Mwongozo mabaraza ya katiba una kasoro kubwa

Mwongozo mabaraza ya katiba una kasoro kubwa

Nagarica

Member
Joined
Feb 21, 2013
Posts
12
Reaction score
4
[TABLE="width: 879"]
[TR]
[TD="bgcolor: #ffffff"][/TD]
[TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][TABLE="width: 599"]
[TR]
[TD]TUME ya Mabadiliko ya Katiba inayoongozwa na Jaji Joseph Warioba imetoa mwongozo kuhusu uundwaji wa mabaraza ya katiba ya ngazi ya serikali za mitaa, ambayo jukumu lake kubwa ni kufanya mapitio na kutoa maoni kuhusu muswada wa katiba mpya utakaoandaliwa na tume hiyo.
Kwa mujibu wa mwongozo huo, mabaraza hayo yataundwa na wajumbe wa aina mbili: Kwanza ni wajumbe wanne kwa kila kata (isipokuwa kwa kata za Jiji la Dar es Salaam ambazo zitatoa wajumbe wanane kwa kila kata) waliochaguliwa na kamati za maendeleo za kata (WDCs), ambao watakuwa wamepatikana kwa kuchaguliwa moja kwa moja na wananchi kutoka ngazi ya vitongoji, vijiji na mitaa.
Aina ya pili ya wajumbe ni madiwani wote wa kila halmashauri ambao wataingia katika mabaraza hayo kwa nyadhifa zao, ambao hatimaye wataungana na wajumbe kutoka kata mbalimbali katika halmashauri zao ili kuunda Baraza la Katiba la Halmashauri ya Wilaya, Halmashauri ya Mji, Halmashauri ya Manispaa na Halmashauri ya Jiji (Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam haimo kwa sababu haina eneo).
Ukifanya uchambuzi makini na mpana, utaona bila shaka yoyote kuwa mwongozo huu una upungufu mkubwa kiasi ambacho ukiachwa utaharibu kabisa uandikwaji katiba mpya.
Kasoro ya kwanza kubwa ni tume kuwapa madiwani upendeleo maalumu usiohitajika wa kuwa wajumbe wa mabaraza ya katiba. Hii siyo haki hata kidogo. Kwanini Tume ya Warioba inawaona madiwani kuwa Watanzania wenye thamani ya pekee na ya juu kuliko wananchi wengine? Kama tumekusudia kuandika katiba mpya ya wananchi, basi mchakato wake usiwe wa kibaguzi, tume haipaswi kuwabagua Watanzania kwa kuwapa baadhi heshima na upendeleo wa pekee na kuwapuuza wengine.
Lazima tume iwaheshimu na kuwapa Watanzania wote fursa ya kushiriki moja kwa moja au kuwakilishwa na watu waliowachagua wenyewe, Watanzania wasichaguliwe watu wa kuwasemea katika mchakato huu muhimu. Sasa hawa madiwani wanamwakilisha nani katika mabaraza ya katiba? Nani kawachagua kufanya kazi hiyo?
Madiwani hawakuchaguliwa kwenda kufanya kazi ya kuandika katiba ya nchi, tumewachagua kusimamia shughuli za maendeleo yetu katika kata zetu, kama wanataka kutuwakilisha pia katika suala hili la katiba, basi wanapaswa kurudi kwetu kutuomba ridhaa kwa kugombea kama watakavyofanya wale wajumbe wengine wa mabaraza ya katiba, siyo kuingizwa tu kinyemela na Tume ya Warioba.
Kingine kinachowafanya madiwani wasikubalike ni ukweli ulio wazi, kwamba wote ni wanachama na viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa, ni wawakilishi wa vyama vya siasa, walichaguliwa baada ya kupendekezwa na kudhaminiwa na vyama vyao, na kwa msingi huo kuna uwezekano mkubwa wakawa watiifu na waaminifu zaidi kwa vyama vyao kuliko wananchi itakapotokea jambo fulani linalopingana na misimamo ya vyama vyao.
Matokeo yake mabaraza ya katiba yatageuka kuwa majukwaa ya siasa. Ni wazi kutakuwa na mivutano na mapambano ya kisiasa miongoni mwa madiwani kwa misingi ya tofauti za itikadi za vyama vyao. Mivutano hiyo haiwezi kuishia kwa madiwani tu, bali itasambaa kwa wajumbe wote wa mabaraza ya katiba ikizingatiwa kuwa hata wale wajumbe wasiokuwa madiwani watapatikana kwa kuchaguliwa na madiwani hao hao, hali ambayo inatoa mwanya wa kuchaguliwa watu kwa misingi ya ukereketwa wa kivyama, kutegemea na chama anachotoka diwani wa kata husika, ambaye ndiye msimamizi mkuu wa uchaguzi katika kata kutokana na wadhifa wake wa Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Kata.
