Mzazi: Zawadi ya kwanza kwa mtoto aliyezaliwa leo

Econometrician

JF-Expert Member
Oct 25, 2013
16,626
30,597
Wazazi sote tunatambua jina analopewa mtoto mara tu anapozaliwa ndio zawadi yake ya kwanza kutoka kwa mzazi/wazazi wake. Je hadi sasa jina ulilompa mwanao kama zawadi yake ya kwanza lina akisi uhalisia wa jina?

Mfano ni gaidi wa aina yake ambaye hajawahi kutokea duniani Ilyich Ramírez Sánchez a.k.a Carlos the Jackal jina lake la kwanza Ilyich alipewa na baba yake ili kumuenzi aliyekuwa mwanamapinduzi wa urusi Vladimir Ilyich Ulyanov na kweli carlos baada ya kukua alikuwa mwanamapinduzi haswa akipinga sera za kimagharibi.

Je jina la mwanao lina akisi uhalisia wa jina na nini ilikuwa sababu ya kumuita kwa hilo jina? (case study iwe kwa mtoto wako wa kwanza kuzaliwa-first born )
 
kwavile sijapata mtoto , naomba nijirefer mimi kwa vile ni first born , jina langu walilonipa linamaanisha wealthy , na kweli mambo yangu si mabaya , tukija kwenye jina la kiukoo walilonipa linashabihiana na mambo nnayopenda kweli, sema nimeshindwa kuweka majina hapa sababu ya privacy
 
Walinipa jina la ndugu wa baba ambaye hata hakuwahi kumuona. Utotoni nilimuuliza sana mzee na hakuwa na majibu. Walinipa chance ya kumpa last born wetu jina.
 
Wazazi sote tunatambua Jina analopewa mtoto mara tu anapozaliwa ndio zawadi yake ya kwanza kutoka kwa Mzazi/Wazazi wake.Je hadi sasa Jina ulilompa Mwanao kama zawadi yake ya kwanza lina akisi uhalisia wa jina ???
Mfano ni gaidi wa aina yake ambaye hajawahi kutokea duniani Ilyich Ramírez Sánchez a.k,a Carlos the Jackal jina lake la kwanza Ilyich alipewa na baba yake ili kumuenzi aliyekuwa mwanamapinduzi wa urusi Vladimir Ilyich Ulyanov na kweli carlos baada ya kukua alikuwa mwanamapinduzi haswa akipinga sera za kimagharibi. Je jina la mwanao lina akisi uhalisia wa jina na nini ilikuwa sababu ya kumuita kwa hilo jina?? (case study iwe kwa mtoto wako wa kwanza kuzaliwa-first born )
Magufuli... Kwa sababu mtoto aje kua mchapakazi na ajue maana ya uzalendo na uadilifu ni nini na sio porojo.
 
Yaani mimi jina langu liko vice-versa kabisa na mimi mwenyewe
 
Zawadi ya kwanza niliyompa ni kujithamini kwa kumpa jina la kiswahili. Sijutii na yeye naona anafurahia kuchangamana kikwetukwetu
 
kwavile sijapata mtoto , naomba nijirefer mimi kwa vile ni first born , jina langu walilonipa linamaanisha wealthy , na kweli mambo yangu si mabaya , tukija kwenye jina la kiukoo walilonipa linashabihiana na mambo nnayopenda kweli, sema nimeshindwa kuweka majina hapa sababu ya privacy
hongera kwa hilo
 
Zawadi ya kwanza niliyompa ni kujithamini kwa kumpa jina la kiswahili. Sijutii na yeye naona anafurahia kuchangamana kikwetukwetu
Mkuu Kuna mdogo wangu wa kike alipata mapacha akaniomba niwape wanae majina nilichagua majina mazuri ya kiafrika-ya kiswahili cha ajabu alipo kwenda kuwabatiza padre akawabadilisha majina akawaita John na Joseph nilichukia sana
 
Unapomtolea mtoto wako jina hakikisha unampa jina zuri.
Ona sasa
Screenshot_2017-01-12-09-48-38-1.png
Screenshot_2017-01-12-09-48-04-1.png
 
Dah... Kabla ya 2020....nataka nifyatue Magufuli aje kuwaongoza kaka zake.. Naona kama wanakuwa wazembe wazembe hivi... Sijajua nitafyatua na nani bado... Maana IQ ya mtoto hutoka kwa mama
 
Mkuu Kuna mdogo wangu wa kike alipata mapacha akaniomba niwape wanae majina nilichagua majina mazuri ya kiafrika-ya kiswahili cha ajabu alipo kwenda kuwabatiza padre akawabadilisha majina akawaita John na Joseph nilichukia sana
Ye naye alikubalije wabatizwe kwa majina ya kizungu? Hizi dini ukiziendekeza unakua mtumwa milele. Next time mwambie dada yako asikubali tena huo ujinga wa wakatoliki
 
Back
Top Bottom