Myahudi wa kwanza kuswalisha Waislam

Myahudi wa kwanza kuswalisha Waislam

Juliana Shonza

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2012
Posts
2,009
Reaction score
1,607
M/kiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Tanzania akiwa anaingia kwenye kikao cha NEC ya tarehe 11 June, whitehouse Dodoma na kushuhudia maajabu akatamka "HAIJAPATA KUTOKEA"

Waacheni watanzania wapigwe na butwaa, waacheni wajae kwenye mikutano yake wakimshangaa kwani HAIJAPATA KUTOKEA ktk historia ya Tanzania na Afrika.

Ni vigumu sana kwa MYAHUDI kuswalisha katika msikiti wa WAISLAMU, kama ilivyokuwa kwa KIONGOZI wa CUF kuisimamia ILANI ya TLP, lakini wapo wayahudi kadhaa wamewahi kufanya hivyo.

Kwa kawaida watu hununua wanasiasa, wakawatumia kwa maslahi yao, kuwasemea ajenda zao, nasema ni kawaida kwa sababu inatokea siku zote na tumeyashuhudia yakitokea, hivyo kwangu ama kwetu ni kawaida wanasiasa kununuliwa.

Lakini katika historia ya Tanzania na Afrika ni MZEE WA KIBO pekee, ndio aliyeweka historia ya kununua CHAMA CHA SIASA kizima kizima, na hakuishia hapo akanunua na MUUNGANO wa vyama vya siasa ili asimame kama mgombea, na amefanikiwa.....nasema kama alivyosema JAKAYA, haijapata kutokea.

Historia hii ya kipekee ilitanguliwa na mtu mmoja tu, anaitwa GIOVANNI LEONE, ambaye alikuwa Kiongozi wa Chama cha Wakristo cha Italy ( DEMOCRAZIA CRISTIANA ama CHRISTIAN DEMOCRACY) ambaye HAKUWAHI kuwa mkristo., lakini aliweka historia ya kuwa kiongozi wa Wakristo ambaye hakuwa Mkristo.

Bwana huyu aliingia madarakani kama WAZIRI MKUU- tarehe 21 June 1963 na kujiuzulu miezi sita baadae tarehe 4 December 1963 kwa kashfa ya Ufisadi.

Mwaka 1968, aliingia tena madarakani baada ya kununua MUUNGANO WA VYAMA VYA UPINZANI ITALY ulioitwa THE PENTAPARTITO ambao uliundwa na vyama vitano kikiwemo PSI, PSDI, PRI, PLI na DC.

LAKINI kama wasemavyo waswahili jasiri haachi asili, Bwana LEONE alidumu madarakani kwa miezi sita tena kwa maana kuanzia tarehe 24 June - 22 Dec 1968 pale ambapo BUNGE lilimuondoa kutokana na matumizi mabaya ya nafasi yake kama Waziri Mkuu wa Italy.

Ni kama GIOVANNI LEONE, EDWARD NGOYAI LOWASSA ameamua kufuata nyazo zake, kitabia na mwenendo wake kisiasa. Itakuwa vigumu kwa LOWASSA kufuata misingi hasiyoijua ya UKAWA, na vigumu kutekeleza ILANI hasiyoijua wala kushiriki kuiandaa na itakuwa vigumu kwake KUAMINI ktk UKAWA ama CHADEMA kwani kwake Chama hicho ni Mama wa Kambo.

Mimi ninabaki na mshangao kama vile watanzania wenzangu wanavyoendelea kumshangaa LOWASSA...HAIJAPATA KUTOKEA kada kindaki ndaki wa CCM kuwa JEMEDARI wa wapinzani...ONLY IN TANZANIA.
 
Rekebisha Title Yako Dada Haviendani Na Maudhui. Mambo Ya Udini Yameingiaje Tena Huku? Au Unataka Wachangiaji Wengi!
 
