Mwongozo - doctors` strike extension

Seto

JF-Expert Member
Jan 15, 2011
953
53
MWONGOZO

STRIKE EXTENSION : ADDITIONAL 48 HOURS WEEK FULL STRIKE


BAADA YA SERIKALI KUTOONYESHA NIA YA KUTATUA MADAI YA MADAKTARI NA BAADA YA MASHAURIANO NA MAPENDEKEZO YA MADAKTARI WA MIKOA MBALIMBALI, IMEAZIMIWA KUWA KUANZIA LEO TAREHE 31/01/2012, KUONGEZA SIKU TATU ZA KUTOFANYA KAZI HADI KUFIKIA SIKU YA IJUMAA YA TAREHE 02/02/2012. WAKATI HUO TUNAENDELEA KUFUNGUA MILANGO YA MAZUNGUMZO NA SERIKALI KWA KUWA TUNATAMBUA NA KUSIKITIA HALI MBAYA YA WAGONJWA ILIYOSABABISHWA NA MIGOGORO HUU..


JE, TUTARUDI NYUMA KUGEUKA JIWE LA CHUMVI? JE TUTARUDI NYUMA KUENDELEA KUPOKEA CALL ALLOWANCE YA 10,000/= WAKATI HATA STAHIKI YETU ILIYOANDIKWA YA HALF PER DIEM HAIJAFANYIWA KAZI?…


JE , TUTARUDI KULE WANANCHI WANAKOKSA VITANDA NA KULALA CHINI, KUKOSA DAWA HATA KAMA ZINAWEZEKANA KUONA WATOTO, WAKINA MAMA NA WAZEE WAKITEKETEA KWA HUDUMA DUNI ZINAZOSEMWA NI ZA BURE NA HAZIPATIKANI? NI KWELI HATUWAPENDI WATANZANIA? JE NANI ATAKAYEWATETEA HAWA????...


JE TUTARUDI NYUMA BILA KUTIMIZWA HATA NUSU YA KILE TUNACHOSTAHIKI KATIKA POSHO YA MAZINGIRA HATARISHI ( RISK ALLOWANCE )????..


SISI TUNAFAHAMU NI MADAKTARI WANGAPI KATIKA KUHUDUMIA WAGONJWA, WASHATUMIA PEP NA KUPATA SIDE EFFECTS KALI HUKU TUKIWA HATUNA POSHO YOYOTE YA MAZIGIRA HATARISHI??....


HATUWEZI KURUDI NYUMA NA KUADHIBIWA KWA CHUKI KALI KUTOKA KWA WATENDAJI WA WIZARA AKIWEMO YULE MTENDAJI MKUU MWENYE KIBURI ANAYENYANYASA NA KUDHARAU WATUMISHI WA AFYA HUSUSAN YA MADAKTARI…


PALE VITISHO VINAPOJITOKEZA KUTOKA KWA NGAZI ZOZOTE ZA DOLA AMA WAGANGA WAKUU AMBAO NAO WATAFAIDIKA MARADUFU KWA POSHO NA MSHAHARA VIKIONGEZEKA,,,, TUVIKATAE VITISHO HIVYO,,, HATA KAMA INAHITAJIKA KUSAINI MARA SITA KWA SIKU,, SAINI NA USOME MAGAZETI NA MAJARIDA MBALIMBALI YA KUKUIMARISHA.. TUNADHARAULIWA MADATARI KUWA HATUJUI STAHIKI ZETU, SABABU HATUSOMI, TUTUMIE MUDA HUU KUSOMA MAJARIDA NA KUKANUSHA TAARIFA CHACHE ZA UPOTOSHAJI KWENYE FORUMS NA MIJADALA MBALIMBALI…

IFAHAMIKE WAZI TAARIFA NA KAULI ZA MH. WAZIRI MKUU ZIMEIMARISHA MTAZAMO HASI WALIO NAO WATUMISHI WA SEKTA YA AFYA KWA WATENDAJI WA WAZIRA…


IFAHAMIKE KUWA MH. WAZIR HAKUJIBU HOJA ZA MSINGI NA ALITUMIA MUDA MWINGI KUSEMA MSHAHARA HAUTEKELEZEKI… MH. WAZIRI MKUU ALITAKIWA KUTAARIFIWA NA WAZIRI WA UTUMISHI KUWA MSHAHARA TAJWA NI STAHIKI YA MADAKTARI KULINGANA NA UTAFITI ULIOFANYWA MWAKA 1998 NA IDARA YAUTUMISHI KUWA UZITO WA KAZI YA MADAKTARI NI SAWA NA YA SENIOR MANAGERS WA UMMA ( REF CIVIL SERVICE BENCHMARK JOB GRADING EVALUATION FINAL REORT 1998)… SABABU YA KUWA MSHAHARA HUO HAUTEKELEZEKI, OFISI YAKE NA UTUMISHI WALITAKIWA KUTAMKA WATATOA ONGEZEKO LA KASI GANI KAMA ILE ILIOTAJWA HAIWEZEKANI..


KWAKUWA MH. WAZIRI MKUU ALIKUBALI KUPOTOSHWA NA WASAIDIZI WAKE PAMOJA A WATENDAJI WA WIZARA YA AFYA,, MUAFAKA WA SUALA HILI UNAELEKEZWA SASA KWA MH. RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA…

IFAHAMIKE KUWA MGOMO HUU NI MIKOA MBALIMBAL NA OFISI ILITOA TAARIFA ILIYOCHELEWA WAKATI MAAMUZ I YA KIKAO YALISHAPITA KUMUOMBA `WAZIRI MKUU AONANE NASI JUMATATU WASAIDIZI WA OFISI YA WAZIRI MKUU WALIELEZWA KUWA MADAKTRI KUTOKA MIKOA MBALIMBALI WANAWASILI JUMAPILI KUITIKIA WITO WA MH.WAZIRI MKUU… IKUMBUKWE KUWA BARUA YA PM ILIKUWA NI KWA AJILI KUZUNGUMZA NA MADAKTARI WOTE WALIO KWENYE MGOMO NA SIO DAR PEKE YAKE…..


TUNAWASHUKURU MADAKTARI NA WATUMISHI WOTE WA AFYA KWA UMOJA NA MSHIKAMANO WANAOENDELEA KUUONYESHA….



MUNGU IBARIKI TANZANIA..


Imetolewa na:

Kamati kuu ya mpito ya Jumuiya ya madaktari kwa niaba ya madaktari wote , TANZANIA…
 
tunawasapoti, tungeandamana, lakini wakisha tuvunja miguu kina kova tutakosa wa kutufunga p.o.p!!!!! msitufikirie vibaya kuwa tumewaachia peke yenu kazi ya kuikomboa nchi yetu. kama vipi ongezeeni kwenye tamko lenu kuwa mko tayari kuwatibu wahanga wa maandamano yoyote ya kudai haki na akauntabilite ya serikali!!!!
 
Nafahamu wazi zipo technique za kiintelenjia zinatomika ili kuufanya mgomo wa madaktari uonekane ni wa kawaida na hauna madhara makubwa.

Ni wazi saizi kuna mgawanyiko wa madokta kuhusu mgomo huo, wapo wanausupport na wanaona bora liende huku vyombo vya habari vikitakiwa kutoupa kipaumbele kuutangaza sana kwa hiyo kuua indirect.
 
Aluta kontinua,mkirudi nyuma tu mmeumia,kazeni uzi wataalamu wetu hadi kieleweke
 
Back
Top Bottom