analysti
JF-Expert Member
- Aug 24, 2009
- 731
- 614
Mara baada ya uteuzi wako, nimekuwa nikifuatilia utendaji kazi wako Muheshimiwa M.Nchemba. Hakika kazi unayoifanya Katika wizara ya Kilimo, mifugo na uvuvi ni kazi ambayo hakika inaweza kutufikisha mahala ambapo kweli kilimo kitakuwa ni uti wa mgongo ulio imara kwa uchumi wetu hapa Tanzania.
Tanzania ni nchi iliyo katika nafasi za mbele kabisa kwa wingi wa Ng'ombe na mifugo mingine hapa duniani, lakini yet ni nchi ambayo sekta hii inachangia kiasi kidogo sana ktk pato la taifa. Hatua ulizozichukua kwa watendaji wa NARCO ni hatua zinazostahili pongezi, kwani NARCO kama ingekuwa imara, na kama ingeongozwa kiuadilifu, hakika taifa letu hivi sasa lisingeitazama secta ya Mifugo kama ilivyokuwa ikitazamwa.
NARCO imekuwa ni kichaka cha watu kujitajirisha, ukifuatilia kwa undani utagundua zaidi ya asilimia 90 ya hao watu uliowasimamisha, wanamiliki ranchi zao binafsi ambazo zimepatikana kwa kuiba mifugo kutoka ranchi wanazoziongoza. Ilikuwa ni desturi wanasiasa kuenda kwenye hizi ranchi na kupewa zawadi za ng'ombe ili waweze kufumbia macho wizi unaotendeka katika mashamba haya.
Muheshimiwa Mwigulu Nchemba, nina hakika kuwa hata wewe walikuwa wameshakupangia kukupatia ng'ombe kadhaa ili kusudi uache waendelee na unyang'anyi wao wa Mali ya Umma, lakini kutokana na uadilifu wako, na msukumo wenye nguvu na mwangwi usiokifani unaotokana na MAGUFULI EFFECT, hakika umeweza kuwatambulisha ya kwamba wizi wa mali ya umma si wakati wake sasa. HONGERA SANA.
Muheshimiwa Mwigulu, naomba sasa uangalie utendaji kazi wa maafisa ugani na maafisa mifugo katika ngazi mbali mbali hapa nchini. Muheshimiwa, hawa watu kama wakitenda kazi ipasvyo, ndio wenye uwezo wa kuibadilisha sekta hii ya kilimo na mifugo kuwa yenye tija kwa wakulima/wafugaji wenyewe na taifa kwa ujumla, na hii itafanikiwa zaidi katika wakati huu ambao nia ya kisiasa ipo dhahiri ila utendaji umeendelea kubaki ule ule wa kasi ya konokono na wizi uliozoeleka. Hali hii ikiachwa iendelee kuwa hivi, pasipo kuwakumbusha majukumu yao, na kuwasimamia watekeleze majukumu yao kwa weledi, hawa maafisa ugani, mifugo, na kilimo hakika watakwamisha juhudi zote uzifanyazo Muheshimiwa.
Mwisho kabisa nakupa pongezi za dhati, na nakuomba ukaze kamba kwani safari bado ni ndefu.

Last edited by a moderator: