Dr. Mwigulu Nchemba
Minister
- Feb 25, 2012
- 419
- 2,168
Ndg wana JF salaam?
Nimelazimika kuja hapa kuweka jambo hili sawa. Nimeona uzi unaoongelea kuwa mimi na mhe Nchimbi tumewashitaki vijana hao waliojitaja kwa kuingilia mawasiliano. Naomba kuweka wazi kuwa
1) Sijawahi kuwasiliana na mhe Nchimbi kwa E mail hata siku moja tangu nizaliwe.
2) Sijapeleka lalamiko la mambo hayo polisi wala vyombo vyovyote vya dola wala vya habari
3) E mail ilibandikwa ikionesha mimi nawasiliana na Nchimbi wala sio e mail yangu wala haijawahi kuwa e mail yangu.
4) Sikuwa hata na sababu ya kuwasiliana na Mhe Nchimbi kwa E mail kwakuwa muda mwingi tuko wote bungeni, kwenye vikao vya chama na mjini.
Inawezekana ni kweli vijana hawa wameitwa polisi, basi kama ndivyo, watakuwa wameitwa kwa kutengeneza e mail kwa majina ya viongozi, kutunga ujumbe wao na kutengeneza kama vile viongozi wamewasiliana na kuusambaza kwa lengo baya la kutaka kuchafua taswira za viongozi mbele ya umma. Hii ni tabia mbaya kabisa na vijana wa aina hii ni mizigo kwa Taifa.
Naunga mkono polisi wafuatilie uzushi na ujinga huo wa watu kutengeneza e mail bandia, mawasiliano feki na kusambaza kama ndio mawasiliano halali ili umma upokee matope waliopanga kupakazia viongozi. e mail yangu iko kika mahali kwenye business card zangu.
Nalaani kitendo chao cha kubandika e mail batili, mawasiliano batili na kusambaza kwenye mitandao, nalaani pia kwa kutokuwa wakweli kama wameitwa kwa kuandaa e mail feki na mawasiliano feki wanakuja huku kuripoti kuwa wameingilia mawasiliano. yapi? Sio e mail yangu, wala sijawahi kuwasiliana na Nchimbi kwa e mail. E mail yangu inafanya academic issues, nawasiliana na supp wangu wa PhD na wanazuoni wengine kwa academic issues.
Ben, look at you?
MAJIBU ya BEN SAANANE

Mwigulu Nchemba,
-Nilichoulizwa Polisi mbele ya mwanasheria wangu ndicho nilichoripoti.
-Sasa kama una updates nyingine it's none of my business
-Pia kumbe kuna vijana waliojitaja kuwa wameingilia mawasiliano?Sasa kulikua na haja gani ya Jeshi la polisi kuniita kama wapo vijana wa aina hiyo ?
-Pia barua pepe hizi zilisambaa kwa kasi kwenye mitandao hata kwenye Thread yako uliyoanzisha tarehe 26.11.2013 .Hukutoa ufafanuzi
-Thread ilipoanzishwa ili utoe ufafanuzi ulikaa kimya now one month.Nilikutumia SMS utoe Ufafanuzi maana watu wataamini ni ukweli.Ukakaa kimya.
-Nilishtuka sana waliponiuliza ulipata wapi password ya Nchimbi.Pia niwasaidie kumjua aliyeweka Jamiiforums na kwenye mitandao.Na pia lengo langu la kuanzisha thread (Ku-recreate kwa maneno yao)ni nini?
-Sasa polisi niliwaambia wao watafute ni nani aliingilia mawasiliano hayo ambayo tulikubaliana ni kinyume cha sheria.Pia watafute chanzo na sehemu ambazo mawasiliano hayo yalipita maana lengo la kuanzisha thread kwa kufanya Copy and Paste ya kilichokua kinazunguka ni kuhakikisha wahusika ambao majina yanayofanana na ya Nchimbi na Mwigulu walitakiwa kutoa ufafanuzi na wewe ulikua online.Thread ilianzishwa at 13:51 na kisha masaa matatu baadae nikaona kimya kimezidi nikakutumia SMS wewe na Nchimbi ambao majina yanayofanana na yenu yalihusishwa .Niliwatumia SMS masaa 3 baadae exactly.Nitaiweka hapa na hata polisi niliwaonyesha kwa kuwa bado ipo ndani ya simu yangu na nilishaichapisha
Polisi walisema pia bado watamhoji Mhe. Nchimbi.Sijui kwanini so far haujahojiwa na Polisi
"Ben,Look at you.!"-By,Mwigulu Nchemba. (Sijui unamaanisha nini)
SMS niliyotuma ni hii
" Hon'ble Nchimbi,
Mawasiliano ya Barua pepe yanayoonyesha kati ya jina la Emmanuel Nchimbi na Mwigulu Nchemba kama yanavyosambaa JamiiForums na Mitandao mingine ya kijamii yanayoainisha njama ovu dhidi ya CHADEMA ni za kweli?Muda wote wahusika mmekaa kimya bila ufafanuzi sasa nimeanzisha thread ili mtoe ufafanuzi.Vinginevyo tutaendelea kuamini ni ukweli.
Mh.Mwigulu nawe umekua kimya pamoja na kuwa member wa JF na Facebook.Ben Saanane
CC:Mwigulu '"