Habari za usiku wana jamii forum wenzangu.
Mungu ni mwema kila wakati.Nilimaliza chuo kikuu mnamo mwaka 201..Sintazijaza dash nilizoziacha ili nisigundulike identity yangu.Wakati naanza mwaka wa kwanza chuoni,naikumbuka siku ilikuwa j3 kwenye saa 3.30 asubuhi tuko lecture room ,wakaja walimu,tunawaita lectures kwa vyuoni ,walikuwa 4,wanawake 2 na wanaume 2 darasani kwetu, tulikuwa kama wanafunzi 80 hivi ,foreigners wakiwa kama 12.Wakatusalimu ,wakajitambulisha then wakaketi mbele.Akaamka mwalimu mmoja mwanamke Madame M,akatuhitaji kila mwanafunzi ajitambulishe then aseme kwanni amekwenda kusoma pale tena course ile.
Nakumbuka nilikuwa nimekaa back bencher kwani nilichelewa nikiwa na shosti yangu T.wakaanza kujitambulisha walokaa mbele na sababu zilizofanya wachague chuo kile na especially course ile.Sikuwa nafatilia.Nilimute tu nyuma nikiwaza ya kwangu.
Basi bana ikafika zamu yangu halafu sina hata habari,nikamsikia Madame M akinambia, binti ulovaa top ya kijani tuambie sababu zilizokufanya uje. ..University,shosti yangu T akanambia B simama ujibu,heee nikawaza kumbe imefika zamu yangu?but nikasimama
Ila nikawa naangalia kwenye room usikute nimedandia nafasi ya mtu. Heee kusimama naona watu wote macho kwangu,Madame M akarudia ok mrembo tuambie kwanini umekuja....University?Utaje na shule ulotoka .
Nikajikaza nikajitambulisha,eer my name is The iron Batterfly,am coming from Tabora girls high school.Well I came into ... University because I want to be like Condoleezer rice.Thank you.Nilipomaliza tu si walimu wala wanafunzi kila mtu aliangua kicheko kikali,mwenyewe nilicheka sana.
Kwa enzi hizo condoleezer rice alikuwa ndo Secretary of state wa USA afu tishio America na dunia nzima watu walikuwa wanasema yeye ndo raisi wa UAS,George Bush alikuwa raisi kivuli.
Next time ntawaletea story nilivyograduate nikarudi kitaa hadi kuingia kwenye system.Haikuwa rahisi but I did it.That's y hadi leo najiona condoliza rice wa Africa Ajaye.It's about 7 years since all this happened.
Sent using
Jamii Forums mobile app