Singo Batan
JF-Expert Member
- Apr 24, 2020
- 304
- 213
Wana jamvi nina jambo ningependa kufahamishwa kuhusu ushiriki wa vijana katika masuala ya siasa na hususan Chaguzi mbalimbali.
Takwimu za kidunia zinaonesha muitikio wa ushiriki katika uchaguzi wa viongozi wa nafasi mbalimbali hasa wanaounda mihimili ya kitaifa (state organs) ni 60% pekee.
Anguko kubwa la muitikio wa upigaji kura na ushiriki katika mchakato wa uchaguzi limeshuhudiwa zaidi bara la Ulaya katika kipindi cha miaka 30 mfululizo tangu miaka ya 1990 na vijana ndio waathirika wakubwa.
Hapa kwetu TANZANIA bado hakuna takwimu zilizothibitishwa za ushiriki wa vijana, lakini tafiti mbali mbali zinaonesha ni vijana chini ya 30% ndio wanashiriki katika uchaguzi wa viongozi wakiwemo Rais, Wabunge, Madiwani na Serikali za Mitaa.
Kwa mujibu wa ripoti za NEC vijana waliojiandikisha kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa 2020 walikuwa takribani 53% ya wapigakura wote milioni 29. Wanaobaki 47% ni watu wa makamo na wazee.
Na tafiti zinafafanua kwamba Muitikio wa upigaji kura kwa wazee umekuwa ni mkubw kuliko vijana.
Swali langu hapa ni
KWANINI / MAMBO GANI YANASABABISHA MUITIKIO WA VIJANA KUWA MDOGO KATIKA MCHAKATO WA UCHAGUZI?
Note: Tatizo hili ni la kidunia sio Tz pekee
KARIBUNI WATAALAMU