Mwizi alienasa toka jana usiku duka la Simu na TV anasuliwa

Ashura9

JF-Expert Member
Oct 21, 2012
740
485
Mwizi alienasa toka jana usiku duka la Simu na TV anasuliwa

Huyo mwizi alifumua bati aingie duka la cm na TV akanata toka Jana ucku hiyo miguu kwenye TV imenasa wamevuta Askari wanne haiachii wakimvutia kwa juu ya bati alikoingilia analalamika anadai msinivute


kwa juu mnivutie kwa ndani kwa juu mnavyonivuta kuna kitu dukani nacho kinanivuta ntafia hapa hapa baada ya police kushindwa kumchomoa wakamuomba mwenye duka tunaomba ukamtoe ndo akavutwa na mwenye duka akafanikiwa kutoka. Huu utaalam unapatikana Kasulu kwa sasa.

 
Aise Kuna umuhimu wa kugaramia utaalamu huo, hata Kama Kasulu mbali, huku mtaani wezi wa madirishani Na kupulizia dawa ya usingizi wamezidi. Hii itakua komesha yao.
 
Only in Tanzania,kwa hiyo technology tuko vizuri sana na ile ya mitego ya kuwanasa wanaokula wake za watu,kwa kweli tunafanya vizuri sana kwenye hiyo fani.
 
Mbona kwenye video kwa juu anaonekana mtu akikata vyuma (grille) kwa msumeno na mara baada ya kukata hiyo grille anaeonekana kumvuta na kumshusha chini huyo mtuhumiwa wa wizi ni askari? Au askari ndiye mwenye duka?
 
Tusishangae hivi karibuni mtu akafungua thread hapa JF kuwa hiyo technology ya kukamata wezi yeye anayo! Na anaweka na namba yake ya simu hapa kabisa!! Kila mtu mganga siku hizi,awamu ya 5 imebana kila kona watu wanatafuta pakutokea! teh! teh!
 
Mbona kwenye video kwa juu anaonekana mtu akikata vyuma (grille) kwa msumeno na mara baada ya kukata hiyo grille anaeonekana kumvuta na kumshusha chini huyo mtuhumiwa wa wizi ni askari? Au askari ndiye mwenye duka?
Mtoa post ulichoandika na video havifanani kabisa tuamini video au maneno yako?
 
Mtoa post ulichoandika na video havifanani kabisa tuamini video au maneno yako?
Kwani mkuu ukiangalia kwenye video huoni kwa juu kuna mtu anakata grille kwa msumeno? Na anaemvuta chini mtuhumiwa siyo polisi? Kwa maana nyingine sijaona mtu mwingine tofauti ambaye anamshusha chini zaidi ya huyo askari. Na ndiyo sababu nikasema labda askari ndiye mmiliki wa duka au kama kweli mmiliki wa duka alimvuta hii haionekani kwenye video. Kulingana na maelezo ya awali iliandikwa mmiliki wa duka ndiye aliyemvuta. Lakini kwenye video haionyeshi hivyo.

Na usishangae katika tukio hili kunaweza kuwa na collusion inayowahusisha mwenye duka, mwizi na mganga ili kuwapata wafanyabiashara au watu wengine wanaohitaji ulinzi wa aina hiyo kwa kulipa fedha nyingi.
 
Aah... Kama Propaganda flani ivi...
You might be right. Kumbuka matukio ya misukule, wachawi kudai kuruka kwa ungo usiku na kuangukia kwenye mapaa au compound za watu na makanisani, wapenzi kudaiwa kugandiana wakiwa kwenye tendo la ndoa (kumbuka tukio la kule Temeke). Baadae ubainika ni matukio yaliyopangwa.

Sikatai kuhusu tukio hilo kutokea lakini pia kuna uwezekano wa tukio lenyewe kupangwa ili baadae wahusika waweze kunufaika kutoka kwa watu watakaoamini uwepo wa ulinzi wa aina hiyo na kuusaka kwa fedha nyingi kutoka kwa mganga.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom