My last confession CHADEMA imekosa road map

My last confession CHADEMA imekosa road map

Mtela Mwampamba

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2012
Posts
537
Reaction score
347
Katika kumbukumbu zangu wakati najiunga na Chadema, kwa nguvu za ushawishi na hoja kutoka kwa kaka yangu, mwanasiasa makini na mwenye maono thabiti ya kesho yake na kesho ya watanzania walio wengi, kijana wa kanda ya magharibi mwa nchi hii Dr. Zuberi Zitto Ruyagwa, aliniambia kuwa

"..tunajenga chama hiki ili kiwe chama bora kitakacholeta maendeleo ya kweli kwa watanzania, ndugu zetu wamechoshwa na umasikini uliokithiri na hawana namna nyingine yeyote isipokuwa matumaini yao yapo juu yenu nyie vizazi vyao ili kuwakomboa kutoka katika umasikini wao, na njia pekee ni kwa kushiriki na kupata nguvu ya maamuzi na utawala.."

Akaendelea kwa kusema kuwa;

"..Chama chetu (CHADEMA) bado ni chama kichanga na hakina sura ya chama cha siasa, bado tu-wanaharakati, tunao wajibu kama vijana ndani ya chama hiki kuleta mabadiliko kwanza ndani ya Chama chetu kukifanya kuwa chama bora zaidi kitakacholeta matumaini mapya mioyoni mwa watanzania kisha tupate kuungwa mkono zaidi na tuweze kushinda chaguzi na kufanya maamuzi ya kimamlaka kama chama tawala, lakini hatutofika huko bila kuwa na SHABAHA, pamoja na mpango kazi wa kutimiza na kutekeleza shabaha yetu hiyo, sisi wana-chadema hatuna budi tukubali hali yetu ya ndani ya chama na hata nje, halafu tufanye bidii kuibadili hali hiyo ilingane na shabaha yetu.."

Mazungumzo haya tuliyafanya mwaka 2006, takribani miaka miaka tisa (9) iliyopita, nasikitika nikisema kuwa bado chadema ya leo haina shabaha wala muelekeo wa kutimiza shabaha hiyo, nasema na kwa ushahidi uliyo bayana kuwa chadema ya leo ni more worse kuliko ya miaka tisa iliyopita, wakati huo vijana walikuwa na matumaini at least ya kuleta mageuzi chanya ndani ya Chama chenyewe ili kiwe bora na imara kuweza kukitoa CCM madarakani, lakini leo hata hayo MATUMAINI kwa vijana ndani ya Chama yamekwishaondoka achilia mbali matumaini ya kuingia magogoni.

Lakini haya ndio matokeo ya kuruhusu akili ndogo kuongoza akili kubwa, ni jambo lisilowezekana kuwa form six failure yaani mtu aliyepata ZERO form six ajione mwenye maana na atake kudharau mawazo ya wengine wote na afuate mawazo yake pekee, kisha mawazo hayo yalete mafanikio na yazae matunda..HAIWEZEKANI.

Hakuna namna kuwa MAANDAMANO iwe ndio hoja ya siku zote, iwe ndio mfumo na shabaha ya kupima mafanikio ya Chama, yaani siku niliyokuwa nasikiliza mkutano mkuu wa Chama ilikuwa ni kama vile mtu anatania, anasema moja ya mafanikio ya Chama chao ni kuendesha maandamano, tena maandamano yaliyopoteza maisha ya watanzania, eti hayo ndio mafanikio, kama sio akili ndogo ni nini..?

Wakati mwingine ninapokumbuka dhamira, ari na kujitoa kwa dhati kutoka katika mioyo ya wazalendo wa kweli wa nchi hii katika kujaribu kukijenga chama hicho zilipozimwa na manyang'au na wapiga dili wa mjini waliokimbilia siasa kama njia ya "nitoke vipi" ni jambo linalokera na kutia uchungu.

Baada ya kumbukumbu hiyo fupi ya maisha yangu ndani ya Chadema, niseme kuwa nawatakiwa vijana wa Bavicha maandamano yatakayowaachia uchungu wasiousahau katika maisha yao.,kwani wajinga ndio waliwao...!!!
 
