Mkweliii
Member
- Apr 15, 2025
- 14
- 5
Kada wa Chama Cha Mapinduzi, Mwl. Mbelwa Petro ameteuliwa na Chama hicho kuongoza timu ya kampeni ya kusaka kura kwa wagombea wa CCM katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29 mwaka huu wa 2025. Akizungumza baada ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo, Mwl. Mbelwa Petro alisema "ninakishukuru Chama chetu, Chama Cha Mapinduzi kwa kunifikiria na kunipa jukumu hili muhimu. Nina hamu ya kuleta uwezo na ujuzi wangu kwenye nafasi hii mpya".
Kwa nafasi hiyo, kada huyo wa CCM atashirikiana na wanachama wengine wa chama hicho kutafuta kura kwa mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama hicho, Dkt. Samia Suluhu Hassan, mgombea wa kiti cha ubunge jimbo la Biharamulo magharibi, Mhandisi Ezra John Chiwelesa na madiwani 17 wa kata zinazounda jimbo hilo la uchaguzi.
Mwl. Mbelwa Petro amehaidi kushirikiana na wanachama na makundi yote rafiki ya CCM kufanya alichokiita "kampeni za kisayansi" ili kupata ushindi wa kihistoria. Akieleza mpango huo, Mbelwa Petro alisema kupitia kampeni za kistaarabu atakazoziongoza katika kipindi hiki, atahakikisha hamasa ya watu kwenda kupiga kura inaongezeka na elimu kwa mpiga kura inaelezwa bayana katika majukwaa ili kupunguza idadi ya kura zinazoharibika katika mchakato wa upigaji kura.
"Kwa kushirikiana na timu yetu nzima ya kampeni, viongozi na wanachama wenzetu kuanzia kwenye nyumba 10, mashinani mpaka kwenye jimbo ni kufanya kampeni za kisayansi na kuhakikisha idadi ya watakaopiga kura inafikia angalau 65% ambao ni sawa na 148,273 kwa idadi ya wapiga kura waliojiandikisha kupiga kura mpaka 2025 wanaokadiriwa kufika 228,113". Alisema.
Aliongeza kwa kusema "kupitia uelimishaji wa majukwaani na kwa mtu mmoja mmoja tutahakikisha kura zinazoharibika kwa kukosea taratibu za upigaji kura zinapungua na kuwa chini ya: 0.5% sawa na kura chini ya 740 zote zitakazopigwa".
Mbelwa Petro alisema kwa mara ya kwanza katika historia ya uchaguzi anahitaji kuona kura za mgombea wa urais kupitia Chama Cha Mapinduzi zinakuwa ni nyingi kupita wakati wowote katika historia ya uchaguzi. "Malengo yetu pia kati ya wagombea wote 17 wa urais, basi kura za Rais wetu mpendwa, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan zifike 148,200 sawa na 99.9% ya kura zote 148,273. Kura za wagombea 16 wengine wa nafasi ya urais ziwe kura 73 tu sawa na 0.049% ili ukikaribisha kwenye wango viwili vya desimali wapate 0.05% ya kura zote 148,273.
Na hatufanyi hivi kwa sababu labda tuna roho mbaya la hasha! tunafanya hivi kumpa heshima yake Rais wetu mpendwa, Dkt. Samia Suluhu Hassan na serikali yake kwa kutupatia miradi iliyokadiriwa kuwa zaidi ya bilioni 95 hapa katika Jimbo letu la Biharamulo".
Kwa upande wa kura za mgombea wa kiti cha ubunge, Mbelwa Petro alisema "tunatizamia kupata kura 148,000 za NDIYO kwa Mhandisi Ezra John Chiwelewa sawa na 99.82% ya kura zote 148,273 zinazotizamiwa kupigwa. Hii litakuwa ni ongezeko la 365% za kura kwa Mbunge wetu Mhandisi Ezra John Chiwelesa ukilingaisha na kura za uchaguzi mkuu wa 2020. Hatufanyi hivi kumkomoa mtu, tunafanya hivi kama pongezi zetu kwa Mheshimiwa Mbunge wetu, Ezra John Chiwelewa kwa utekelezaji mjarabu wa ilani ya uchaguzi ya 2020-25, aliongeza.