Na kwa kuzingatia ukweli huo, ndipo hoja ya kupinga pendekezo lingine la Tume ya Warioba la kuwapa madiwani mamlaka ya kusimamia chaguzi za wajumbe wa mabaraza hayo wanaowakilisha kata zao linapopata nguvu, pendekezo hili halikubaliki kwa sababu haki haiwezi kutendeka katika chaguzi hizo, ni wazi madiwani na wajumbe wengine wa kamati za maendeleo za kata watachagua watu kwa kuongozwa na itikadi za vyama vyao, watawachagua viongozi na wanachama wa vyama vyao au watu wanaowajua kwa kina kuwa waungaji mkono au wakereketwa wa vyama vyao na kuwaacha watu wengine wenye sifa madhubuti, lakini siyo wanachama au waungaji mkono wa vyama vingine.
Na jambo baya zaidi ni kwamba karibu asilimia 90 ya kamati za maendeleo za kata nchini zinadhibitiwa na wanachama na viongozi wa chama kimoja tu, chama tawala - Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutokana na chama hicho kuwa na madiwani na wenyeviti wa serikali za vijiji na mitaa wengi kuliko chama kingine chochote, maofisa watendaji wa kata na vijiji wote ni wana CCM, ambao ndio wajumbe wa WDCs.
Kwahiyo, kama mwongozo huu wa Tume ya Warioba utaachwa uendelee, maana yake ni kwamba asilimia 90 ya mabaraza ya katiba ya ngazi za serikali za mitaa yataundwa na wanachama na viongozi wa CCM pekee, na kwa maana hiyo tutegemee katiba mpya yenye mwelekeo wa katiba ya sasa kwa sababu ni msimamo wa viongozi wa CCM, kwamba kusiwepo mabadiliko makubwa ya kikatiba. Wanataka mambo mengi yaliyomo kwenye katiba ya sasa na ambayo yanapingwa na Watanzania walio wengi, yaendelee, yakiwemo muundo wa muungano wa Tanganyika na Zanzibar na madaraka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ingefaa Tume ya Warioba ikaandaa mwongozo unaowapa Watanzania haki ya kuchagua wenyewe watu wa kuingia kwenye mabaraza ya katiba badala ya kuwachagulia, na pia iandae kanuni madhubuti na za wazi za kuongoza chaguzi za wajumbe wake, na kuajiri wafanyakazi wake wa muda mfupi ambao watafanya kazi ya kusimamia chaguzi hizo, na hivyo kuwa na watu watakaowajibika moja kwa moja kwa tume hiyo, ikiwemo kuwashtaki ikiwa wataharibu chaguzi hizo kwa ushawishi wa aina yoyote.
Halafu hakuna maelezo ya wazi kutoka kwa tume kuhusu majukumu ya mabaraza ya katiba, kwani mbali ya kuelezwa kijumla jumla tu kwamba yatakaa na kufanya uchambuzi na kisha kutoa maoni kuhusu rasimu ya katiba mpya itakayoandaliwa na Tume ya Warioba, lakini hatuelezwi na wala sheria ya mabadiliko ya katiba haisemi ni kwa vipi maoni hayo ya mabaraza ya katiba yataathiri maoni ya wananchi yaliyomo kwenye rasimu ya katiba.
Hapa hofu yangu ni kwamba, isije ikawa maoni ya mabaraza ya katiba yakayapiku ya wananchi na kuharibu kabisa lengo zima la kuanzisha mchakato huu wa katiba mpya, ambao bila shaka ni kuwapatia Watanzania fursa ya kushiriki kuandika katiba ya nchi yao na si kuwakilishwa na watu wachache.
Tunaitaka tume izingatie ushauri wote unaotolewa na wananchi mmoja mmoja, taasisi au vikundi vya kijamii kuhusu mwongozo wa mabaraza ya katiba, kwani ni kwa njia hiyo ambapo tume itapata mwongozo bora na madhubuti ambao utakuwa na manufaa kwa mustakabali wa uandikaji wa katiba mpya ya nchi yetu, na hivyo kuharakisha maendeleo ya nchi kiuchumi, kijamii, kisiasa na kiutamaduni.

SOURCE: TANZANIA DAIMA
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Kama kawaida yao magamba yanataka kuchakachua na msifikirie hawakuliona hilo haya ni makusudi ili hoja zao za katiba zipite chadema inabidi tuamke ili kupinga upuuzi huu
 
Mwandishi amepaniki.diwani ni mwakilishi wa wananchi wa kata husika ni haki kabisa kuwapo ktk mabaraza.wananchi watawapigia kura wajumbe wengine wanne sa kama hao wote watakuwa wanachama ama wapenzi wa chama flani hilo siyo tatizo la tume na wananchi waliowachagua.watu wengine bana,kulalamika kila kitu,kwanini hamjiamini?
 
Back
Top Bottom