Shonza ww je umejisahau au ? Ulikua na damu ya mapinduz lkn umehamia kwa wazee
 
Rekebisha Title Yako Dada Haviendani Na Maudhui. Mambo Ya Udini Yameingiaje Tena Huku? Au Unataka Wachangiaji Wengi!
Shifa yako ni uelewa tu..,sio kila linalotajwa kwa jina la dini linahusu dini...elewa maudhui usipotee kwenye lugha ya picha na mafumbo ukakosa maana.
 
mi nalimshangao kwa wewe binti jinsi unavyojidhalilisha hapa JF
 
Ishu ya Lowassa kuhamia UKAWA na kupewa nafasi ya kugombea Urais ina maudhui mapana mno kuliko suala la kuuongoza upinzani . Fuatilia maneno ya Kina Freeman Mbowe na wengine ....kuna tafsiri za mikakati ya huko mbele mabayo kam unavyosema, itakuja kuwashangaza wengi!
 
Naona umekuwa reporter wa Mwenyekiti wa CCM siku hizi! Kaazi kwelikweli!
 
siamini la kununua chama, ni mawazo yako, ila inawezekana ameenda kwa hasira na wao wakampokea kwa manufaa yao! hakuna mwenya ushahidi wa kununua chama, ni ngonjera tu, waliompokea na yeye kila mtu ana manufaa yake binafsi
 
Lowasa atakuwa deppressed baada ya uchaguzi huu pale shamrashamra, vifijo, nderemo na misafara ya bodaboda itakapokuwa haipo, pale atakapobaki peke yake na familia yake huku magazeti hayamuandiki tena. Atakuwa the Lone man!
 
Msiibe kura tu nyie maccm..ila hivi hamna hata ccm mmoja anasema magufuli atafanya nini..?! Au ni mzuri kiasi gani..?! Ila naona wengi mmekazana na lowasa tu
 
Ni aibu na fedheha kwa kijana wa kitanzania kupinga mabadiliko wakati yeye mwenyewe hana ajira ya uhakika.wazazi wake,ndugu zake na jamaa zake jembe la mkono likiwa limewang'ang'aniamikononi tangu uhuru wa nchi hii.nasema ni aibu kwa kijana kupinga mabadiliko huku macho yake yakiona watanzania wakilia umasikini miaka hamsini sasa.jamani ni aibu sana.hapa ndo naamini msemo usemao kuwa " ukiona abiria anang'ang'ania kwenye gari bovu ujue kuna mzigo wake"
 
Wee Juliana. Nimeamini hufanani na elimu yako, haijawai tokea ilikuwa ya Mweyekiti kukataliwa au kushushuliwa na Halmashauri yake kwa kutokutenda haki.
Vile vile tupe habari ya Mwai Kibaki na KANU. Jifunze siasa yenye sura ya usomi na siyo ushabiki tuuuu. Wenye chama cha CCM wanasema mambo sivyo yanavyopashwa . for more details pls consult Comred Kinana and Nape as the reinforced opposition is the only force demolishing the party by now.
 
Dada shonza! huyu EL. si ni kapi? fisadi, mwovu, hana sifa ya kuwa rais na hawezi kuwa rais? Sasa mnaweweseka nini???
 
Last edited by a moderator:
endelea kupiga kampeni mkuuu usichoke...


ila usisahahu msemo usemwao ""mti wenye matunda ndiyo unaorushiwa mawe"..
 
Hivi huyu dada kaandika nini hapa? Mara sijui ukristo wa Italy....udini na siasa wapi na wapi??? Ama kweli elimu ni muhimu kwa watanzania
 
Ishu ya Lowassa kuhamia UKAWA na kupewa nafasi ya kugombea Urais ina maudhui mapana mno kuliko suala la kuuongoza upinzani . Fuatilia maneno ya Kina Freeman Mbowe na wengine ....kuna tafsiri za mikakati ya huko mbele mabayo kam unavyosema, itakuja kuwashangaza wengi!

Nakubaliana na dose yako kwa huyu binti. Tatizo sijui kama atakusoma vizuri, lakini wengine tumekuelewa. Safi sana, nimeamini kuwa wewe unafahamu kuwa oil chafu imenunuliwa kuua mchwa
 
Back
Top Bottom