Mwili kuvimba baada ya kula (hives)

Gushleviv

JF-Expert Member
Mar 14, 2011
3,431
5,132
Habari wadau wa Jukwaa hili,

Nimekuwa nikisumbuliwa na tatizo la mwili kuvimba mara nyingi ninapomaliza kula chakula uvimbe ninaoupata ni mithili ya mtu alietembelewa na mdudu.

Nimefuatililia na kugundua aina ya uvimbe ninaoupata kitaalamu unaitwa "HIVES". lakini pia wakati flani huwa inatokea navimba mdomo na kuwashwa sana tatizo hili nimekuwa nalo muda mrefu sana tafadhali naomba msaada wa tiba au ushauri wa namna ya kukabiliana na tatizo la Mzio (Allergy) huu.

Natanguliza Shukrani zangu za dhati.

index.jpg
M3200466.2e16d0ba.fill-920x613.jpg
 
polee! huwa unavimba unapokula chakula cha aina yoyote au ?
Asante, kusema ukweli ni vyakula mbalimbali. mwanzo nilidhani vyakula vya kukaanga (fried food) lakini baada nikagundua kuwa ni zaidi ya hapo.
 
Asante, kusema ukweli ni vyakula mbalimbali. mwanzo nilidhani vyakula vya kukaanga (fried food) lakini baada nikagundua kuwa ni zaidi ya hapo.
nenda hosptl kwa msaada zaidi,huenda kuna kitu una allergy nacho ktk hivyo vyakula! mf mafuta yanayotumika wakt wa kupikia n.k
 
Asante, kusema ukweli ni vyakula mbalimbali. mwanzo nilidhani vyakula vya kukaanga (fried food) lakini baada nikagundua kuwa ni zaidi ya hapo.
mimi tatizo hilo ninalo kama nitakula kamba au nikimeza vidonge vya hedex na asprin, sijaenda hospital ila situmii vitu
 
Habari wadau wa Jukwaa hili,

nimekuwa nikisumbuliwa na tatizo la mwili kuvimba mara nyingi ninapomaliza kula chakula. Uvimbe ninaoupata ni mithili ya mtu alietembelewa na mdudu. nimefuatililia na kugundua aina ya uvimbe ninaoupata kitaalamu unaitwa "HIVES". lakini pia wakati flani huwa inatokea navimba mdomo na kuwashwa sana. Tatizo hili nimekuwa nalo muda mrefu sana.
Tafadhali naomba msaada wa tiba au ushauri wa namna ya kukabiliana na tatizo la Mzio (Allergy) huu.

Natanguliza Shukrani zangu za dhati.

View attachment 1048425View attachment 1048426
Hebu kula vyakula jamii ya mboga mboga tu, yaani nafaka na majani na matunda na nuts na legumes tu, usitumie nyama, mayai, maziwa, sugar na oils, then ujiwa poa njoo uni tag tena.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante kwa ushauri mkuu, je kuna hospital yoyote unaifahamu kuna mtaalamu mzuri wa allergy?
Regency wako vizuri sana, wana maspecialist wa masuala ya ngozi. Utapata matibabu vizuri kabisa..
Kama una bima ya Afya (NHIF) itakua rahisi kwako kuweza kumudu gharama za pale.
Specialist wa ngozi anapatikana siku za Jumatano na Alhamisi.
Wahi mapema asubuhi upangiwe appointment mapema na daktari

Asante sana ndugu, nitajitahidi wiki ijayo niwahi pale.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom