Israel ni miongoni mwa nchi ndogo sana duniani lakini imefanikiwa kuwa Taifa kubwa na lenye ushawishi mkubwa sana kakika ulimwengu huu.
Licha ya kuzaliwa upya mwaka 1948 baada ya kuwa utumwani katika kila pembe ya dunia kwa zaidi ya miaka ya 2000.
Wachambuzi wa mambo ya unabii wanasema kutawanywa kwao kulifuatia uovu mkuu waliomfanyia Mungu. Aidha kurejeswa kwao ni kutimia kwa unabii kwamba siku za mwisho MUNGU angeliwarejesha katika nchi yao ya enzi.
Watu hawa walirejea eneo lile lile kulikokuwa makao makuu ya nchi yao kipindi cha utawala wa Mfalme wao Maalufu Daudi yaani Jerusalemu, wakiwa hawajapoteza idedity yao, lugha na utamaduni licha ya kuishi mbalimbali.
Katika kipindi kifupi wameweza kubadili nchi yao kutoka kuwa jangwa lisilomea kitu kuwa nchi inayoongoza duniani kuzalisha na kuuza matunda na mboga mboga, jana Waziri Mkuu Netanyahu akiongea na marafiki wa Israel Jijini Nairobi alisema ng'ombe anayetoa maziwa mengi zaidi kuliko wote duniani anatoka Israel, pia Wayahudi wamefanikiwa kupata maji safi na salama yakiwa hayana wala chembe ya chumvi licha ya kutokuwa na mito na maziwa kama ilivyo kwa Tanzania.
Lakini pia tunafahamu namna Israel ilivyobobea katika masuala ya start-up entrepreneurship, innovation na technology management.
Hivi umewahi kujiuliza flash disc unayoitumia imetoka wapi? Jibu ni kwamba iligunduliwa na Myahudi. Hata Marekani yenyewe licha ya kuonekana kwamba inatoa msaada mkubwa sana wa kijeshi na kiuchumi kwa Israel ukweli ni kwamba wanaoendesha uchumi wa Marekani ni Wayahudi.
Kabla ya kuvunja uhusiano na Israel wayahudi walikuwa wamekwisha anza kutusaidia maeneo mengi sana ikiwemo elimu na afya ambapo walijenga ukumbi imara kabisa wa Nkurumah pale UDSM, pia naambiwa hata Bugando Hospital walijenga wao.
Wayahudi walianza pia kuwekeza kwenye kilimo. Kitendo chetu cha kuwakana wayahudi kimetuletea hasara kubwa sana. Kujifanya tunawahurumia Wapalestina umekuwa ni mzigo usiobebeka tena maana hawana msaada wowote.
Maandiko yako wazi kabisa. Nchi ile ni ya wayahudi, Mwarabu akitaka kuishi ataishi kwa amani lakini si kudai haki ya urithi wa nchi ile.
Tuwakaribishe watu hawa watusaidie katika kilimo tuachane na Waziri wa Kilimo kila siku yeye ku-deal na migogoro ya wakulima wadogo wadogo tunahitaji uwekezaji mkubwa wa kilimo. Tutumie eneo dogo lakini tuwe na output kubwa.
Katika eneo la IT wanaweza kutusaidia sana. Hata juhudi za Mhe. Rais za kutafuta msaada katika ukusanyaji wa mapato kitaalam zaidi zinaweza kupata msaada kutoka kwa hawa jamaa.
Namshauri Mhe. Rais atembelee Israel anaweza kujifunza mambo mengi sana. Nawasilisha.