Myahudi wa kwanza kuswalisha Waislam

Myahudi wa kwanza kuswalisha Waislam

Bi mdogo uliyeingia choo cha kiume, kumbe upo! Mi nilishkusahau.

Hainiingii akilini mpinzani utuonye kwamba tutaanguka, tangu lini mtu akamtakia heri adui yake? Lowassa huyu alikuwa kiongozi kwenye chama chako, mkaanzisha ngonjera za KUVUA GAMBA mkafyata, kwa nini UMMA usiamini kwamba ni msafi?

Shida yenu mmecheza ngoma msiyoijua asili yake sasa mnatapatapa. Kama una mashaka na Lowassa pole
 
MYAHUDI wa kwanza kuswalisha WAISLAMU.

M/kiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Tanzania akiwa anaingia kwenye kikao cha NEC ya tarehe 11 June, whitehouse Dodoma na kushuhudia maajabu akatamka "HAIJAPATA KUTOKEA"

Waacheni watanzania wapigwe na butwaa, waacheni wajae kwenye mikutano yake wakimshangaa kwani HAIJAPATA KUTOKEA ktk historia ya Tanzania na Afrika.

Ni vigumu sana kwa MYAHUDI kuswalisha katika msikiti wa WAISLAMU, kama ilivyokuwa kwa KIONGOZI wa CUF kuisimamia ILANI ya TLP, lakini wapo wayahudi kadhaa wamewahi kufanya hivyo.

Kwa kawaida watu hununua wanasiasa, wakawatumia kwa maslahi yao, kuwasemea ajenda zao, nasema ni kawaida kwa sababu inatokea siku zote na tumeyashuhudia yakitokea, hivyo kwangu ama kwetu ni kawaida wanasiasa kununuliwa.

Lakini katika historia ya Tanzania na Afrika ni MZEE WA KIBO pekee, ndio aliyeweka historia ya kununua CHAMA CHA SIASA kizima kizima, na hakuishia hapo akanunua na MUUNGANO wa vyama vya siasa ili asimame kama mgombea, na amefanikiwa.....nasema kama alivyosema JAKAYA, haijapata kutokea.

Historia hii ya kipekee ilitanguliwa na mtu mmoja tu, anaitwa GIOVANNI LEONE, ambaye alikuwa Kiongozi wa Chama cha Wakristo cha Italy ( DEMOCRAZIA CRISTIANA ama CHRISTIAN DEMOCRACY) ambaye HAKUWAHI kuwa mkristo., lakini aliweka historia ya kuwa kiongozi wa Wakristo ambaye hakuwa Mkristo.

Bwana huyu aliingia madarakani kama WAZIRI MKUU- tarehe 21 June 1963 na kujiuzulu miezi sita baadae tarehe 4 December 1963 kwa kashfa ya Ufisadi.

Mwaka 1968, aliingia tena madarakani baada ya kununua MUUNGANO WA VYAMA VYA UPINZANI ITALY ulioitwa THE PENTAPARTITO ambao uliundwa na vyama vitano kikiwemo PSI, PSDI, PRI, PLI na DC.

LAKINI kama wasemavyo waswahili jasiri haachi asili, Bwana LEONE alidumu madarakani kwa miezi sita tena kwa maana kuanzia tarehe 24 June - 22 Dec 1968 pale ambapo BUNGE lilimuondoa kutokana na matumizi mabaya ya nafasi yake kama Waziri Mkuu wa Italy.

Ni kama GIOVANNI LEONE, EDWARD NGOYAI LOWASSA ameamua kufuata nyazo zake, kitabia na mwenendo wake kisiasa. Itakuwa vigumu kwa LOWASSA kufuata misingi hasiyoijua ya UKAWA, na vigumu kutekeleza ILANI hasiyoijua wala kushiriki kuiandaa na itakuwa vigumu kwake KUAMINI ktk UKAWA ama CHADEMA kwani kwake Chama hicho ni Mama wa Kambo.

Mimi ninabaki na mshangao kama vile watanzania wenzangu wanavyoendelea kumshangaa LOWASSA...HAIJAPATA KUTOKEA kada kindaki ndaki wa CCM kuwa JEMEDARI wa wapinzani...ONLY IN TANZANIA.
 
Hizi makala utaziandika nyingi sana siku hizi, ili ufikiriwe kwenye kura za viti maalumu...
 
Huyu Juliana si alikuwa CHADEMA mbona alipotimuliwa na kuwa Gamba ameishia kupewa nafasi ya kugombea ubunge viti maalum, mbona hatushangai mama ???. Au ndio ya Nyani haoni la kwake
 
Ishu ya Lowassa kuhamia UKAWA na kupewa nafasi ya kugombea Urais ina maudhui mapana mno kuliko suala la kuuongoza upinzani . Fuatilia maneno ya Kina Freeman Mbowe na wengine ....kuna tafsiri za mikakati ya huko mbele mabayo kam unavyosema, itakuja kuwashangaza wengi!

Wenye akili ndogo hawaelewagi.
Akili kubwa ishakuelewa.
Hivi huyo dada aliyeanzisha huu uzi ana nafasi gani huko CCM kwa sasa?
 
Dada katoa mawazo yake kama kukubali tukubali kwa hoja na kama kukataa tukatae kwa hoja sio kutumia jazba na matusi tunajenga uadui wakati sisi wote ni taifa moja...!!
 