"..tunajenga chama hiki ili kiwe chama bora kitakacholeta maendeleo ya kweli kwa watanzania, ndugu zetu wamechoshwa na umasikini uliokithiri na hawana namna nyingine yeyote isipokuwa matumaini yao yapo juu yenu nyie vizazi vyao ili kuwakomboa kutoka katika umasikini wao, na njia pekee ni kwa kushiriki na kupata nguvu ya maamuzi na utawala.."

Akaendelea kwa kusema kuwa;

"..Chama chetu (CHADEMA) bado ni chama kichanga na hakina sura ya chama cha siasa, bado tu-wanaharakati, tunao wajibu kama vijana ndani ya chama hiki kuleta mabadiliko kwanza ndani ya Chama chetu kukifanya kuwa chama bora zaidi kitakacholeta matumaini mapya mioyoni mwa watanzania kisha tupate kuungwa mkono zaidi na tuweze kushinda chaguzi na kufanya maamuzi ya kimamlaka kama chama tawala, lakini hatutofika huko bila kuwa na SHABAHA, pamoja na mpango kazi wa kutimiza na kutekeleza shabaha yetu hiyo, sisi wana-chadema hatuna budi tukubali hali yetu ya ndani ya chama na hata nje, halafu tufanye bidii kuibadili hali hiyo ilingane na shabaha yetu.."

Mazungumzo haya tuliyafanya mwaka 2006, takribani miaka miaka tisa (9) iliyopita,

HE! hayo ndio ulyoambiwa wewe huko nyuma mkiwa wawili tu ...au yalizungumzwa kwenye mkutano fulani?
 
He! Haki ya Mungu kuna watu na viatu! Yaani ktk mkutano mkuu bora kati ya mikutano mikuu ya vyama Tanzania umechomoka na kamstari kamoja ka kukosoa! Pole nasikia ulipima ubavu wa walinzi wetu ukaambulia kichapo.
 
unaonaje na huyo mwenzio mliyekuwa mnajadiliana naye mkikomaa kuimarisha chama chenu na mkaiacha cdm ijifie kama usemavyo?siamini chama kilichokosa shabaha kinakufanya unashinda kwenye keyboard kila siku
 
Kuna mtu nimemuuliza leo vipi umeomba likizo ofisini ili ujiunge maandamano?...anajiumauma....poor cdm maana mnategemea wanaoandamana wawe wale wapga debe na mama ntilie nyie.muwe jf mkijisifia saa ya ukomboz....manina zenu mtaandamana online...tumewastukia
 
bado mnaipenda cdm lakini ccm iliwapenda zaidi.
 
Kuna mtu nimemuuliza leo vipi umeomba likizo ofisini ili ujiunge maandamano?...anajiumauma....poor cdm maana mnategemea wanaoandamana wawe wale wapga debe na mama ntilie nyie.muwe jf mkijisifia saa ya ukomboz....manina zenu mtaandamana online...tumewastukia
Kiongozi nimekupa like yako.,sasa acha hawa waliojificha maofisini wanatumia muda wa muajiri kufanya ka-ajira kadogo ka mtaa wa Ufipa hapa JF..,kuna huyu jamaa mwingine yupo South Africa anakula raha hotelini kwake..,na ndio maana nikasema wajinga ndio waliwao.
 
Maskini ya Mungu, tokea ujiunge na CCM hakuna mazuri ya ccm uliyowahi kuyaweka humu, zaidi ni kuandika habari za CHADEMA.......... Tunatambua kuwa bado unaipenda CHADEMA, lakini kaka nikuambie tu kuwa CHADEMA haikupendi wewe!! Fanya mambo yenu yale ya Lumumba
 
Unamzungumzia Zitto wa mwaka 2006 alikuwa anaendana na mtazamo wa chama. Ndiyo maana katika hizo unazojifanya kumnukuu hazungumzii mimi. Anazungumzia chama kama chama. Lakini alipopata umaarufu akavimba bichwa kwa kuvimbishwa na hao aliokuwa akiwakosoa. Wewe kwa sasa ni Mwanachama wa CCM jaribu kuwashawishi wenzio kama unao huo ushawishi katika chama chenu ama umufuate huyo unayemsifia umshawishi kwa hoja kwa kuwa anawaza siasa za kesho ajiunge na chama chenu ama wewe ukajiunge kwenye chama chake cha ACT.

