Mzee Kinana alizunguka nchi nzima kukinadi chama lakini kipindi hiki mmh!

kalisheshe

JF-Expert Member
Mar 19, 2020
867
1,000
Waswahili wanasema Moto ukiwaka sana basi unaelekea kuzima.

Ilikua kidogo tu CCM ife vibaya kipindi Cha Kikwete ila uwepo wa watu machachali Kama Nape Nnauye, Kinana na wengine ulifanya chama chetu kibaki kwenye ramani.

Hali Ni tofauti Sana kipindi hiki, kwa wasiofahamu wanaweza kuhisi chama kiko imara sana ila kwa sisi tulioko ndani tunakiona kinachotokea.

CCM ya kipindi hiki imejaa mamluki wengi sana, ambao wamekuja kwa maslahi yao binafsi. Nakumbuka wakati nipo chuoni, vijana wengi walikuja kuchukua kadi za chama ili tu waonekane kwenye soko la ajira.

Wengine waliamua kuwa active baada ya kuona Mwenyekiti anafanya teuzi nyingi kutoka UVCCM. Msiwaone vijana wengi wanaimba nyimbo za chama mkahisi Ni wafia chama la hasha! Hao wapo kimaslahi zaidi.

Chama kinahitaji watu imara sana kipindi hiki kuliko kipindi kingine chochote, tukiombee Sana chama hiki Kama bado tunakipenda.
 
kalisheshe

JF-Expert Member
Mar 19, 2020
867
1,000
CCM ya Makamba ilikuwa ya kihuni sana ,ilikuwa himaya ya kundi flani ,Knana.akajaribu kuokoa jahazi ,lakini aleikoa ccm ni mgombea wao Magufuli na kakisuka chama haswa,ndio maana wengi wanagombea kupitia chama hicho,imani imerudishwa ndani ya chama
Sisi tulioko ndani ndo tunaelewa kinachoendelea. Tusiposhtuka mapema tutapigwa vibaya sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lusungo

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
21,461
2,000
CCM ya Makamba ilikuwa ya kihuni sana ,ilikuwa himaya ya kundi flani ,Knana.akajaribu kuokoa jahazi ,lakini aleikoa ccm ni mgombea wao Magufuli na kakisuka chama haswa,ndio maana wengi wanagombea kupitia chama hicho,imani imerudishwa ndani ya chama.
Teh teh unacomment utafikiri hutumii bundle ya Lumumba
 
matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
2,974
2,000
JPM haitaji hayo. Wale walikomaa kwa sababu hawakuwa na walichokifanya.
Sasa huyu alitakiwa asizunguke popote bali ahutubie taifa siku moja tu kabla ya uchaguzi
 
Proved

JF-Expert Member
Sep 10, 2018
10,331
2,000
Kipindi hiki atazunguka Polepole na Bashiru bila kumsahau Musiba hivyo ondoa hofu ya kushindwa.
 
mandolo

Senior Member
May 21, 2020
183
500
JPM haitaji hayo. Wale walikomaa kwa sababu hawakuwa na walichokifanya.
Sasa huyu alitakiwa asizunguke popote bali ahutubie taifa siku moja tu kabla ya uchaguzi
Toka zako hapa, hata wiki2 hazijaisha tangu Rais Kikwete atufumbue macho. Kumbe miradi hii mnayoitegemea iwasadie kwenye kampeni yeye ni founder.
 
Chintu

JF-Expert Member
Feb 4, 2011
5,226
2,000
Ile CCM ya akina Kinana na Nape ndiyo tuliyokuwa tumeichoka,
ndio maana hata Mabango walikuwa wanaandika CHAGUA MAGUFULI.
CCM ya sasa ndiyo hasa iliyokuwa inatakiwa na wananchi. Sio ile ya "unanijua mimi?"
 
LESIRIAMU

JF-Expert Member
Feb 12, 2008
6,317
2,000
Nilisema Mh hana washauri wa kweli? Kuna walio ni beza kwa vile hawajui nilikuwa na maana gani.. Asante kwa kuendelea kuwainyesha picha.

Hata leo bado kachemka kusema kampeni za ufunguzi zifanyike Dodoma. Hkuangalia alipata wapi kura nyingi awape hiyo heshima.

Hakuangalia population ya Dodoma na miji mingine ili aone upepo ukoje? Kama ni marekebisho yafanyike mapema. Au kwa vile watu wao husombwa kwa malipo hamna shida.. Ila siwaamini washauri wa huyu baba.
 
Ningeshauri rais wa nchi asiwe mwenyekiti wa chama, naona majukumu yanakuwa mengi mpaka anaelemewa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
LESIRIAMU

JF-Expert Member
Feb 12, 2008
6,317
2,000
CCM ya Makamba ilikuwa ya kihuni sana ,ilikuwa himaya ya kundi flani ,Knana.akajaribu kuokoa jahazi ,lakini aleikoa ccm ni mgombea wao Magufuli na kakisuka chama haswa,ndio maana wengi wanagombea kupitia chama hicho,imani imerudishwa ndani ya chama.
Hapo uko nje ya reli. Wengi wana gombea kwa kutumia nyota ya Magu. Pia kuamini hata akishindwa ata tangazwa kama kwenye chaguzi ndogo. Hakuna mwenye uchungu n chama hapo. Wote ni maslahi binafsi..
 
FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
20,874
2,000
Walikuwa na Nape..Mzee wa mabao ya mkono....kijana akaambulia kuvunjika mkono na kufukizwa uwaziri kisa kuligusa toto la ba mkubwa!!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom