Mwili wa Binadamu unavyo fanya kazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwili wa Binadamu unavyo fanya kazi

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Oct 17, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 17, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Binaadam ameumbwa akiwa mwenye uwezo wa kumudu kufanya mambo mbali mbali kwa kutumia mwili wake. Mwili wa binaadam umegawika katika viungo tofauti: Kuna viungo vya kutoa sauti (Vocal), kuna viungo vya kusikia (Audio) kuna viungo vya kuonea(Visual) na kuna viungo vinavyomuwezesha kujisogeza huku na huku (Mobile). Zaidi ya yote hayo kuna ubongo ambao unadhibiti na kurekebisha mwendo wa viungo vyote (Central Organism) pamoja na kuwa na uwezo wa kupokea habari, kuzihifadhi, kuzichambua, kufikiri na kubuni.

  Ubongo wa binaadam ni sehemu ya muhimu ya mwili ambao ndio unamuongoza yeye, sio tu katika kudhibiti nafsi bali katika kutekeleza jambo lolote analotaka kulifanya ama kwa mwili wake au kwa kutumia akili yake.

  Viungo vya mwili wa binaadam vina kazi mbili kubwa:

  1. Sensory Motor: Kupokea taarifa na kuipeleka kwenye ubongo. Ubongo huichambia taarifa na kuichukulia hatua au kuihifadhi.

  2. Psycho Motor: Uwezo wa viungo kufanya kazi mbali mbali baada ya kuamrishwa na ubongo itekeleze kazi hio.  MAISHA YA BINAADAM NA MAZINGIRA YAKE

  Maisha ya mwanadam hupita katika daraja 5 muhimu nazo ni :-


  a) Misha ya tumboni kwa mama.
  b) Maisha ya mikononi kwa mama.
  c) Utoto.
  d) Utu uzima.
  e) Uzee

  a) Maisha ya Tumboni kwa Mama


  Mtoto hufanyika wakati wa mbegu ya mwanamme inapokutana na mbegu ya mwanammke. Baada ya kufanya tendo la ndoa katika kipindi cha dakika 15 hadi 30 tangu manii ya mwanamme kumuingia mwanammke, mbegu za uzazi za mwanamme hufika katika ua la uzazi la mwanammke lililochanua ambalo kawaida huchanua katika kipindi cha wiki moja na nusu tangu kumaliza hedhi. Katika kipindi hicho mbegu ya uzazi ya mwanamme ikimuingia mwanammke na kufika kwenye ua, mwanamke atashika mimba.

  Katika kipindi cha saa 24, mbegu ya uzazi ya mwanamme hupenya ndani ya mbegu ya mwanammke, na kwa muda wa siku 7 mbegu hugeuka na kuwa tonge la damu.

  Katika kipindi cha mwezi mmoja tonge la damu hukuwa na kuwa pande zito la damu na huziba mfereji wa kupitia damu ya hedhi.

  Kidogo kidogo pande hilo la damu hugeuka na kuwa pande la nyama, katika kipindi cha siku 40 pande la nyama huwa kiumbe chenye uhai wake wala sio sehemu ya umbo la mama. Kiumbe hicho hupata chakula na hewa kutoka kwa mamayake, kidogo kidogo kiumbe hicho hukua na kutoa sehemu nyengine za viungo vya mwili wake. Katika kipindi hicho mtoto huanza kuota mishipa yake ambayo ndio inayomuwezesha kuota sehemu tofauti za viungo vyake na hatimae mishipa ambayo hupitisha chakula katika sehemu za viungo hugeuka na kuwa mifupa. Mpaka kumalizika siku 90, viungo vyote vya mtoto vinakuwa vimeshakamilika kuumbwa.

  Katika hatua inayofuata mtoto hukuwa na kuanza kucheza kwa kuhangaika au kujivuta vuta akiwa katika fuko la uzazi. Kwa kufanya hivo mtoto anapata nafasi ya kuchezesha mwili wake na huzidi kukuwa.

  Baada ya kupindi cha pili cha siku 90 kumalizika, (Allah S.W) Mwenyeezi Mungu humleta malaika ambae huja na kitabu na kuandika mambo yote amabayo anayoyaahidi kuyatekeleza wakati atakapoletwa ulimwenguni tangu kuzaliwa hadi siku ya kufa. Kila kitu kinaandikwa katika kitabu.

  Katika kipindi hiki mtoto hujitayarisha kuja ulimwenguni na inapofika siku 45 tangu alipojiwa na Malaika, (Allah S.W) Mwenyeezi Mungu humleta Malaika kwa mara nyengine tena ambae kwa mara hii humtoa uhai wake kwa siku 15 ili mwili wake uwe tohara kutokana na madhambi ya mama yake. Kwani kwa muda wote alioko tumboni alikuwa akiishi kama ni sehemu ya mamayake na alikuwa akila chakula kinachotokana na mamayake, chakula ambacho kinaweza kuwa kimechumwa kwa njia ya halal au kwa njia ya haram.

  Baada kutoharishwa, Mwenyeezi Mungu humleta mtoto duniani akiwa tohara hana madhambi yoyote.
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Oct 17, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  MAISHA YA BINAADAM NA MAZINGIRA YAKE

  Maisha ya mwanadam hupita katika daraja 5 muhimu nazo ni :-

  a) Misha ya tumboni kwa mama.
  b) Maisha ya mikononi kwa mama.
  c) Utoto.
  d) Utu uzima.
  e) Uzee

  b. Maisha ya mikononi kwa mama:


  Isipokuwa katika jamii ya viumbe vyenye kubadilika badilika umbo mpaka kufikia hatua ya utu uzima ambapo hupata umbo la kudumu linalofanana na jamii yake, wanaadamu ni viumbee pekee ambavyo wanapozaliwa huwa hawajiwezi wala kujimudu kwa jambo lolote.
  Watoto wachana huwa hawajui kitu wala hawawezi kujisaidia jambo lolote, kila kitu wanataka wapangiwe na kufikiriwa. Mtoto huwa anahitaji mapenzi na huruma.

