RUCCI
JF-Expert Member
- Oct 6, 2011
- 1,702
- 1,716
Mwinjilisti wa Kanisa la Waadiventisha Wasabato, Yese Mileyi (50) ameuwawa kwa kuchomwa mishale miwili na watu wasiojulikana ambapo mshale mmoja ulimpata shavuni na mwingime mgongoni na kufariki dunia hapo hapo.
Tukio hilo lilitokea Septemba 8 mwaka huu majira ya saa 1:14 jioni katika Kijiji cha Mahando mterini, Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro.
Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Fulgence Ngonyani amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mwinjilisti huyo alikuwa anatokea shambani kuelekea nyumbani na kuchomwa mishale hiyo na watu wasiojulikana na kusababisha kifo chake.
Kamanda alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Huruma , huku jeshi la polisi likiendelea kuwasaka waliofanya mauaji hayo.
Katika hatua nyingine jeshi la polisi limewataka wananchi wa Moshi kufanya siasa za amani na utulivu na kuacha kuchana picha za wagombea walizo zibadhika katika sehemu mabalimbaliza mkoani humo.
Kamanda Ngonyani alisema kumekuwapo na matukio mengi yanayoripotiwa na wagombea wakiwashutumu baadhi ya wananchi kuchana mabango pamoja na picha za wagombea.
Chanzo: Mwananchi