Mwizi anapojenga wivu kwa mke wa mtu……….

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,806
15,354
Zamani wakati nilipokuwa mtoto, ilikuwa ni aibu kubwa mtu kuambiwa amefumaniwa. Kama ni vijijini, wapiga ngoma wa kijijjini wakiongozwa na Manju wao walitunga nyimbo kuzungumzia jambo hilo. Kufanya mapenzi kiholela, iwe mjini au vijijini, lilikuwa ni jambo linalotazamwa kwa jicho la bezo.

Leo hii, kujamiiana kunachukuliwa kama moja ya burudani muhimu sana. Kwa hiyo watu kutoka nje ya ndoa zao, ni jambo ambalo linafanyika kama kwamba, ni sifa muhimu sana. Siku hizi mtu anaweza kufanya jambo hilo na yeyote, mradi tu amepata nafasi ndogo ya kujificha.
Labda hata wewe unaweza kushangazwa na jambo hili, kuna wakati mwanaume anaanza uhusiano wa kimwili na mke wa mtu, huku akijua hilo ni kosa. Lakini baadae mwanaume huyo huanza wivu kwa mwanaume halali wa mke husika…………. Ajabu eh!.............. Je unadhani huyu ‘mwizi’ ni kichaa? Hapana, inakuwa hivyo na ndio maana watu hufumaniwa!
Wataalamu wa saikolojia wanasema, kwa mfano, mtu anapofikia mshindo wakati wa tendo, anakuwa ameingia kwenye ukaribu wa kiwango cha juu na mtu aliyeshiriki naye tendo. Baada ya tendo hilo choyo huanza, na hapo muhusika anaanza kuingia kwenye hofu ya kuachwa na hivyo anajikuta akitaka kudhibiti mienendo ya huyo mke wa mtu, jambo ambalo linaweza kupelekea kufumaniwa kwa urahisi………………………… Kwa hiyo ukiingia kwenye uhusiano na wake za watu, basi ujue ipo siku utafumaniwa tu……………………………
 
Husninyo

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
23,735
9,119
Duh! Tatizo watu wanayajaribu mapenzi halafu wanataka wayape mipaka (limits). Mapenzi ni hisia na kadri siku zinavyokwenda hisia huzidi kujijenga(kama utaruhusu). Huwezi kuzuia vile unafeel. Kama unadate mme/mke wa mtu huku ukiamini unajipa limit ya mahusiano yenu ujue upo wrong na kama ukiweza kujipa mipaka ni lazima utakuwa unaumizwa na hilo penzi la wizi na mwisho wa siku lazma ufumaniwe.
 
Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,806
15,354
Duh! Tatizo watu wanayajaribu mapenzi halafu wanataka wayape mipaka (limits). Mapenzi ni hisia na kadri siku zinavyokwenda hisia huzidi kujijenga(kama utaruhusu). Huwezi kuzuia vile unafeel. Kama unadate mme/mke wa mtu huku ukiamini unajipa limit ya mahusiano yenu ujue upo wrong na kama ukiweza kujipa mipaka ni lazima utakuwa unaumizwa na hilo penzi la wizi na mwisho wa siku lazma ufumaniwe.

Kumbe iko kote kote.............. nilisahau ku-balance gender..................
 
Nzowa Godat

JF-Expert Member
Jun 15, 2011
2,760
795
Jambo hili limetokea dhahili kabisa kwenye kanisa la moravian Igamba Mbozi ambako makahaba watu wazima wake za watu wameunda kikundi cha 'vijana' B. Kwa hakika hicho ni kikundi cha UZINZI na UFUSKA. Maana wamejipanga in pairs wanajifanya kukesha misibani na kwenye mazoezi ya kwaya, lakini ukweli ni wazinzi.
Petro anathibitisha kwamba
kukawia kurudi kwa Yesu ni
kwa sababu ya upendo na
rehema na huruma Zake –
anataka kutoa nafasi zaidi watu
watubu. Lakini anasema pia
kwamba hakuna mashaka
yoyote – Yesu atarudi. Na
atakaporudi, atakuja akiwa na
ghadhabu kubwa.
 
