Mwl. Nyerere: Msaafu au hirizi?

Mwl. Nyerere: Msaafu au hirizi?

Liberal

Member
Joined
Jan 29, 2012
Posts
35
Reaction score
5
Unafiki unaoendelea kwa sasa hapa Tanzania unatisha. Tusipokuwa makini tutapoteza historia yetu kama Taifa. Huu ni ujumbe kwa wana-CCM na UKAWA. Karibuni kwa mawazo huru!

===========

Kwa Msomaji

MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE: MSAAFU AU HIRIZI?

Kwanza nichukue fursa hii kukupa Hongera kwa kazi ngumu ya ‘Ujenzi wa Taifa' ingawa unakutana na mambo mengi yanayo athiri ujenzi huo. Nimemesisitiza Ujenzi wa Taifa nikiwa naamini kwamba taifa hili la Tanzania limeeanza kujengwa tarehe 26 April 1964 na ujenzi huo unaendelea hadi leo. Waasisi wa muungano wetu walifanya sehemu yao wakamaliza na kutuachia sisi tuundeleze na kuuimarisha. Tutakubalina sote kuwa ujenzi hauna mwisho. Leo utapaka rangi, kesho utaziba ufa, kesho kutwa utabomoa sehemu fulani ya nyumba napengine nyumba yako ikipitwa na muda basi utaibomoa ili uijenge upya na kuiimarisha zaidi. Mtu yeyote anayeipenda nyumba yake basi hatasita kuikarabati nyumba yake mara kwa mara.
Nyumba hii ya Tanzania ilikuwa na mising yake imara ya umoja, usawa na haki kwa kila mtanzania. Kwa kipindi hicho, karne ya 20 misingi iliweza kuwa imara kulingana na hali ya hewa. Leo kwenye hali ya hewa tofauti, mafuriko kila uchwao, pengine misingi hiyo si imara tena. Je, tuweke viraka au tubomoe tujenge upya? Kipi bora?

Kwa kuona taifa hili la Tanzania linahitaji kujengwa upya, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akaanzisha mchakato wa katiba ikiwa ni sehemu ya kuimarisha Muungano wetu, muungano ulioasisiwa na wazee wetu mwalimu Nyerere na Sheikh Karume. Kwa kuamini kuwa tofauti za hoja ndio nguzo kuu ya ujenzi imara, Bunge la Katiba likapata makundi mawili hasimu: UKAWA na TANZANIA KWANZA. Hongereni wabunge wetu.
Katika makundi hayo wapo wanaomuona Nyerere kama msaafu, mtakatifu na labda niazime neno la kizungu "PERFECT" na kwamba hapaswi kusemwa "Vibaya". Hawa ni TANZANIA KWANZA ambao kwa asilimia kubwa ni CCM. Wapo wanaomuona Nyerere kama mtu tu na si msaafu hivyo kuna sehemu alikosea na lazima maovu yake yawekwe bayana. Hawa ni UKAWA ambao ni CUF, CHADEMA, NCCR-MAGEUZI na MTIKILA. Wajumbe 201 wao wamegawanyika na wengine hawana mwelekeo. Wote hawa wanajenga kwa namna tofauti tofauti.

Ndugu zangu, Mh. Tundu Lissu alipokuwa akitoa ufafanuzi wa mawazo ya wachache katika kamati yao, alitumia maneno mengi na makali yaliyoonyesha u-binadamu wa mwalimu Nyerere. Mimi siwezi kusema kuwa alimkashifu lakini namsifu sana kwa kuwa alisema aliyoyaamini. Tunajenga Taifa, Taifa halijengwi kwa kufichana fichana. Sema bayana watu waamue. Wabunge wa CCM waligeuka mwiba wakawa wakali sana. Kwa wiki mbili mfululizo walikuwa wakionyesha ubaya wa Lissu kwa kumsema vibaya Nyerere. Wapo waliomuita ‘Wakala wa Shetani' na wengi walimuona msaliti wa Taifa, hivyo kupoteza mwelekeo wa hoja za kitaifa.

Nimegundua kuwa Nyerere ‘anapendwa sana.' Kama si unafiki tulionao kwake basi tumshukuru Mungu. Nyerere alikuwa ni mtu anayependa haki na usawa. Je, tunamuenzi? Nyerere si msaafu wala si hirizi kwamba kila alichokisema kilikuwa sawa. Wengi wa wabunge wanaomuona Nyerere kama "PERFECT BEING" ni wanafiki na ndio wanaolibomoa Taifa hili. Naomba nikope uzoefu kutoka Jimbo la Bunda. Mwaka 1995 wakati wa kampeni za uchaguzi, Mh. Steven Masato Wassira alimuita Nyerere "Kapitwa na Wakati" na leo 2014 Mh. Wassira ndio mtetezi mkuu wa Mwl. Nyerere!!! Ni heri mchawi kuliko mnafiki. Naomba nimuulize mbunge wangu Mh. Wassira, ‘Sasa Nyerere hajapitwa na wakati?' au kadri siku zinavyozidi kusonga mbele ndo nyerere anakuwa "Up to date?"

Katika moja ya vikao vya bunge mwaka huu wa fedha 2013/14, Mh. Lukuvi alikaririwa akisema "…tukitajana humu ndani hapatoshi waheshimiwa wabunge…", ni alipokuwa akijibu hoja juu ya majina ya wauza unga yaliyowasilishwa kwa Rais. Maana yake ni kwamba baadhi ya wabunge ni wafanyabiashara wakubwa wa dawa za kulevya! Leo Mh. Lukuvi ni mtetezi mzuri wa Muungano na Mwl. Nyerere? Tunampenda sana Nyerere!! Jamani tumuongope Mungu.

