Mwigulu Nchemba: Umeihujumu CCM Arumeru? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwigulu Nchemba: Umeihujumu CCM Arumeru?

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by SEBM, Apr 2, 2012.

 1. S

  SEBM JF-Expert Member

  #1
  Apr 2, 2012
  Joined: Mar 7, 2012
  Messages: 496
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Kaka yangu Mwigulu,
  Awali ya yote nikupe pole kwa kupoteza Jimbo la Arumeru Mashariki kwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)

  Kaka, Utakumbuka tangu mchakato wa Kura za Maoni, kulikuwepo tetesi ndani ya CCM kwamba wewe, Nape na wanachama wengine hamkuwa mnamuunga mkono Sioi.Ulikaririwa (haikuthibitishwa0 katika vikao vya ndani kwamba ulikuwa unampiga zengwe la wazi Sioi na hata ulijichomeka katika mchakato wa kura za maoni(ulikanusha hapa JF).

  Kaka, baadaye ndugu Sioi alipata kura zinazomtosha na kumshinda William Sarakikya.Kundi lako kimkakati likaonekana kuwa na nguvu kwani katika halli isiyotarajiwa na wengi, mkapitisha zoezi la kurudia kura baina ya Sarakikya na Sumari ambapo Sumari aliikuka mshindi na kuthibitishwa na vikao vya juu kuwa mgombea wa Ubunge Arumeru Mashariki kwa kupitia CCM.


  Kaka, CCM wakafanya kosa kubwa ambalo ndiyo msingi wa post yangu hii:

  1.Walikuamini, wakakufanya uwe kampeni Meneja; ikiwa na maana wewe ndo msimamizi mkuu wa kampeni, muongoza mikakati na mtu muhimu sana katika kampeni.Ikumbukwe kwamba, miezi michache nyuma uliongoza kampeni kule Igunga na ukafanikisha ushindi.


  2.Kosa la pili ulilolifanya ni kumhusisha Rais mstaafu BWM akatika ufunguzi (na ufungaji) wa kampeni.Ulichokosea ni kutokukubaliana na ukweli kwamba BWM ahana mvuto kwa wananchi wa Tanzania na vile vile, hakukuwa umemuandaa na kukubaliana naye nini cha kufanya.Kosa kubwa hasa ni kufungua kampeni zenu baada ya CHADEMA kufungua za kwao; badala ya kuelezea sera zetu na mnawafanyia nini wananchi(walau miaka michahe baada ya mtangulizi - RIP - kutokufanya chochote), mkafanya mkutano ule kuwa ni sehemu ya mipashao na mijembe.Mkapa akafikia kumsema Vicent Nyerere kwamba si wa ukoo wa Nyerere!Yaliyofuatia baadaye ni historia, lakini yalipoteza credibility ya chama chako.


  3.Kaka, kosa jingine ulilolifanya, ukiwa kama mkuu wa kampeni, uliruhusu uhuni na udhalilishaji mkubwa.Kwamba kitendo cha wewe kuwa jukwaani, ukamruhusu Bwana Lusinde kutoa lugha nzito za kejeli na matusi, huku wadada na wamama wakishangilia, haikuwa ya kiungwana.Wewe ndiyo ulimleta Lusinde na wewe ndiyo ulimruhusu kupanda jukwaani.Wewe ndo ulimtuma atoe yale matusi mazito?Kwa nini haukumkataza?Watu wengi wana audio na video ya maneno yale na wala haukusikika kokote ukikemea.


  4.Kaka, kosa jingine ulilolifanya ni kuruhusu baadhi ya wabunge na makada waandamizi ambao inasadikiwa wako katika kundi hasimu,kupanda jukwaani na kumwombea kura Sioi kwa mbwembwe nyingi wakati inajulikana ni anti Sioi.Swali la msingi: kulikuwa na mantiki kwa Sendeka na Nnauye kupanda jukwani na kumwombea kura Sioi?


