Mwili wa aliyefukiwa mgodini waopolewa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwili wa aliyefukiwa mgodini waopolewa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Mar 12, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 12, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Hatimaye mwili wa mtu mmoja kati ya watu saba wanaohofiwa kufa katika moja ya mashapo (mashimo) yaliyopo katika mgodi wa dhahabu wa Geita baada ya kuingia kwa lengo la kuiba mawe yenye madini ya dhahabu, umeopolewa ukiwa unaelea.
  Mafanikio hayo yamekuja baada ya siku nne mfululizo za kusaka miili hiyo lakini inadaiwa mazingira magumu, na mvua iliyokuwa

  inaendelea kunyesha siku za hivi karibuni ni baadhi ya kikwazo kikubwa kilichokuwa kinalikabili zoezi la uokoaji.
  Ofisa Madini Mkazi Wilaya ya Geita, Mhandisi Abdallah Sementa, anayeongoza zoezi hilo kiufundi amethibitisha kuopolewa kwa mwili wa mtu mmoja na kumtaja kuwa ni Advetus Leonard (22) mkazi wa kijiji cha Kuhamba wilayani Muleba mkoani Kagera.

  'Tukio hilo limetokea siku nne zilizopita baada ya watu wanaodaiwa kunusurika katika ajali hiyo kudai kuwa wenzao wengine saba walisukumwa na kiifusi cha udongo baada ya kukatika kutoka sehemu waliyokuwepo wakijaribu kuvunja miamba ya mawe ndani ya shapo (shimo) hilo kwa ajili ya kupata dhahabu.

  Waliongeza kuwa wakiwemo humo ghafla sehemu kubwa ya kifusi kilichochanganyika na miamba na mawe makubwa kilikatika na kuwasukuma watu wengine waliokuwemo humo nao wakiiba kwa kujaribu bahati yao hadi katika kina kirefu cha shapo hilo linalodaiwa kuwa na urefu kati ya zaidi ya mita 60.

  Inadaiwa kuwa watu hao kwa nyakati tofauti waliiingia ndani ya shapo hilo ambalo limechimbwa kwa mzunguko mithiri ya uwanja wa mpira kwenda chini kwa utenganisho wa vituo tofauti limejaa maji kuazia umbaili wa mita 20 kutoka uswa wa ardhi na mita zingine zaidi ya 40 zinazobaki kwenda chini zimejaa maji.

  Matukio ya majaribio ya wananchi kuingia kwa nguvu mgodini humo kwa lengo la kuiba mawe limekuwa kama jambo la kawaida katika mgodi huo hatua ambayo imekuwa inawalazimu wakati mwingine walinzi wa mgodi huo kutumia nguvu kuwazuia wanaoingia kwa lengo la kuziuia uhalifu na ajaili kama hiyo.  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

  Poleni sana Wafiwa


   
Loading...