The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
45,193
95,668
mimi hujiuliza hili swali..
watu wanaiba mwisho wanaamua kuhalalisha.wanaoana baada ya kuachana na wenzi wao..

sasa kuaminiana kuna kuwa vipi hapo??????
 
Nzowa Godat

JF-Expert Member
Jun 15, 2011
2,760
795
Petro anathibitisha kwamba
kukawia kurudi kwa Yesu ni
kwa sababu ya upendo na
rehema na huruma Zake –
anataka kutoa nafasi zaidi watu
watubu. Lakini anasema pia
kwamba hakuna mashaka
yoyote – Yesu atarudi. Na
atakaporudi, atakuja akiwa na
ghadhabu kubwa.
 
Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,806
15,354
mimi hujiuliza hili swali..
watu wanaiba mwisho wanaamua kuhalalisha.wanaoana baada ya kuachana na wenzi wao..

sasa kuaminiana kuna kuwa vipi hapo??????

Swali lako linahitaji Thread inayojitegemea...........lakini kwa kifupi ni kwamba, mara nyingi watu wanapokutana kimwili, bila kujali kama wanafanya tendo hilo kwa kuiba au kudokoa, huwa wanagusika kihisia, na hapo hujiweka kwenye nafasi ya kuingia ndani kabisa kwenye uhusiano, kiasi kwamba, hawawezi kumudu kujificha............... kwa kawaida, baada ya kukutana kimwili, wivu huanza, kuchungana huanza, mamlaka juu ya wengine huanza na hisia za kwamba huyu anapaswa kuwa wangu tu huanza................ na hapo ndipo mambo huharibika. lakini unadhani wanaume au wanawake wanaokimbia nyumba zao na kwenda kwa mahawara wanapata chochote cha maana huko? ukweli ni kwamba hakuna cha maana chochote wanachokipata zaidi ya majuto ya baadae...............
 
BPM

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
2,760
572
mapenzi hayana majaribio , ukishaanza mahusiano nje ni rahisi sana kugundulika iwapo mwenza wako atakuwa angali na mapenzi na hisia kwako lakini kama hana hisia hata ukitoka hata weza kufeel umuhimu wako hivyo mnapotezeana
 
Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,806
15,354
mapenzi hayana majaribio , ukishaanza mahusiano nje ni rahisi sana kugundulika iwapo mwenza wako atakuwa angali na mapenzi na hisia kwako lakini kama hana hisia hata ukitoka hata weza kufeel umuhimu wako hivyo mnapotezeana

Yeah..........! nakubaliana na wewe, lakini kama mke huyo wa mtu anatoka nje kwa sababu ya fedha........wengine huita kuchuna buzi........... Inaelezwa kwamba mara nyingi katika kutoka nje ya ndoa wake za watu hujitahidi sana kuwa makini, hutokea kufumaniwa kama alimpenda kwa dhati huyo aliyetoka naye. kama kutoka kwake kulivutwa na fedha, basi penzi hilo linakuwa halijateka hisia zake, na hapo kuhemkwa kunakuwa hakupo.............................
 
