What happened to my country? Tanzanians have become so unfriendly towards foreigners, especially the Kenyans. Hiyo naithibitisha mimi mwenyewe kwani niliwahi kumchukua rafiki yangu Mkenya kuja Tanzania...maneno aliyokuwa akiambiwa anapojulikana ni Mkenya, sikuamini. Kuanzia kuitwa kila mara kwa kebehi...wee Mkenya, hadi kuulizwa: mnafuata nini huku?!
Kwa kweli huwezi kufahamu hayo mpaka uwe Mkenya au uongozane na Mkenya.
Katika analysis zangu Watanzania wamefikia katika hali hii kwa sababu zifuatazo:
1- Kuathiriwa na wanasiasa- si kificho kuwa wanasiasa wengi wa Tanzania wako dhidi ya Kenya, kiasi hata kama jambo ni dhidi ya manufaa ya nchi. Mfano kujitoa kwenye soko la COMESA, kuwekewa vikwazo wawekezaji wengi wa Kenya kiasi kwamba sasa wana prefer Rwanda, South Sudan na Uganda. Wanasiasa hawa mara kwa mara wanatoa matamshi ya kuhofisha kuwa Wakenya watafanya hivi na vile, lakini kwa kweli wanaficha hofu yao ya kuumbulika, kwa maana nyingine wanaficha their 'inferiority complex'
2- Ufinyo wa upeo wa mawazo
3- Chuki za miaka ya nyuma: ni kweli katika utawala wa Kenyatta na Moi Watanzania walinyanyaswa sana Kenya. Kulikuwa na kufukuzwa-fukuzwa kila mara. Kuna wakati wazazi wa Kitanzania walifukuzwa na kuwaacha watoto wao sshuleni!i
Binafsi nilikuwa nafanya kazi Nairobi na kila siku ya Mungu wafanyakazi wenzangu Wakenya walikuwa wakiniuliza wee m-TZ utaruddi lini Kwenu?
Lakini jamani, wakati umesonga mbele sana, mambo mengi yamebadilika. Na kwa kweli Kenya is a natural partner to Tanzania. Kuna mengi yanayojumuisha Tanganyika na Kenya hata kuliko Tanganyika na Zanzibar.
Tusahau yaliyopita kwani mavi ya kale hayanuki.