Mwigulu: Serikali imeshalipa fedha za miradi, wakandarasi waliokimbia bila kulipa wafanyakazi watafutwe na wakamatwe

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,498
Waziri Mkuu, Mwigulu Nchemba Machi 13, 2026 akizungumza na wananchi wa eneo la Majalila, Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi, amesema Serikali tayari imeshalipa fedha zote za utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayoendelea katika maeneo mbalimbali.

"Kila eneo ambapo mradi unatekelezwa Serikali imeshalipa fedha za mradi huo, wale wanaofanya kwenye miradi hiyo, mafundi, vibarua wapate malipo yao, hii habari ya Watu wanafanya kazi wanaendelea kunung'unika huku Serikali ikiwa imeshalipa fedha zote za miradi ya maendeleo halikubaliki, hii inagombanisha Serikali na Wananchi."

"Mkuu wa Mkoa waambie hawa wanaosimamia miradi yote wa waandikie wakandarasi sitaki kusikia wananchi wanadai fedha kwenye mradi ambao Serikali imeshalipa. Kama wapo wanaodaiwa na wengine miradi imeshakamilika wameondoka na fedha za Wananchi, mtume kamanda wa polisi wa mkoa awasiliane na makamanda wenzao wawatafute popote walipo wakamatwe wasiwe huru mpaka watakapolipa fedha ambazo wanadaiwa."

Mhe walipe,maana hali imekuwa ngumu sana.
 
Inaonekana Mhe. PM hana taarifa sahihi

Miradi mingi haijaletewa fedha, Wakandarasi wengi wamekopwa hivyo wengi wapo kwenye hatari ya kufirisiwa na mabenki

Sio vizuri kuongea Siasa Kila wakati hasa unapogusa maslahi ya wengi
Mwigulu ni msanii achana nae yeye aendelee na maigizo yake ila kwa watu tunaomfahamu vizuri wala hata hatusumbui yeye anapenda sifa za majukwaani
 
Yeye ametoka Wizara ya fedha miezi 4 tu iliyopita, anajua kwamba Wakandarasi hawajalipwa ila jukwaani anaongea Siasa za uongo

Miradi mingi ya 2025/26 haijatekelezwa kutokana na ukata

Hadi tunafikia hatuna ya kuuza akina yetu ya dhahabu 🙌
 
Huyo ni muhuni kama wahuni wengine
 
Yeye ametoka Wizara ya fedha miezi 4 tu iliyopita, anajua kwamba Wakandarasi hawajalipwa ila jukwaani anaongea Siasa za uongo

Miradi mingi ya 2025/26 haijatekelezwa kutokana na ukata

Hadi tunafikia hatuna ya kuuza akina yetu ya dhahabu 🙌
Sisi tuko uko kwenye sekta hiyo Mwigulu anapenda sana maigizo na Wakandarasi siku wakijitambua wanasiasa wataacha kuwafanya uwanja wao wa kupatia sifa
 
Inaonekana Mhe. PM hana taarifa sahihi

Miradi mingi haijaletewa fedha, Wakandarasi wengi wamekopwa hivyo wengi wapo kwenye hatari ya kufirisiwa na mabenki

Sio vizuri kuongea Siasa Kila wakati hasa unapogusa maslahi ya wengi
Sahihi anapiga porojo mbele ya kadamnasi ili aonekane anapiga kazi kumbe wapi yeye ndio chanzo cha masaibu yote kwa kuua mfuko wa barabara (Road Fund) kipindi waziri wa fedha sahivi anajitoa ufahamu eti wakandarasi wameshalipwa fedha zote kwa pesa ipi watu wamefilisiwa na taasisi za fedha kisa madeni mali zao zimeishia kuuzwa .​
 
Eti jamani watu wanalia njaa na ukata halafu huyu muhuni anadai wamelipwa pesa zote hakuna kinachodaiwa tuendelee kuwaogopa wanasiasa wa dunia ya tatu tena mwezi mtukufu na kwaresma
 
Mwaka jana miradi yote waliotangaza tarura walilazimika kusitisha kisa madani ya nyuma unatakagaza kazi huna pesa na hujalipa madeni ya nyuma ya watu
 
Inaonekana Mhe. PM hana taarifa sahihi

Miradi mingi haijaletewa fedha, Wakandarasi wengi wamekopwa hivyo wengi wapo kwenye hatari ya kufirisiwa na mabenki

Sio vizuri kuongea Siasa Kila wakati hasa unapogusa maslahi ya wengi
Mheshimiwa PM anaongea kisiasa, wakandarasi wengi wanaiacha miradi kutokana na kukosa malipo serikalini.
 
