Mwili wazuiwa Hospitali ya Mwananyamala baada ya kugundulika una Dawa za Kulevya

NGolo Kante

Member
Feb 28, 2017
80
131
Dar es Salaam. Mfanyabiashara Happy Mboya (38) amefariki dunia katika hospitali ya Mwananyamala na mwili wake kuzuiwa kutoka baada ya kugundulika kuwa na dawa za kulevya.

Happy alifariki dunia Jumapili ya Desemba 16 na mwili wake ulipangwa kusafirishwa jana kwenda Moshi kwa mazishi leo.

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Rogers Siyanga alisema jana kuwa Polisi wa Kituo cha Osterbay jijini hapa wamechukua mwili wa marehemu na kuupeleka katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Alisema ameshatuma maofisa wake katika hospitali hiyo ili kufuatilia kwa karibu tukio hilo ikiwa ni pamoja na kupata taarifa za kina ikiwamo aina ya dawa alizomeza na kiasi.

Siyanga alisema baada ya uchunguzi kukamilika, atatoa taarifa kamili juu ya tukio hilo.

Wakati Siyanga akisema hayo, Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Jumanne Muliro alipoulizwa kuhusu suala hilo alitaka apewe muda ili kufuatilia.

“Ndiyo nasikia kwako ila naomba nipe muda nitakujulisha ukweli wa suala hili,” alisema Muliro.

Akizungumza jana, baba mdogo wa marehemu, Ally Bilali alisema baada ya kurejea nchini, Happy alifikia katika nyumba ya kulala wageni ambayo haikufahamika na mtu mwingine isipokuwa mume wake.

“Hata dada yake alikuwa hafahamu kuwa amesharudi kwa sababu alidai kuwa simu yake imeharibika na wasingeweza kuwasiliana kumbe ilikuwa kumficha. Alipata taarifa baada ya mdogo wake kuzidiwa na wahudumu kumpigia simu ndipo alienda kumchukua kumuwahisha hospitalini,” alisema.

Alisema baada ya kufika hospitalini na kupimwa, alionekana kuwa na njaa kali jambo ambalo lilimlazimu daktari kumuandikia dripu za maji ili kumsaidia.

“Lakini hizo dripu hakuwekewa na hatukuambiwa sababu ya msingi hadi alipofariki. Taratibu za kusafirishisha mwili kwenda Moshi zilipofanyika ndiyo tuliambiwa kuwa hatuwezi kutoa mwili kwa sababu una dawa za kulevya.

Alimtuhumu mume wa marehemu kuhusiana na tukio hilo huku akidai kwamba tayari anashikiliwa na jeshi la polisi.

Bilali alisema Happy ambaye ameacha watoto wawili, alikuwa mkazi Sinza na mfanyabiashara kati ya India na China. Hata hivyo, hakubainisha aina ya biashara aliyokuwa akifanya katika mataifa hayo.
 
Yaani mtu akifikia hatua ya kukubali kufanya biashara hii, tena kuwa punda hakika tamaa inakuwa imezidi uwezo wake wa kufikiri!
 
Amekufa wakati kodi yetu ajalipa?! Biashara yote hiyo aliyofanya..!
 
Back
Top Bottom