Mwisho wa bima ya gari

Mwisho wa bima ya gari

BRO SANTANA

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2015
Posts
1,845
Reaction score
2,249
Wakuu mpo njema!!?
Naomba kujua bima ya gari ikiisha muda wake unapewa muda gani kisheria ili ukate bima mpya kabla traffic hawajaanza kusumbua?
Ahsanteni sana.
 
Mimi ninavyojua bima haisubiriwi wala kuwa na mda wake bali ikiisha tu lazima uunganishe
Labda sio bima ninayoijua mimi yaani Insurance
 
Siku moja kabla ya kuisha unatakiwa uweke nyingine na hii ni kwa faida yako mmiliki na hasa kama gari ni ya Abiria.
 
Namaanisha kwa traffic kukusumbua barabarani
Bima haina Grace periodi labda kama gari umeipaki nyumbani.

Hii sheria imewekwa kwa faida ya mmiliki punde ikitokea ajali.

Kwa mfano ukiendesha gari bila bima then kwa bahati Mbaya ukamgonga Mchezaji wa mpira wa miguu ukamvunja mguu kabisa.
Ujue hapo atakufungulia kesi ya madai ya kumlipa mamilioni ya pesa mpaka atakapozeeka mana maisha yake anategemea mpira ili apate kipato cha kuendesha familia yake.
Hapo kama huna bima utalazimika kulipa mwenyewe.
Kama huna kesi Mali zitauzwa ukishindwa kesi mahakamani.

Ndio maana vyombo vya moto muda wote vinatakiwa kuwa na bima iliyo hai vinapokua barabarani.
 
Ikisha we tembelea tu Gari lako
Hakuna noma!

Ova
 
Back
Top Bottom