Mwinyi ataka Mahakama itoe haki bila kuingiliwa

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
125,745
239,396
Rais Mstaafu , Ali Hassan Mwinyi ameitaka Mahakama kutoa haki kwa wakati bila kuingiliwa na chombo chochote , au mtu yeyote ili kuifanya iweze kuaminiwa na wananchi .

Mzee Ruksa alitoa rai hiyo wakati akizindua maadhimisho ya wiki ya sheria na utoaji elimu ya sheria , katika viwanja vya mnazi mmoja , Jijini D' Salaam .

Chanzo - Mwananchi

Mytake - Lisemwalo lipo .

=======

Mwinyi ataka Mahakama itoe haki kwa wakati
mzeemwinyi_1.jpg

Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi

Kwa ufupi
Mzee Mwinyi maarufu Mzee Ruksa, alitoa rai hiyo jana wakati akizindua maadhimisho ya Wiki ya Sheria na Utoaji Elimu ya Sheria, katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.

By James Magai na Sada Amir, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz
Dar/Mwanza. Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi ameitaka Mahakama kutoa haki kwa wakati bila kuingiliwa na chombo chochote, au mtu yeyote ili kuifanya iweze kuaminiwa na wananchi.

Mzee Mwinyi maarufu Mzee Ruksa, alitoa rai hiyo jana wakati akizindua maadhimisho ya Wiki ya Sheria na Utoaji Elimu ya Sheria, katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.

Maadhimisho hayo yenye kaulimbiu ya “Umuhimu wa utoaji haki kwa wakati, kuwezesha ukuaji wa uchumi”, yatafikia kilele Februari 2 yakiashiria kuanza mwaka wa Mahakama.

Katika hotuba yake, alisema ili Mahakama itende haki kwa wakati, lazima ishirikiane na wadau wote ili kuleta ufanisi.

Alisema huo ndiyo msingi wa amani, na utulivu na ndiyo msingi wa maendeleo.

Awali, Kaimu Jaji Mkuu, Profesa Ibrahimu Juma alisema sheria ni kitu muhimu katika maisha ya jamii na hakuna nyenzo nyingine yoyote inayowezesha mtu kuishi katika jamii zaidi ya sheria.
 
Rais Mstaafu , Ali Hassan Mwinyi ameitaka Mahakama kutoa haki kwa wakati bila kuingiliwa na chombo chochote , au mtu yeyote ili kuifanya iweze kuaminiwa na wananchi .

Mzee Ruksa alitoa rai hiyo wakati akizindua maadhimisho ya wiki ya sheria na utoaji elimu ya sheria , katika viwanja vya mnazi mmoja , Jijini D' Salaam .

Chanzo - Mwananchi

Mytake - Lisemwalo lipo .
Independence and transparency of the judiciary vanished with the demise of Justice Mwalusanya, Lugakingira and Katiti to mention but a few!
 
Bahati mbaya sasa muhimili wa sheria umeungana na mhimili wa Bunge na kuwa ni chini ya serikali.. Unaongozwa na kutenda kwa kuongozwa na Serikali.. Very sad kwa kweli..
 
Anajikosha tu tusione kama hawasikitiki. Waliyemchagua wenyewe kawarudi?? Nasema; maneno hayavunji mfupa. Aendelee kidogo kwa kusema ni nini aliona hata akayatamka maneno hayo ndo tutajua kaumia.
 
Rais Mstaafu , Ali Hassan Mwinyi ameitaka Mahakama kutoa haki kwa wakati bila kuingiliwa na chombo chochote , au mtu yeyote ili kuifanya iweze kuaminiwa na wananchi .

Mzee Ruksa alitoa rai hiyo wakati akizindua maadhimisho ya wiki ya sheria na utoaji elimu ya sheria , katika viwanja vya mnazi mmoja , Jijini D' Salaam .

Chanzo - Mwananchi

Mytake - Lisemwalo lipo .
Huyu mzee anaongea hayo lakini kesho ataenda Ikulu kukanusha kuwa kanukuliwa vibaya!
 
Umri ukienda sana nadhani pia kumbu kumbu zinafutika juzi unasema ndani ya mwaka mmoja tu mheshimiwa kafanya kazi ambayo haikuwahi kufanywa na marais wote waliopita sasa iweje tena Mahakama haitoia haki au hizi mahakama hazikubahatika kupata au kufaidika na uongozi uliotukuka wa mwaka mmoja ili zifanye kazi kwa ufanisi!!! Hawa watu sijui wanatuonaga hatunazo!!!! Unafiki una tabia moja nao ni kusahausahau msimamo wako!
 
  • Thanks
Reactions: MTK

Ndg yng mwenye chongo haoni kengeza!
 
Back
Top Bottom