Mwonekano bomba Unalipa

doppla2

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2014
Posts
1,391
Reaction score
1,458
Salaam JF

Kuna mambo unaweza kubisha lakini katika Real World yaani mazingira ya kawaida itabidi ukubali tu.

Katika mazingira mengi, mtu mwenye Mwonekano bomba, awe Me au ke kiaina, watu wamekuwa wepesi kuwasaidia kutatua changamoto zao ukilinganisha na wale wenye Mwonekano wa kawaida.

Iwe vyuoni au mashuleni vijana wenye Mwonekano bomba, just naturally ujikuta wamekuwa famous na kiaina kupewa upendeleo fulani hivi, kama vile kupewa uongozi, maksi za upendeleo etc.

Nakumbuka tulupokua chuo tukitaka kujua mwl ataleta maswali yapi kwenye Paper, tulikuwa tunamtumia mdada mwenye umbo zuri kwenda kwa teacher ku prob..., and most of the time tulifanikiwa.

Si vyuoni tu, hata maofisini, usiombe muajiriwe na binti mzuri na mwenye muonekano bomba, unaweza kujichukia, bonus zote atapewa yeye. Safari za kikazi utashangaa yeye ndo Priority.

Nimewahi kuona Mwonekano bomba ulivyomsaidiaga jirani yangu tukiwa hospitali, manesi na madokta walikuwa wanamhudumia kijana yule kwa uangalizi wa karibu sana, ukilinganisha na wagonjwa wengine ndani ya chumba kile.

Hata Kitaa, mtu mwenye Mwonekano bomba lazima awe maarufu, anajulikana na wengi na kila mtu anatamani awe rafiki yake


Jamani ukijariwa Mwonekano bomba ujue Mungu Kakupa mtaji wa maisha bora. Ni jukumu lako kuutumia mtaji huo kwa busara na hekima ili ufanikiwe .

Naomba kuwasilisha wadau,

karibuni TEAM Mwonekano bomba, mtoe uzoefu wenu kwenye hili.
 
Onyesha mwonekano bomba kwa picha
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…