acha matata
Senior Member
- Jan 5, 2011
- 165
- 39
Nikiri kuwa mimi ni mwana-ccm niliyehama chama kwakutupa kadi kapuni baada ya kuona chama kimetekwa na mafisadi. Wapo wengi sana wanamna hiyo ninaowajua.
Pia nikiri kuwa mimi ni miongoni mwa watu waliotokea kumchukia Mwiguru Nchemba alipojitoa ufahamu na kusemekana kupanga mipango ovu juu ya vyama pinzani vya ccm hasa hasa CHADEMA.
Kwasiku za karibuni, Mwiguru amekuwa akijipambanua kwahoja nzito na zenye mashiko kwa umma. Hata hivyo, nimekuwa nikiendelea kuwa na mashaka.
Leo nikisikiliza hotuba yake na kuilinganisha na ya Lowasa, Nchemba ameendelea kuwa na hoja za mashiko kama kweli zikitekelezwa. Hoja kama za 1. Makao makuu kuhamia Dodoma; 2. Mbinu za kuinua viwanda vya ndani 3. Mbinu za kuongeza ajira; 4. Kurekebisha mifumo ya ajira kwenye utumishi ya umma;
Walio wengi wetu tulimsikia jana Mh. Ngoyae Lowasa; ambaye inasemekana watanzania wengi matumaini yao yako kwake (!!??). Binafsi sikupata ramani kamili na njia mbadala atakazotumia kuufikisha umma wa watanzania Kwenye nchi ya uchumi wa kati. Angalau nimeiona kwa Mwigulu Nchemba.
Napenda kujifunza kutoka kwa wenzangu.
Nawasilisha
Kwani yupo chama gani?
Mimi pia aisee. Naomba nianzishe group ya kumsaport
Sidhani kama kusema ni ishu...Bali kasema nini ndo jambo la msingi.. Kuhamia Dodoma my footMwigulu Nchemba amethubutu kusema kuhusu katiba na kwenye escrow amesema
Hao akina lowasa walikuwa bubu
Well done Nchemba hutashinda ilaumeonyesha njia

Nadhani ni mapema kusema kuwa hatashinda. Kama kweli tumeona anaonyesha njia, tusimame nyuma yake. CC ya chama ina watu wenye busara na watasikiliza maoni ya wananchi. Wakisikiliza maoni yao wenyewe, pia watampa kura zao wenyewe huyo wanayeona onawafaa hadi zitoshe kumpa urais
......Nyambafuuu!! Mtu kaiba jina la mtu mwingine na hadi leo analitumia bila ya aibu, hii inamaanisha kuwa huyu jamaa ni mwizi, kigeugeu na haaminiki mpaka ameamua kujikataa mwenyewe.Nikiri kuwa mimi ni mwana-ccm niliyehama chama kwakutupa kadi kapuni baada ya kuona chama kimetekwa na mafisadi. Wapo wengi sana wanamna hiyo ninaowajua.