Mzalendo wa kweli ni nani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mzalendo wa kweli ni nani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by chama, Mar 9, 2012.

 1. c

  chama JF-Expert Member

  #1
  Mar 9, 2012
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kauli ya mh. waziri mkuu Pinda imeniacha nikujiuliza maswali mengi ni nani mzalendo wa kweli kwenye taifa hili. Mh. Pinda umedai madaktari wamekuwa si wazalendo kwa kitendo chao cha kuitisha mgomo nchi nzima; lingekuwa ni jambo la busara kama mh. Pinda ungeupima uzalendo wako kabla ya kuwatuhumu madaktari. Mh. Pinda ni lazima ufahamu kitendo cha madaktari kugoma kimesababishwa na wewe binafsi kukosa uzalendo; umeangalia maslahi ya kisiasa zaidi na kuwaacha watanzania wasio na hatia wakiteseka kwa kukosa matibabu; bado kuna familia zinaomboleza misiba waliyoipata kwenye mgomo wa awali. Hivi kabla hujakuja na kauli finyu ya kukosa uzalendo uliliangalia Bunge lako na mawaziri wako? Labda ungetutajia ni nani kati yao ni mzalendo, wote mmegeuka washirika wa ufujaji na wizi wa mali ya umma. Mh. Pinda badala ya kutafuta suluhisho la kudumu umekuja na hoja ya eti serikali imejipanga kukabiliana na mgomo huo ni ulaghai wa wazi kwa watanzania hilo ni suluhisho la muda mfupi tu; kumbuka hata kabla ya vuguvugu la migomo utendaji wa kazi wa madaktari wetu ulikuwa duni kutokana na maslahi duni, kwa kukumbusha tu ili mtanzania wa kawaida apate huduma bora ni lazima ujuane na daktari mhusika au umpe chochote. Mpo wanasiasa mnaodai fani ya udaktari ni wito nakubaliana nanyi ila labda niwakumbushe kidogo wakati wa Mwl. Nyerere siasa ilikuwa ni wito ilikuwa ni aghalabu kumuona mwanasiasa amejilimbikizia mali; siku hizi mmebadili mfumo siasa ni biashara, viongozi mmekuwa hamna maadili. Leo inakuwaje madaktari wanapokuwa na madai ya msingi muwaone wamekosa uzalendo? Hivi ikitokea mawaziri wako wakiona huna uwezo wa kuwaongoza utakuwa na sababu gani ya kung`ang`ania madaraka? Umemshauri mh. Raisi aongee na wazee wa Dar es salaam, kumbuka wazee wa Dar es salaam hawawakilishi maoni ya wazee wa Tanzania. Mh. Pinda badala ya kukurupuka na jazba za kisiasa tumia hekima; ikiwa mgomo wa madaktari unakushinda hivi utaweza kumudu mgomo wa wafanyakazi Tanzania iwapo utatokea?

  Chama
  Gongo la Mboto DSM
   
 2. T

  The Infamous JF-Expert Member

  #2
  Mar 9, 2012
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 719
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  mimi hapa ninachokiona ni hawa mawaziri wawili kuwa wazalendo, wajiuzuru, wasisubiri Raisi awanongoneze, wafanye uzalendo tu kama wa Mh Lowasa, sio kesi...
   
Loading...