  5. Kaka, hili pia linahusishwa na ile hali ya nyie kutokuwa wakweli na waaminifu mbele ya jamii.Kwamba, inazungumzwa kuwa Maji Marefu(Ngonyani), alienda kwenye kambi ya CHADEMA na kutaka kuongea na Mh. Nassari.Lakini haijulikani kulitokea nini, ila kesho yake magazetini(Tanzania Daima na Mwananchi), wakaonekana wakiwa wamekumbatiana huku wakicheka katika hali ya matani kabisa.
  Hamad, Ngonyani akasema alitishiwa kuuawa na wafuasi wa CHADEMA kwa maelekezo ya Nassari na zile picha zilitungwa tu na Mwananchi na Tanzania Daima.
  Hali hiyo ikazua tafrani na mambo kadha wa kadha.Na wachambuzi na wapembuzi wa mambo ya habari na wana intelijensia, wakabisha kwamba ile ilikuwa ni picha ya kirafiki na Ngonyani anaogopa tu kupuuzwa na Makada wenzao.


  Kaka, sababu ni nyingi zinazoniaminisha kwamba ukiwa Mkuu wa kampeni, haukutimiza wajibu wako ipasavyo.Na ndiyo maana nashawishika kusema kwamba kuna dalili za wewe kuwahujumu CCM Arumeru.


  Hongera sana Mh. Joshua Nassari(MB).
  TULIANZA NA MUNGU, TUMEMALIZIA NA MUNGU!
   
 2. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #2
  Apr 2, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,696
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  The ship was doomed to sink, the captain should take all the blame.
   
 3. Avanti

  Avanti JF-Expert Member

  #3
  Apr 2, 2012
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 1,209
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Watanzania tunajua kutafuta mchawi baada ya msiba, hata kama ni msiba wa kawaida tu. nafikiri hii ni asili yetu, huwa hatukubali kiurahisi. Anyway, nawapongeza CCM kukubali kushindwa na CDM Arumeru, wameonesha ukomavu wa kisiasa, naamini ingekuwa CDM wameshindwa wangekataa matokeo.
   
 4. m

  mvunjamiwa JF-Expert Member

  #4
  Apr 2, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 455
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Mpe vipande vyake huyo kijana. anafanya mambo kama mzee bwana. sijui na yeye ameshakuwa kafisadi!!
   
 5. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #5
  Apr 2, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Pole na hongera kwa imani yako........hivi hujamsikia Nape akilalama akidai kuhujumiwa?
   
 6. b

  bangusule Senior Member

  #6
  Apr 2, 2012
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 185
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  SEBM,
  hayo ni makundi hasimu kwenye kugombea madaraka ndani ya CCM. wanapowakabili Chadema wana CCM wote ni kitu kimoja. unashangaa ya Arumeru wakati kwenye uchaguzi wa Igunga Rostam na Nape walikuwa wakipiga kampeni pamoja??
   
 7. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #7
  Apr 2, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Katika kujibu thread zangu Mwigulu alidai kuwa WanaArumeru hawaitaji sera wanahitaji porojo.
  Mzee wa Mamvi naye akaja na Hapo,Hapo Je!
  Aibu hii ni ya CCM Wote!
   
 8. Avanti

  Avanti JF-Expert Member

  #8
  Apr 2, 2012
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 1,209
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Kulalama wakati umekubali matokeo ni ni tofauti na kukataa matokeo. Mtu muungwana anaweza akajua kuwa kahujumiwa, akalalamika lakini akakubali matokeo. Umejiuliza mfano CCM wangektaa matokeo na wakawatangazia wafuasi wao kuwa wamehujumiwa ingekuwaje?
   
 9. K

  Kana Amuchi Member

  #9
  Apr 2, 2012
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Avanti, wafuasi wa ccm wasingeamini maana hakuna kiongozi wa chadema aliongozana na polisi jana kukamata vijana wa ccm na kuwaweka ndani. usidhani wana ccm ni vilaza wote. kwanza ndio waliopiga kura za kumfanya Nasari ashinde. Wangewaacha polisi na huyo ambaye angekataa matokeo wakaenda zao kushangilia ushindi wa mbunge wao Nasari kama walivyofanya jana.
   