Wamechagua kuongea uwongo kupitia majukwaa ya kisiasa

Kama ulivyosema, Wakandarasi wengi wametelekeza miradi kutokana na changamoto ya malipo kuchelewa

Hali hii ikiendelea, itapelekea wengi kufirisika
 
Sahihi anapiga porojo mbele ya kadamnasi ili aonekane anapiga kazi kumbe wapi yeye ndio chanzo cha masaibu yote kwa kuua mfuko wa barabara (Road Fund) kipindi waziri wa fedha sahivi anajitoa ufahamu eti wakandarasi wameshalipwa fedha zote kwa pesa ipi watu wamefilisiwa na taasisi za fedha kisa madeni mali zao zimeishia kuuzwa .​
Hii Nchi Kila Kiongozi anaona sawa kuongea uwongo

Yeye anajua hali aliyoiacha Wizara ya Fedha

Kibubu kimekauka hadi wanafikia kuuza akina ya dhahabu

Wakandarasi wanadai

Deni la Taifa limepanda hadi kufikia 107Trilioni

Mifuko ya Kijamii imeishiwa fedha hadi kupelekea Wastaafu kusubiria pension zao hadi kuishia kufa kwa stress

Then PM anakuja hadharani kusema hayo anayosema 🙌
 
Sisi tuko uko kwenye sekta hiyo Mwigulu anapenda sana maigizo na Wakandarasi siku wakijitambua wanasiasa wataacha kuwafanya uwanja wao wa kupatia sifa
Hajui anawatia hasira Wakandarasi kwa kuwasemea uwongo

Tembelea miradi mingi barabarani imesimama kwa kukosa fedha
 
Hii Nchi Kila Kiongozi anaona sawa kuongea uwongo

Yeye anajua hali aliyoiacha Wizara ya Fedha

Kibubu kimekauka hadi wanafikia kuuza akina ya dhahabu

Wakandarasi wanadai

Deni la Taifa limepanda hadi kufikia 107Trilioni

Mifuko ya Kijamii imeishiwa fedha hadi kupelekea Wastaafu kusubiria pension zao hadi kuishia kufa kwa stress

Then PM anakuja hadharani kusema hayo anayosema 🙌
Hawa watu hapana ni kuwakataa na kauli zao za kilaghai siku zote tena aina ya hawa wavaa bendera ndo wakuogopwa vibaya sana matapeli wa mchana kweupwe
 
Mwaka jana miradi yote waliotangaza tarura walilazimika kusitisha kisa madani ya nyuma unatakagaza kazi huna pesa na hujalipa madeni ya nyuma ya watu
Hali mbaya sana kwa wakandarasi tena bora hata Tarura wanalipa kwa kuchellewa kidogo Tanroads wako hoi haijulikani utalipwa lini mpaka imepelekea wengi kutoomba kazi maana ni majanga
 
Hawa watu hapana ni kuwakataa na kauli zao za kilaghai siku zote tena aina ya hawa wavaa bendera ndo wakuogopwa vibaya sana matapeli wa mchana kweupwe
Wametuona Wananchi ni watu wa kudanganyika

Ukipita barabarani humo Kila mahali miradi ya Lami haijakamilika na Wakandarasi hawapo site kisa fedha

Yeye PM anasema wamelipwa 🙌

Kama wangekuwa wamelipwa wangetelekeza miradi yao kweli
 
Miradi mingi mkandarasi yupo site miradi gani mkandarasi ameitelekeza?
 
Back
Top Bottom