My lovely country will survive

vitus juma

Member
May 20, 2015
98
43
Mwanzoni mwa miaka ya sabini idd Amin dada alianza harakati za kutoa vitisho juu ya taifa langu huru, kwabahati mbaya Nyerere alikaa kimya na hatimaye 1978 dhamira ikatimizwa.

Katika Ulimwengu wa sasa njia pekee ya kuepusha vitisho baina ya nchi na nchi siyo demokrasia bali vitisho mfano ikatokea nchi fulani ikasema kisiwa chote cha Unguja ni chake basi hapo hatuitaji vikao ila mazoezi ya nguvu ya kijeshi kwenye ukanda wa kisiwa ndipo adui atabaini alipo sipo na ataacha kutuchezea lakini tukimkalia kimya ataota mapembe na kuturarua mchana kweupe.

Nimejifunza mengi kupitia Korea Kaskazini. Bila vitisho hii nchi ingeshaingiliwa kijeshi na Marekani kama ilivyotokea Vietnam.
Ningekuwa waziri wa mambo ya nje nisingetoa taarifa iliyoratibiwa na Malawi juu ya kukamatwa kwa majasusi wetu ila ningewasiliana na balozi wa nyumba kumi aliye mpakani na nchi ya Malawi kisha ningemtumia waandishi wa habari akanushe uzushi huo kisha magazeti yaandike "BALOZI WA NYUMBA KUMI TZ ATOA UFAFANUZI WA MAJASUSI KUKAMATWA NCHINI Malawi."

Jibu la mwenye hila ni kumpuuza kwanza. Walitudhalilisha nasi ilibidi tuwadhalilishe kwa kiwango kile kile. Big up to my country and her leaders, we are stronger more than.
 
Back
Top Bottom