Napenda kusisitiza kuwa, Mwl. Nyerere si msaafu na tusimtumie kama hirizi ya kujikingia. Kama tunataka kulijenga Taifa hili kwa uimara wake, basi tusisite kusema ukweli na ni ukweli tu ndio utakao tuweka huru. Taifa hili ni letu sote, si la CCM, CHADEMA, CUF, NCCR-MAGEUZI n.k. Tabia ya wachache kujiona ndio wenye hati miliki ya Taifa hili haifai hata kidogo. Tume ya Warioba ilifanya kazi yake kwa muda wa miezi 22 kuzunguka Tanzania nzima kukusanya maona yetu. Ni sisi ndio tuliotoa maoni na yakawakilishwa kwa Rais na baadae Bungeni. Inashangaza na kusikitisha sana kuona kazi iliyofanywa na tume haifai…isipokuwa yanafaa maoni ya CCM. Msituchezee akili hata kidogo. Taifa hili lina watu 48 milioni napengine ni milioni 5 tu ndio wanachama wa CCM. Wengine hatuna vyama. Msitusemee tafadhari.

Katika ufungunzi wa wiki ya muungano, Mh. Ommy Mwalimu alikaririwa akisema tutaulinda muungano huu kwa gharama zozote zile. Nini maana ya maneno hayo? Tusitumie nguvu zetu kuulinda muungano. Muungano utajilinda wenyewe kwa misingi dhabiti. Pengine kwa miaka 50 tumetumia nguvu kuulinda ikiwa ni pamoja na kuyaamini ya waasisi bila kuyatafakari na kuyapima. Ni kwa maneno hayo "…kwa gharama zozote zile" ndo hatutaki kusikia chochote "kibaya" juu ya Mwl. Nyerere na Muungano. Nilitangulia kusema hapo juu, maneno ya mwalimu Nyerere si msaafu kwamba usipingwe. Alipokosea patawekwa wazi. Hivyo gharama zozote zisitumike kubomoa muungano kwa kivuli cha kuujenga.

Tanzania ni nchi yenye ‘young population' na hii kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012. Yaani 44% ya watu wake wana miaka chini ya 15. Ni watu hawa ambao hawaijui kabisa historia ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Mwl. Nyerere. Swali langua ni Je, tutaendeleaje kuulinda muungano na kutetea historia za waasisi wetu kwa nguvu zote na gharama yoyote?!

Sera za kipindi cha communism haziwezi kamwe kuwa halali kwa kipindi hiki. Taifa la Tanzania litajengwa imara kwa sera na miiko imara inayoendana na kipindi cha sasa. Kuanza upya si ujinga. Niwasihi sasa watanzania wenzangu wenye kuipenda nchi yetu tupige vita kusemewa na wachache wanaojiita wawakilishi wa wananchi na wakati wakijiwakilisha wenyewe. Naipenda Tanzania inayofuata maadili yaliyowekwa na wazee wetu. Kuwaenzi si kuwatetea bali ni kuwaishi. Napenda muungano ulio imara kwa sera.

Niwatakie mafanikio mema katika kulijenga taifa letu la Tanzania bila woga wa kificho.

Mkama Ildephonce
SAUT-Tabora
+255 754 884 208
 

Attachments

Wamarikani hawajawahi kusema George Washington alikuwa super human,au Lincon alikuwa si mtu wa kawaida .Wamaerikani kwa makusudi kabisa waliamua kuwaenzi viongozi hawa kutukana na misingi waliyoijenga kwa nchi ya marikani.
Wenzetu walichukuwa yale mema yao,na KUYASAHASU
 
Ujinga walionao wengine au tuseme ujinga walionao wao kwa wao ,ni kuwa kumsifu na kutetea mambo ya Nyerere ,au utaonekana hujasema kitu kama hujamtaja Nyerere ,au kama hujamlaumu mtu aliepishana mawazo na Nyerere ,basi wamekuwa na kaujinga haka ndani ya vichwa vyao ,na ni njia moja wanayoona itawapatia sifa na kupigiwa makofi na kuonekana wao ndio wao ,si mnaelewa ile hadithi ya mfalme alieadhiriwa na mtoto mdogo kuwa mfalme hujavaa nguo.

Sasa hawa wagagagigikoko wao humtumia nyerere kama njia ya kukubalika yaani kama ni mtume wao ,na dini yao ni CCM sasa watu wakishafika stage hiyo huwa hawasikii wala hawaoni ila wengine ni pangu pakavu tia mchuzi ,wao humhusisha Nyerere ili na wao wawemo ,yaani wamowamo tu ,tena hawa huwa hatari zaidi wanaweza hata kukufungulia mashataka au kukupiga ,ukimuuliza Nyerere kazaliwa lini hana jibu :loco::iamwithstupid:
 
Watanzania tunakufuru sana, nyerere hakuwa malaika wala mungu! Viongozi wetu sijui lini watatumia vichwa vyao kufikiri!
 
Watanzania tunakufuru sana, nyerere hakuwa malaika wala mungu! Viongozi wetu sijui lini watatumia vichwa vyao kufikiri!

Kama nilivyosema hapo juu, mwisho wa siku watanzania hawa hawa ambao CCM wanajinasibu kuwasemea kwa kumtetea Nyerere wataamua kusema wenyewe. Muda utaamua
 
Back
Top Bottom