Mwongozo mpaka unafika nje kwa njia rahisi

Mwongozo mpaka unafika nje kwa njia rahisi

kyaibumba

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2017
Posts
745
Reaction score
1,080
Mi ntasaidia kutoa conection ya kufika eneo husika
ila please keep in mind mi sitoi kazi ila ni michongo tu ya kufika sehem na kutembea, kama ukiamua kuzamia mwenyewe ni wewe, ila dhamira yangu ni kuja kutembea, kama ni kazi utakuja kutafta mwenyewe,
maelezo nayotoa yako applicable kwa sweden. finland, ukraine, Polland, Croatia, na nyinginezo

mwongozo mpaka unafika nje kwa njia rahisi ni ifuatavyo

1. Kuwa na pass ya kusafiria
2. kuwa na Ticket ya kuja na kurudi
3. Kuwa na suffient fund yaan angalau 100 USD kwa siku utakayokaa nayo ionekane kwa bank statement
4. Kuwa na hotel Reservation ambayo minimum ni 50 USD kwa siku
5. Kuwa na Travel Insurance ambayo inacover mpaka gharama za 30,000 Euros
6. tumia vielelezo hivo kuomba visa
7. Hakikisha una confidence ya kutosha pindi utakapoitwa kwenye interview ya kupewa visa,

hiyo ni njia ya kwanza kama unakuja kwa matembezi yako binafsi bila kutegemea mtu,
hasa kwa wanaotaka kuja UKRAINE ubalozi wa ukraine Tanzania hakuna mpaka Nairobi,

NJIA YA PILI NI KUPATA MTU WA KUKUPA MWALIKO
Huyo atakusaidia kupata yote hayo kwa mgongo wake
maana akikuarika hakuna haja ya kupeleka hotel booking, au bank statements, au Travel Insurance vyote anasimamia yeye isipokuwa utabidi ukubaliane ama ujilipie Ticket ya kwenda na kurudi, na hela ya kuapply visa kwenye Embassy,

NJIA YA TATU NI KUTUMIA AGENTS
Hawa mara nyingi huwa ni tourist groups and companies, wanakupa sponsorship
ila unawalipa wao kiasi fulani ili wakukamilishie taratibu za kukuarika japo si lazima ukifika eneo husika lazima ukae katika nyumba zao, hii inakusaidia kuepuka usumbufu wa ubalozi wanaotaka vigezo vingi kwamba uwe na na dollars 100 per day alafu hotel ambayo uki book kabla ya kufika eneo husika unapata za bei ya juu, kumbe ukishafika mji husika inakuwa rahis kupata hata za bei dnogo hata dolla 8 tu kwa siku, lakin ukisaka kwenye booking.com hiyo hawaioneshi,

KWA WASAKA VIBARUA ni kwamba hakikisha unasafiri ukiwa na angalau visa ya miezi mitatu,
nchi nzuri za kufika ukajipatia kibarua haraka ni Norway, hata Sweden kidogo.
ukifika ukajizubaisha zubaisha unaepelwa kwenye camp na unapewa shule ya ufundi wa jambo lolote , mpaka hapo baadae utakapopata vibali

Meneo magumu kwenda kwa ulaya ni Ufaransa, uingereza, ujerumani maana wameongeza boder controll sana labda uende kama tourist alfu usake job na saa nyingine kupata kazi kwa njia ya kawaida ni ngumu
 
Sawa Mkuu sema Nchi za kutafuta maisha ni China,Singapore, Australia, Vietnam,Cambodia na Hong Kong ingawaje hapo pana bidhaa nyingi za kutuma Africa na pia South Korea...
cambodia kuna nini mkuu
 
Canada ni vipi? Hebu tupatie uzoefu wa huko kwa aliyeko huko, napenda kwenda Canada.
 
Sawa Mkuu sema Nchi za kutafuta maisha ni China,Singapore, Australia, Vietnam,Cambodia na Hong Kong ingawaje hapo pana bidhaa nyingi za kutuma Africa na pia South Korea...
Mkuu China ambayo raia wake wanafanya uchuuzi Kariakoo au China nyingine!
 
cambodia kuna nini mkuu
Mkuu Cambodia kuna viwanda vingi vya saa,Viatu na mpira hizi original bidhaa nyingi za Ulaya zinatoka hapo na Vietnam huko kuna maisha ya kupata pesa tofauti na Nchi mnazozizjua Kenya wana flight yao inatua katika hizo Nchi Mbili wajasiriamali wengi wanachukua bidhaa hapo na Vietnam...
 
Mkuu China ambayo raia wake wanafanya uchuuzi Kariakoo au China nyingine!
Mkuu ukiwa China unakuwa busy kuliko unavyodhania wewe ni kwenda viwandani na kutuma bidhaa unazopata order Tanzania hasa kariakoo vitu vinatumwa kila siku kwa ndege na maji kuliko kwenda kusumbuka huko kwingine huko Asia ndio kuna maisha Mimi naenda kununua bidhaa na kurudi nishakaa sana Hong Kong najua maisha ya vijana wanaojituma huko maisha yanaenda vizuri...
 
Sawa mkuu ni jambo jema kama umezungumza kwa kutumia uzoefu.
 
Back
Top Bottom