Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,266
Mzee wa miaka 60 mkazi wa Kijiji cha Isasa Wilayani Nkasi, Charles Gervais amejiua kwa kunywa sumu kutokana na kinachoelezwa kuwa ni wivu wa mapenzi
Taarifa za awali za Polisi zinaeleza kuwa, Gervais alichukuwa uamuzi wa kujiua kwa kunywa sumu baada ya kukataliwa na mkewe Maria Mtete(35) ambaye alimtaka mume huyo ampatie talaka kwa kuwa amempata Mwanamume mwingine ambaye ni rika lake
Kamanda wa polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa ni la usiku wa kuamkia jana katika Kijiji cha Isasa, wilayani Nkasi. Alisema Gervais alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu katika kituo cha Afya katika Kata ya Kirando, mwambao wa ziwa Tanganyika wilayani Nkasi
"Mzee huyo alikunywa sumu ambayo haijajulikana mara moja, aliamua kukatiza maisha yake kwa kuchukua uamuzi huo baada ya kukataliwa na mkewe Maria Mtete ambaye alidai waachane kwa kuwa alikuwa amepata Mwanamume mwingine", alieleza Kamanda
Alisema mwili umehifadhiwa katika chumba cha maiti katika kituo cha Afya cha Kirando kwa uchunguzi ili kubaini aina ya sumu aliyokunywa.
Aidha, Kamanda alisema Mke wa marehemu alitoroka baada ya tukio hilo.
Chanzo: HabariLeo