BPM

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
2,760
572
Swali lako linahitaji Thread inayojitegemea...........lakini kwa kifupi ni kwamba, mara nyingi watu wanapokutana kimwili, bila kujali kama wanafanya tendo hilo kwa kuiba au kudokoa, huwa wanagusika kihisia, na hapo hujiweka kwenye nafasi ya kuingia ndani kabisa kwenye uhusiano, kiasi kwamba, hawawezi kumudu kujificha............... kwa kawaida, baada ya kukutana kimwili, wivu huanza, kuchungana huanza, mamlaka juu ya wengine huanza na hisia za kwamba huyu anapaswa kuwa wangu tu huanza................ na hapo ndipo mambo huharibika. lakini unadhani wanaume au wanawake wanaokimbia nyumba zao na kwenda kwa mahawara wanapata chochote cha maana huko? ukweli ni kwamba hakuna cha maana chochote wanachokipata zaidi ya majuto ya baadae...............

wengi watokao nje hupenda sana kuelezea CV za wenzi wao na wale wa nje wanatumia udhaifu wa watokaji kuwahadaa na wao wanaona kule ndo muhimu sana
 
BPM

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
2,760
572
Yeah..........! nakubaliana na wewe, lakini kama mke huyo wa mtu anatoka nje kwa sababu ya fedha........wengine huita kuchuna buzi........... Inaelezwa kwamba mara nyingi katika kutoka nje ya ndoa wake za watu hujitahidi sana kuwa makini, hutokea kufumaniwa kama alimpenda kwa dhati huyo aliyetoka naye. kama kutoka kwake kulivutwa na fedha, basi penzi hilo linakuwa halijateka hisia zake, na hapo kuhemkwa kunakuwa hakupo.............................

mkuu hata kama ametoka kwa ajili ya kufuata pesa bado itabidi aonyeshe juhudi ili aweze kupata zaidi na ndipo huyo mtoa pesa atakuwa namcontrol anavyotaka na kumfanya mwanamke amdharau mmewe kwa vile kule anaona ana ziada apatayo
 
Roulette

JF-Expert Member
Dec 15, 2010
5,581
5,338
Kweli siku hizi values zinaonekana kama ujinga. ukipata nafasi ya kuiba na usiibe watu wanakucheka eti unajifanya mnoko. ukishangaa rafiki yako anasex "for pleasure" kwa one night stand anakuona mshamba sababu ulimkataza...
Ila hayo mengine ya kuoneana wivu kwa make/waume wa watu sitasema sana sababu kuna wakati mapenzi yakiwa ya dhati huyo mwizi anaishia kugeuka mwenye mali... na sio lazima kufumaniwa kama mliamua kujitambulisha wenyewe.
 
Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,806
15,354
wengi watokao nje hupenda sana kuelezea CV za wenzi wao na wale wa nje wanatumia udhaifu wa watokaji kuwahadaa na wao wanaona kule ndo muhimu sana

Yuko rafiki yangu alikuwa kijogoo sana wa wake za watu......... nilifanya kazi sana kumrekebisha, maana la sivyo sidhani kama angekuwa hai leo hii. Aliwahi kunisimulia kwamba, siku moja alikuwa na mke wa mtu, ambaye alimwambia kuwa ameamua kutoka nje ya ndoa ili kumkomoa mumewe, baada ya kumfumania mara mbili na ma-house girl...............(Mara nyingi wanawake hutoka nje ili kulipa kisasi)
Siku moja baada ya kufanya mapenzi, walianza kupiga stori pale kitandani............. yule jamaa yangu akamuuliza............. "hivi wewe na mumeo huwa mnafanya tendo la ndoa mpaka kufikia mshindo kama inavyotokea ukiwa na mimi?"..............Swali la kijinga eh!
Alichofanya yule mwanamke ni kunyanyuka na kuvaa na kisha kuondoka zake............... baadae jamaa alipokea ujumbe kwenye simu yake ya mkononi kwa namba asiyoifahamu ikisema............. "mie kutembea na wewe sio kwamba simpendi mume wangu, ukweli ni kwamba nampenda sana, kwa hiyo usijione mshindi, nilifanya hivyo kwa ajili ya kupunguza maumivu ya kihisia, na kuanzia leo tusijuane mshamba wewe........."
Ilimchukua muda kidogo, jamaa yangu kujua ule ujumbe umetoka kwa nani...........
 
2 Reactions
Reply
Top Bottom