GE2025 Mzee Mbembe: Rais Samia alitupeleka Wasanii Korea kujifunza, Oktoba tuka Tiki tu!

GE2025 Mzee Mbembe: Rais Samia alitupeleka Wasanii Korea kujifunza, Oktoba tuka Tiki tu!

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Mwigizaji maarufu kama Mzee Mbembe, amesema, Serikali ya Awamu ya Sita ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, imewafanyia makubwa wasanii nchini ikiwemo kuwapa fursa ya kusafiri nchini Korea Kusini kujifunza zaidi kuhusu teknolojia mpya za uandaaji filamu na tamthilia pia kuhusu masoko na mbinu mpya za uwasilishaji.

Amesema hayo leo Septemba 13 kwenye Uwanja wa Kandahar, Jimbo la Kigoma Kusini kwaajili ya kumuunga mkono Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, anayenguruma ndani ya Mkoa wa Kigoma akielezea miradi mikubwa ya kimaendeleo iliyotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia.

 
Back
Top Bottom