  Kidogo kidogo mtoto huanza kusoma watu wake wa karibu nae huweza kubagua watu tofauti na kumjua mama yake. Wakati wote mtoto anajifunza mambo mbali ya kujitahidi kupambana na hali ya kutegemea watu. Kila anapopata uwezo wa kujifunza kitu kipya basi hufanya hivyo

  bila kuogopa kuumia. Kwa njia hiyo hujifunza kukaa, kutambaa, kusimama na kukimbia. Wakati huo huo huwa anajifunza kusema na kufahamu mambo yanayofanyika katika mazingira yake.
  Baada miezi 24 tangu kuzaliwa uchanga wa mtoto humaliza kwa kuachishwa mziwa.

  c. Utoto:

  Tofuti na viumbe vyengine wanaadamu huwajibika kuwalea watoto wao kwa kuwafundisha heshima, adabu, desturi na namna ya kuishi na watu katika. Watoto wanahitaji kulishwa chakula bora chenye afya ili kuifanya mishipa yaO ya fahamu iwe mepesi katika kufahamu mambo, na kusomeshwa lengo la maisha wakiwa bado wadogo ili waweze kujiandaa na safari ndefu ilio mbele yao. Safari ambayo itawabidi wapambane nayo bila ya masaada wa watu wengine.

  Katika kipindi cha utoto akili ya watoto huwa kama kioo inakamata kila kitu wanachokiona na kusomeshwa, lakini sehemu ya ubongo wao inayohifadhi, kutunza habari mbali mbali na kufanya uchambuzi wa mambo huwa haijakuwa kiasi cha kuwa na uwezo wa kuyaweka yote wanayosomeshwa au kuyaona. Ili ubongo ufanye kazi lazima ufanyiwe mazoezi ya mara kwa mara mpaka taarifa inayoipokea iweze kuganda

  kama smaku. Kupata mazoezi hayo panahitajika kufanywa mpango maalum wa mafunzo. Ni wajibu wa wazee kuwapa mafunzo watoto wao ili wapate elimu waweze kupambana na mazingira wanayoishi na kufahamu lengo la maisha la kuwa wameumbwa na Mola wao kuja kumuabudu si mwengine isipokuwa Allah S.W moja tu. Mola wa Haki na kujiandaa na siku ya marejeo.

  d. Utu Uzima:

  Katika Kipindi ambacho mtoto amaekuwa mtu mzima na kuanza kujiendesha mwenyewe bila ya kutegemea wazazi, kipindi hiki ni kipindi cha mtihani mkubwa wa maisha. Wakati huu viungo vinakuwa vimekakamaa na vyenye uwezo wa kufanya kila kazi.

  Mazingira anayoyaishi yana mchanganyiko wa mambo ya kila aina. Wako watu wema na wabaya, kipindi hiki ni kipindi cha kuendeleza mambo yote ambayo alipokuwa mtoto alifunzwa na wakati huo huo awafunze watoto wake. Wakati huu mtu anatakiwa awe raia mwema, mwenye tabi nzuri anaekubaliana na jamii na kuwa mstari wa mbele katika kupigania na kuendeleza mambo yote yenye manufaa kwake na watu wengine na kujiepusha na vishawishi na shetani.
  Ikiwa alipata malezi mema utotoni basi bila mambo atakayoyfanya utu uzimani yatalingana na malezi yake.

  e. Uzee:

  Kipindi cha mwisho wa safari ya mwanadam ulimwenguni ni kufikia hatua ya uzee. Viungo vinakuwa vimechoka, cells neurones enzymes na vyote hivo huwa vimekwisha nguvu protein inapungua katika mwili, protein ikipungua na nguvu zikiisha husababisha Memory ya akili kupungua kuhifadhi mambo na yale yaliyohifadhika huwa yanasahaulika. Katika hali ya uzee ni hali sawa na ya mtoto mchanga.

  Watoto ambao wamebahatika kuishi na wazee wao hadi kufikia hatua hiyo inawapasa wao sasa kuwalea wazee wao kama walivolelewa wao wakati walipokuwa wachanga, wanatakiwa wawe wapole wasiwakemee. Na wakati wote waoneshe huruma kama vile hapo mwanzo wazazi wake walivokuwa na huruma na mapenzi juu ya mtoto wao mchanga. Waombee dua wazee wako na uwaombee rehma, kwani sasa ni wakati wako wewe mtoto kumlea mzee wako.

  Mwenyezi Mungu anatuambia katika aya ya 23 mpaka 25 Surat Bani Israel haya yafuatayo:
  " Na Mola amehukumu kuwa msiabudu ila yeye tu. Na ameagiza kuwafanyia wema wazazi wawili. Kama mmoja wao akifikia uzee, naye yuko pamoja nawe au wote wawili basi usiwaambie hata aah na wala usiwakemee. Na useme nao kwa lugha ya heshima"
  "Na uwainamishie mbawa kwa unyenyekevu na kuwaonea huruma (kwa kuwaona wamekuwa wazee). Na useme "Mola wangu warehemu wazee wangu kama walivyonilea mimi"
  " Mola wenu anajua sana yaliyo ndani ya nyoyo zeni. Kama mkiwa wema (kwa wazee wenu), yeye ndie mwenye kusamehe makosa ya wote wenye kurejea kwake.
   
Loading...