 10. U

  Ubongo Silaha Senior Member

  #10
  Apr 2, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 140
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Kuamini CCM imehujumiwa ingekuwa ni kuwa mfinyu wa fikra na wapumbavu tu ndio wangeamini wamehujumiwa.
  1. CCM wana historia ya kuhujumu matokeo, hata ya ndani ya chama; Chadema hawana
  2. CCM wana historia ya kubebwa na dola, hasa polisi; Chadema wasingeweza kufanya hujuma polisi wakiangalia
  3. CCM kwa tabia zao wamejenga taswira ya kutoaminiwa
   • Angalia kwenye kura za maoni; wametuhumiana wao kwa wao kuhujumiana
   • Kama wanaweza kuhujumiana wao kwa wao; hawashindwi kuhujumu vyama vingine
  4. CCM wameanza kutuhumiwa kwa uvunjaji wa amani; tukio la Mwanza ni mfano na Polisi walivyoshughulikia ni uhuni...Linganisha na tukio la Kiwira ambapo walienda kuwaokoa watuhumiwa wa rushwa kivita.
  Mambo yote haya yanafanya iwe vigumu kuamini CCM inaweza kuhujumiwa
   
 11. Bazazi

  Bazazi JF-Expert Member

  #11
  Apr 2, 2012
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 2,029
  Likes Received: 561
  Trophy Points: 280
  Good analysis. Najua Mwigulu Nchemba ni mwanajamvi aje ajibu hoja
   
 12. msadapadasi

  msadapadasi JF-Expert Member

  #12
  Apr 2, 2012
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 504
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  ni kweli kabisa wangeshinda CC=Magamba wangekuwa wameiba kura... wewe tofauti ya kura 6000 mchezo, mie mwenyewe ningekuwa wa kwanza kuanza kupinga eboo... ila Vijibweni sipingi na wala kwa wagogo kule Dododma sipingi...
   
 13. wasaimon

  wasaimon R I P

  #13
  Apr 2, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 222
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM wameshindwa kihalali kabisa kwani ndicho walichokipanda sasa kumtafuta nani mchawi mm nadhani hili ndani ya chama watatafutana wenyewe kwenye mavikao yao huko. Hapa wananchi wa Arumeru Mashariki wameonyesha jinsi gani pesa haiwezi kununua KURA. Hivyo basi hizi ni salamu kwa mjomba kwamba 2015 chama tawala kinatakiwa kijipange kweli kweli. Wananchi hawataki porojo tena bali wanataka vitendo, wameru wasingeweza kukubaliana na uongo uliodhali kabisa wa kurejeshewa ardhi yao kupitia chama tawala wakati wanajua toka Uhuru CCM ndo iko madarakani na wameshindwa kufanya hivyo, hivyo wameamua liwalo na liwe ndo Nasari wameona labda anaweza kuwa mkombozi wao. Nadhani Chama Tawala sasa kiache siasa za kukumbatia wale ambao si chaguo pendwa kwa wananchi. Tatizo ndani ya chama tawala ukiwa mkweli basi unachukiwa na utatengenezewa mizengwe mpaka wahakikishe wamekutoa, hili nalo ni tatizo. Nashukuru na najivunia kuwa Mtz haswa kwa kipindi hiki ambacho demokrasia imeonyesha kushika nafasi yake taratibu hivyo basi ADUI YAKO MUOMBEE NJAA. Akili kumkichwa kwani naambiwa na wahenga eti SIKIO LA KUFA HUWA HALISIKII DAWA sijui ni kweli? Mtanisaidis wahenga.
   
 14. O

  OMEGA JF-Expert Member

  #14
  Apr 2, 2012
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 671
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 60
  My friend Mwigulu: 1.you can fool some people sometimes but you can not fool all the people all the time
  2.Bringing people like Wasira in the modern campaign is like teaching the old dog new tricks.
  3.Always learn to change the game formaty and tactics depending on the team you are playing with,u applied IGUNGA formaty in a different team,the opponent learned your formaty in Igunga,they came prepared,you were not intelligent enough to shift to another formaty
   
Loading...