaani.
 
Sijawahi kusoma mada za huyo Mohammed ila historia huwa haifutiki

Ninachokijua mimi ni kwamba kuna kikundi cha watu kilicho anzishisha chokochoko za kudai Uhuru wengi wao wakiwa ni wakazi wa Dar es salaam waki huo Nyerere alikuwa mwalimu wa Pugu secondary

Baadae hiki kikundi kikaon kinahitaji mtu wa kumsimamisha mwenye kariba km ya Mwalimu Nyerere ndipo walipoenda Pugu secondary na kukutana na Mwalimu Nyerere na kumpa mikakati
Wazolee,
Nakuwekea hapo chini historia ilivyokuwa:

Pablo Blanco said:
ok,yaishe mzee wangu,wewe ni mtu wa heshima sana, naomba historia hii adimu ya nyerere kuwa mwenyekiti
''Pablo,
TAA hawakuwa na Mwenyekiti walikuwa na President.

1950 palifanyika mapinduzi TAA kuwatoa madarakani TAA President Mwalimu Thomas Plantanna Katibu Clement Mtamila.

Waliopanga na kukamilisha mapinduzi haya walikuwa Hamza Mwapachu na Abdul Sykes wakisaidiwa na Schneider Abdillah Plantan.

Sababu ya mapinduzi haya ni kuwa TAA chini ya uongozi wa Mwalimu Thomas ilishindwa kukidhi mategemeo ya wanachama ambao walitaka kuiona TAA inaingia katika siasa za kuitoa nchi katika mikono ya Waingereza.

Kutokana na mapendekezo ya TAA Constitutional Development Committee ambao wajumbe walikuwa Mufti Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Said Chaurembo, Hamza Mwapachu, Steven Mhando, Abdul Sykes na John Rupia yaliyopelekwa kwa Gavana Edward Twining, serikali ikishtushwa sana kwani mapendekezo yalizungumza ''kura moja mtu mmoja,'' na Tanganyika huru 1963.

Earle Seaton Mwanasheria kutoka Bermuda aliyekuwa akifanya shughuli zake za uwakili Moshi alisaidia sana katika kutayarisha mapendekezo haya.

Huyu Seaton alikuwa rafiki wa Abdul Sykes.

Kutokana na mapendekezo haya Dr. Kyaruzi akahamishwa kupelekwa Jela ya Kingolwira kisha Nzega.

Hii ilikuwa njama za Twining kupangua uongozi thabiti wa TAA.
Mwapachu akapelekwa Nansio, Ukerewe.

Abdul Sykes akashika nafasi ya Dr. Kyaruzi akawa Kaimu Rais na Secretary.
Huko nyuma Abdul na Mwapachu walikuwa wamepanga kuibadili TAA kuwa chama cha siasa.

Kuanzia mwaka wa 1951 Abdul akawa na mazungumzo na Chief David Kidaha Makwaia kumtaka ajiunge na TAA wamchague Rais wa TAA na kisha waunde TANU kwenye mkutano mkuu wa TAA wa mwaka unaofuatia.

Mazungumzo haya hayakuzaa matunda.
Mwaka wa 1952 Julius Nyerere akaja Dar es Salaam kama mwalimu Pugu.

Joseph Kasella Bantu akampeleka Nyerere nyumbani kwa Abdul Sykes kumtambulisha.

Unaweza ukasema safari ya Nyerere kuja kuwa kiongozi kwa kuchaguliwa kwanza kuwa TAA President 1953 inaanza hapa.''

Itaendelea...
 
Nakupongeza kwa maandishi na hoja zenye upeo na akili kwa jumla. Mzee MS kwa sisi tunaofahamu asili ya imani yake anayoitetea kwa hila hatushangai ila tunampuuza!
Tabia yake ya kugeuzageuza mambo kwa hila ndiyo pia iliyounda hiyo imani yake! Kupindua pindua historia, kuchanganya uongo na ukweli, hila n.k...
Mzizi...
Ukweli ni upi?
Nitafurahi kukusoma.
 
Wazolee,
Tunaendelea...
Kuanzia mwaka wa 1952 Nyerere alipokutana na Abdul Sykes kulikuwa na mazungumzo baina ya Abdul Sykes na Hamza Mwapachu kuhusu kumuingiza Nyerere katika uongozi wa TAA kama rais katika uchaguzi wa mwaka wa 1953.

Haya ni baada ya mazungumzo kati ya Abdul Sykes na Chief Kidaha Makwaia kutofikia muafaka.

Miezi ya mwanzo ya mwaka wa 1953 Abdul akiongoza na Ali Mwinyi Mwinyi Tambwe walisafiri kwenda Nansio kwa Hamza.

Huyu Ali Mwinyi Tambwe alikuwa Katibu wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika, yaani umoja wa Wasilam wa Tanganyika chama alichoasisi Kleist Sykes mwaka wa 1933 akiwa Katibu na Mzee bin Sudi akiwa Rais.

Viongozi hawa walishika nafasi hizo hizo pia katika African Association.

Abdul alitaka kauli ya mwisho kutoka kwa Hamza kuhusu Nyerere kama yeye ampishe Nyerere kwenye nafasi ya urais na amsaidie kushinda nafasi hiyo na mwaka unaofuatia 1954 waunde TANU na kudai uhuru wa Tanganyika.

Hamza alkuwa anaamini kuwa kwa ngwe ile iliyobakia kwa Waafrika kupata nchi yao Nyererealikuwa anafaa sana katika kuongoza vita vile kuliko Abdul Sykes.

Hamza alimtaka Abdul amsaidie Nyerere kuchukua uongozi kwani kwa siasa za Dar es Salaam za wakati ule ikiwa Abdul atagombea urais wa TAA dhidi ya Nyerere kwa nia ya kupata ushindi, Nyerere asingeweza kumshinda Abdul hata kidogo kwani chama chenyewe kilikuwa kinaishi ndani ya nyumba ya akina Sykes kuanzia mwaka wa 1929 baba yake Abdul alipokuwa Katibu muasisi wa African Association na 1950 Abdul alipoingia katika uongozi wa TAA baada ya kifo cha baba yake 1949.

Lakini kubwa ambacho Hamza alimweleza Abdul ni kuwa yeye Abdul ni Muislam na ikiwa ataongoza harakati za uhuru Waingereza watachukulia hilo kama vurugu zingine za Waislam dhidi ya serikali lakini Nyerere kama Mkristo Waingereza hawatokuwa na hofu kubwa.

Ikiwa historia ya TANU itaandikwa bila kuwataja Hamza Mwapachu na Abdul Sykes mengi sana katika historia ya Nyerere yatapotea na kwa hakika historia yenyewe ya TANU.

Sasa unaweza kusoma kuhusu uchaguzi ule wa mwaka wa 1953 kati ya Abdulwahid Kleist Sykes na Julius Kambarage Nyerere uliofanyika Ukumbi wa Arnautoglo tarehe 17 April 1953 hapo chini:

www.jamiiforums.com

Ukumbi wa Arnautoglo safari ndefu ya Mwalimu Nyerere ilipoanzia - JamiiForums
UKUMBI WA ARNAUTOGLO SAFARI NDEFU YA MWALIMU NYERERE ILIPOANZIA George Arnautoglo alikuwa Mgiriki tajiri na ndiye aliyejenga jumba hilo akalitoa kwa matumizi ya Waafrika wa Tanganyika. George Arnautoglo alikuwa hawapendi Waingereza kwa kuwa walikuwa wameikalia nchi yake Greece ambako Padri...
www.jamiiforums.com
www.jamiiforums.com
 
Back
Top Bottom