Kuhusu maandamano haya huja kwa namna ya short plan programme kijana. Fedha zinaliwa bure kule Dodoma hakuna katiba itakayopatikana unategemea nini? Au kwa kuwa juzi hapa nilikuona Dodoma unafaidika kwa kuwaomba wakusaidie kwa kile wanachopata kutokana na batili hiyo? Hatua ya kwanza ilikuwa kufikisha ujumbe kwa kila aliyeaminika kuwa anaweza kuokoa hizo fedha za walipakodi zinazotafunwa pale Dodoma imeshindikana akiwamo mkuu wa nchi kushindwa. Unataka wananchi wafanyaje kama sio kuandamana?

Nafikiri wananchi wanapaswa wachukue hatua ya juu zaidi kwa kila mbunge anayeshiriki vikao hivi wamwone kama KIBAKA na kutane na HASIRA KALI ili kukomesha kabisa tabia za kihuni pamoja na wapambe wao ukiwamo na wewe. Jitambue bana hata katika ualimu somo la Development Study mbona linafundisha vizuri sana na ulilisoma? Ama akili za mtu siku hizi zina-reflect sura yake? Tumikieni nchi acheni kutumikia watu na huyo nduguyo. Ni hayo tu ndugu yangu Mwampamba.
 
Wewe ni kati ya Watanzania wengi wasiojielewa....

Yaani unaiponda CDM wakati huo upo CCM....hahahaha
 
Kiongozi nimekupa like yako.,sasa acha hawa waliojificha maofisini wanatumia muda wa muajiri kufanya ka-ajira kadogo ka mtaa wa Ufipa hapa JF..,kuna huyu jamaa mwingine yupo South Africa anakula raha hotelini kwake..,na ndio maana nikasema wajinga ndio waliwao.

We gamba tafuta kazi ikusaidi kuliko unafiki.

Jamaa ako analalamika mmempoza na kumtenganisha na kamanda Mbowe.

Anaanza kuweweseka, dhambi ya usaliti inawatesa CHADEMA habari ya mujini.
 
Ulikuwa na hoja nzuri sana ila umefika sehemu umeona kana kwamba MBOWE ni mtu ambaye amefeli masomo yake umefanya ushabiki ambao siyo wa msingi. Sasa wewe kama msomi katika nchi una impact gani kwa ustawi wa jamii? na kama MBOWE ni zero mbona akijukuna kichwani police wanaandamana nchi nzima kumdhibiti huo ni wenda wazimu. Tunataka kuona wewe kama kijana na msomi na hao ambao unawataja akina Zitto na Kitila mnana chakufanya kupiti usomi wenu huo kuleta madiliko ya kimfumo nchini mwetu ili kuondokana na umaskini wa mwili na akiri kupitia elimu yenu, kinyume chake mmekuwa sehemu ya kuleta dhuluma na kurudisha mapambano ya mageuzi nyuma huna cha kutuambia uma wewe acha CHADEMA ishindwe iwe furaha kwako na vibaraka wenzako jionee haibu na uruma kama kijana na mwenye jukumu la kukuza uwazi, uajibikaji na uzalendo. Sasa uko ulipo ni mpiganaji au na wewe ni mwizi na mdhurumaji wa mali za uma jitambu wewe ni nani katika Taifa hili.
 
nimekutana na wanachadema kadhaa hapa udsm wanaponda sana hizi siasa za kiuanaharakati zisizo na ushawishi
 
MANI kuna mfu kafufuka huku. Naamini kabisa mtela na yule demu bado wanaipenda sana sana Chadema. Ukibisha weee mbishi
 
Last edited by a moderator:
Kiongozi nimekupa like yako.,sasa acha hawa waliojificha maofisini wanatumia muda wa muajiri kufanya ka-ajira kadogo ka mtaa wa Ufipa hapa JF..,kuna huyu jamaa mwingine yupo South Africa anakula raha hotelini kwake..,na ndio maana nikasema wajinga ndio waliwao.

Wewe hapo Lumumba Unakula nini Lami?
 
Back
Top Bottom