Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Waziri Mkuu wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, amewatahadharisha Watanzania juu ya ukopeshaji wa fedha usio rasmi, maarufu kama "Kausha Damu," akitaja kuwa ni mfumo wa kinyonyaji unaowadumaza wananchi kiuchumi.
Akizungumza jijini Dodoma leo, Februari 5, 2026, wakati akizindua mitaji ya shilingi bilioni 200 kwa ajili ya makundi mbalimbali, Dkt. Mwigulu amewahimiza wananchi kukimbilia taasisi rasmi za kibenki ambazo zina riba nafuu na zilizodhibitiwa kisheria.
Waziri Mkuu amebainisha kuwa dhana ya kwamba mikopo ya "Kausha Damu" haina masharti magumu ni upotoshaji, kwani riba zake ni kubwa kiasi cha kumfanya mkopaji kuwa mtumwa wa madeni badala ya kuleta maendeleo.
Dkt. Mwigulu amezitaka taasisi za kifedha kufanya mageuzi katika utoaji wa mikopo midogo, ikiwemo kupunguza idadi ya kurasa za mikataba ambazo zimekuwa zikiwaogopesha wakopaji wadogo. Ameshauri benki kutengeneza mifumo rahisi ya kujiunga na huduma hizo ili kuwavuta watu waliokuwa wakikimbilia utaratibu usio rasmi.
Waziri Mkuu amemuelekeza Waziri wa TAMISEMI kuhakikisha wakuu wa mikoa wanachukua hatua kali dhidi ya watu wanaofanya ukopeshaji wa kinyonyaji kwenye maeneo yao. Aidha, ameelezea masikitiko yake kuwa hata watumishi wa umma, wakiwemo wa Benki Kuu, wamekuwa wakijiingiza kwenye mikopo hiyo kutokana na mazoea na uoga wa benki.