Mwigulu Nchemba punguza wapambe ongeza washauri

Eroza

Member
Joined
Mar 18, 2015
Posts
39
Reaction score
4
Mbunge wa jimbo la Iramba magharibu napenda kukushauri buuure kabisa, hao watu unaowaita wasaidizi wako ni mizigo na ni kero kwa wapiga kura wako na watanzania kwa ujumla.

Wanafanya kazi ya kukuridhisha wewe na kusahau kwamba wanatakiwa kukusaidia wewe kukuunganisha na wananchi, hawana mikakati endelevu kwa ajili ya vijana wako wa Iramba.

Zaidi ya kujinufaisha wao, wamezoea luxury life na kuwapuuza mpaka nduguzo 2020 usipoliangalia hili utashinda ubunge kwa asilimia 51 tu tena kwa gharama kubwa sana.

Wanairamba wanahitaji watu wa kuwasaidia, tunajua utakuwa bize na shughuli za kiserikali, Unda team work yenye vision na jimbo lako, achana na hao wapambe wanaokuvisha miwani ya mbao.
 
Hao kila jimbo ambalo linaongozwa na ccm wapo. Wanaishi kiujanja ujanja tu
 
Wanawaumiza sana wananchi,dharau kibao..
 
Mdogo wangu Mwigulu, unawasaidizi au unakundi la wapika majungu? At your level nadhani umri wako na elimu yako vinakuwezesha kufanya kazi zako binafsi bila kutaka wapambe. Labda unafanya hivyo kujijengea msingi wa kuwa mmoja wawapika majungu wakubwa by 2020. JITEGEMEE KIUTENDAJI NA KIFIKRA.
 
Mbona hiyo ndo ccm ....wao wako kwaajili ya chama tu.......na matumbo yao
 
Mdogo wangu Mwigulu, unawasaidizi au unakundi la wapika majungu? At your level nadhani umri wako na elimu yako vinakuwezesha kufanya kazi zako binafsi bila kutaka wapambe. Labda unafanya hivyo kujijengea msingi wa kuwa mmoja wawapika majungu wakubwa by 2020. JITEGEMEE KIUTENDAJI NA KIFIKRA.

Ye mwenyewe ni Mtu wa majungu
 
Mbunge wa jimbo la Iramba magharibu napenda kukushauri buuure kabisa, hao watu unaowaita wasaidizi wako ni mizigo na ni kero kwa wapiga kura wako na watanzania kwa ujumla.

Wanafanya kazi ya kukuridhisha wewe na kusahau kwamba wanatakiwa kukusaidia wewe kukuunganisha na wananchi, hawana mikakati endelevu kwa ajili ya vijana wako wa Iramba.

Zaidi ya kujinufaisha wao, wamezoea luxury life na kuwapuuza mpaka nduguzo 2020 usipoliangalia hili utashinda ubunge kwa asilimia 51 tu tena kwa gharama kubwa sana.

Wanairamba wanahitaji watu wa kuwasaidia, tunajua utakuwa bize na shughuli za kiserikali, Unda team work yenye vision na jimbo lako, achana na hao wapambe wanaokuvisha miwani ya mbao.

Inawezekana saaana akazisikia shughuli za serikali redioni na bungeni tu. Huo uhakika wako sijui umeupata wapi!
 
Back
Top Bottom