Mwisho wa kulipia daraja la Nyerere (Kigamboni)

2kimo

JF-Expert Member
Jan 23, 2014
2,029
2,072
Wadau kuna mambo lazima tuyajadili!!
Nani anayejua ni lini NSSF wataacha kuchaji kwa ajili ya kupita darajani? Kwa malipo ya sasa wamekadiria kwa rate hii ya sasa, itawachukua miaka mingapi kurejesha pesa zao! Na baada ya pesa zao kurejea ndio utakuwa mwisho wa tozo?

Na tunalipia just kwa kuwa pesa za mkopo au kuna sababu nyingine?
Kuna baadhi ya watu wanahoji mbona mwendo kasi watu hawalipii njia, au pesa za nje ndio wanagharamia hadi walio kijijini Ila mkopo wa ndani ndio wakazi tu?

Vipi kuhusu UDOM? Nao pia ni mkopo wa taasisi za mifuko ya hifadhi za jamii, kwanini wanaosoma nao wasigharamie mkopo?

Kwanini Kigamboni tu?

Kwanini sio mto Rufiji au Malagarasi etc?

Kwanini gharama ziko juu?
 
Sio kazi ya NSSF kujenga madaraja. Lakini kwakuwa Serikali haiwezi kufanya mambo yake yote yenyewe, taasisi zinahitajika kuisaidia serikali. Unaona kwenye elimu, afya n.k
NSSF imeitikia with kufanya hivyo kwa gharama za wanachama wake, lazima uwarudishie wanachama hela zao na upate faida pia. Miradi ya mikopo iliyofanya serikali itarudishwa/itarejeshewa fedha zake kwa KODI YAKO Mtanzania.
 
Washington bridge ina miaka zaidi ya 75 na mpaka leo watu wanalipia. Sasa wewe unalalama wakati hata miezi mitatu haijafika, unaulizia lini itakuwa mwisho wa kulipia.
Bongo bwana mnatafuta vya kulinganisha na Mambo ya Duniani huko,
 
Washington bridge ina miaka zaidi ya 75 na mpaka leo watu wanalipia. Sasa wewe unalalama wakati hata miezi mitatu haijafika, unaulizia lini itakuwa mwisho wa kulipia.
Siyo kulalama ni juu ya serikali kutujusha kwamba huo mkopo unaisha lini na tozo zinazotozwa ni za kudumu au ni kwa ajili ya kufidia gharama zao na baadaye daraja litakabidhiwa serikalini
 
Back
Top Bottom