MYAHUDI wa kwanza kuswalisha WAISLAMU.

M/kiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Tanzania akiwa anaingia kwenye kikao cha NEC ya tarehe 11 June, whitehouse Dodoma na kushuhudia maajabu akatamka "HAIJAPATA KUTOKEA"

Waacheni watanzania wapigwe na butwaa, waacheni wajae kwenye mikutano yake wakimshangaa kwani HAIJAPATA KUTOKEA ktk historia ya Tanzania na Afrika.

Ni vigumu sana kwa MYAHUDI kuswalisha katika msikiti wa WAISLAMU, kama ilivyokuwa kwa KIONGOZI wa CUF kuisimamia ILANI ya TLP, lakini wapo wayahudi kadhaa wamewahi kufanya hivyo.

Kwa kawaida watu hununua wanasiasa, wakawatumia kwa maslahi yao, kuwasemea ajenda zao, nasema ni kawaida kwa sababu inatokea siku zote na tumeyashuhudia yakitokea, hivyo kwangu ama kwetu ni kawaida wanasiasa kununuliwa.

Lakini katika historia ya Tanzania na Afrika ni MZEE WA KIBO pekee, ndio aliyeweka historia ya kununua CHAMA CHA SIASA kizima kizima, na hakuishia hapo akanunua na MUUNGANO wa vyama vya siasa ili asimame kama mgombea, na amefanikiwa.....nasema kama alivyosema JAKAYA, haijapata kutokea.

Historia hii ya kipekee ilitanguliwa na mtu mmoja tu, anaitwa GIOVANNI LEONE, ambaye alikuwa Kiongozi wa Chama cha Wakristo cha Italy ( DEMOCRAZIA CRISTIANA ama CHRISTIAN DEMOCRACY) ambaye HAKUWAHI kuwa mkristo., lakini aliweka historia ya kuwa kiongozi wa Wakristo ambaye hakuwa Mkristo.

Bwana huyu aliingia madarakani kama WAZIRI MKUU- tarehe 21 June 1963 na kujiuzulu miezi sita baadae tarehe 4 December 1963 kwa kashfa ya Ufisadi.

Mwaka 1968, aliingia tena madarakani baada ya kununua MUUNGANO WA VYAMA VYA UPINZANI ITALY ulioitwa THE PENTAPARTITO ambao uliundwa na vyama vitano kikiwemo PSI, PSDI, PRI, PLI na DC.

LAKINI kama wasemavyo waswahili jasiri haachi asili, Bwana LEONE alidumu madarakani kwa miezi sita tena kwa maana kuanzia tarehe 24 June - 22 Dec 1968 pale ambapo BUNGE lilimuondoa kutokana na matumizi mabaya ya nafasi yake kama Waziri Mkuu wa Italy.

Ni kama GIOVANNI LEONE, EDWARD NGOYAI LOWASSA ameamua kufuata nyazo zake, kitabia na mwenendo wake kisiasa. Itakuwa vigumu kwa LOWASSA kufuata misingi hasiyoijua ya UKAWA, na vigumu kutekeleza ILANI hasiyoijua wala kushiriki kuiandaa na itakuwa vigumu kwake KUAMINI ktk UKAWA ama CHADEMA kwani kwake Chama hicho ni Mama wa Kambo.

Mimi ninabaki na mshangao kama vile watanzania wenzangu wanavyoendelea kumshangaa LOWASSA...HAIJAPATA KUTOKEA kada kindaki ndaki wa CCM kuwa JEMEDARI wa wapinzani...ONLY IN TANZANIA.
 
Na bado mtahangaika sana hakuna rangi mtaacha ona mwaka huu.
 
Kwani hujaona it is also only in Tanzania mambo yanafanyika ambapo kwingine yasingeweza. Twiga kuingia kwenye ndege bila mtu kujua nk nk
 
unapoteza muda, watanzania wameamua mabadiliko, wewe baki na wazee hukohuko lumumba ya ukawa yanakuwashia nini.
 
Juliana Shonza

Hivi ni kusema Lowassa anashinda urais, lakini hukubaliani na njia (means) anayotumia...
 
Last edited by a moderator:
Juliana Shonza

Hii taarabu ipeleke chalinze

Watanzania wanataka mabadiliko so hata ukisema lowasa atawauza wote utumwani watamchagua lowasa

Hata ukiweka mbuzi na CCM watu watachagua mbuzi

So beat it
 
Last edited by a moderator:
Miaka 54 ya Uhuru. Labda hiki ndicho tunachojivunia.
Kwa Mtanzania wa sasa hivi anaeipenda ccm, ujue eidha mzazi Mmoja wapo au wote wana ajira ccm mfano baba ni katibu/mwenyekiti n.k nyumba ya ccm, gari la ccm na accommodation zote zinatoka ccm hilo sina tatizo nao.
Lakini kwa Mtanzania mwenzangu na mimi kuishabikia ccm na hali halisi iliyopo inabidi achekiwe akili. Bora ukimwi kuliko ccm.
 
Attachments

  • 11873478_827494597347835_135105622057025183_n.jpg
    11873478_827494597347835_135105622057025183_n.jpg
    80.6 KB · Views: 71
  • 515a31bc957016dd79d62313a0d7dfe0afb1e05a.jpeg
    515a31bc957016dd79d62313a0d7dfe0afb1e05a.jpeg
    37.8 KB · Views: 58
Back
Top Bottom