Hadi Team Mamvi wametulia hawathubutu kuleta vurugu ... kweli kimeeleweka leo.
Binafsi Huyu bwana nimemsikiliza tangu mwanzo, amekuwa makini sana tofauti na wagombea wengine. Mfano, ameepuka kufanya upuuzi uliofanywa na wenzake, ambapo Lowasa alimkosoa na kumkejeli Kikwete, na Wasira alitumia muda mwingi kumkosoa Lowasa na kumkejeli. Tusisahau hawa wote ni chama kimoja, hoja ndio kitu cha msingi.
Nimekoshwa sana na jinsi anavyochambua hoja, anajua kinachoendelea ndani ya serikali, anajua vikwazo vya kutatua, anajua mbinu na bila shaka hizi mbinu ziko jikoni tayari ila hakukuwa na uthubutu. Hapa ni hoja, nia, na uthubutu.
Huyu bwana historia yake funika mbovu, sidhani kuna atakaemsogelea maana historia hii inawagusa wapiga kura wengi wakiwemo akina mama na vijana.